CARDI B APIGA CHINI DILI YA MABILIONI YA PESA, AJITOA KWENYE UHUSIKA WA FILAMU YA “ASSISTED LIVING”
Rapa wa kike kutoka Marekani Cardi B amelipiga chini dili nono lenye thamani ya shilling billion 3.2 za Kenya kwa kujiondoa kwenye nafasi ya uhusika mkuu wa filamu ya ucheshi iitwayo ‘Assisted Living’ ambayo inatayarishwa chini ya kampuni ya Paramount Movies. Kwa mujibu wa tovuti ya Deadline, Cardi anatajwa kuchukua maamuzi hayo kutokana na kuzidiwa na ratiba zake. Cardi B amejiondoa kwenye nafasi hiyo ikiwa ni wiki mbili tu kuelekea siku ya kuanza uzalishaji (production) wa filamu hiyo. Kuondoka kwake kumeleta athari kubwa kwani kampuni ya Paramount Movies imebidi kuahirisha utengenezaji wa filamu hiyo. Hata hivyo wanasema hawajafungua mashtaka kwani wanaamini Cardi B anaweza kurejea tena siku za usoni.
Read More