Breeder LW Aandika Wimbo wa Milioni 6 YouTube Akiwa Bypass!
Rapper maarufu wa Kenya, Breeder LW, amewashangaza mashabiki wake baada ya kufichua kuwa aliandika na kurekodi wimbo wake maarufu “Dedi Dedilee” kwa dakika 10 tu, akiwa kwenye Barabara ya Southern Bypass, Nairobi. Kupitia Insta Story yake, Breeder alisema kwamba aliuchana au freestyle wimbo huo mzima papo hapo, bila maandalizi maalum. Kulingana naye, hii ilikuwa moja ya nyimbo zilizokuja kwa haraka sana lakini zenye athari kubwa maishani mwake. “Wrote this song in 10 minutes, I literally freestyled everything tukiwa Southern Bypass. One year later, this song changed our lives!!” Tangu kuzinduliwa kwake zaidi ya mwaka mmoja uliopita, “Dedi Dedilee” umevuma kwa kasi na kufikia mafanikio makubwa. Video rasmi ya wimbo huo kwenye YouTube imeshatazamwa zaidi ya 6.3 milioni hadi sasa, ikidhihirisha ukubwa wa ushawishi wa Breeder katika muziki wa kisasa wa Kenya. Wimbo huu umeibuka kuwa anthem ya mitaa, ukichochea mijadala, trends, na changamoto mbalimbali mitandaoni. Mtindo wake wa trap na drill, pamoja na chorus rahisi na ya kukumbukwa, umemfanya Breeder LW kujipatia umaarufu mkubwa. Mashabiki wengi wameelezea kuvutiwa na uwezo wa Breeder kuunda wimbo wa kiwango cha juu kwa muda mfupi, wakimpongeza kwa ubunifu wake wa asili. Kwa sasa, Breeder LW anaonekana kuendelea kung’ara katika game ya muziki huku akiahidi kuachilia kazi mpya hivi karibuni.
Read More