CINDY SANYU AWACHANA WASANII WALIOTIA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA MUUNGANO WA WANAMUZIKI UGANDA

CINDY SANYU AWACHANA WASANII WALIOTIA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA MUUNGANO WA WANAMUZIKI UGANDA

Nyota wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu amewatolea uvivu wasanii ambao wametia nia ya kugombea wadhfa wa urais wa muungano wa wanamuziki nchini humo kwenye uchaguzi ambao utafanyika hivi karibuni. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Cindy ambaye kwa sasa ni rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda amesema wasanii hao hawana vigezo vya kuongoza muungano huo na badala yake wamuachie nafasi akamilishe baadhi ya miradi ambayo alianzisha akiwa afisini kwa manufaa ya wanamuziki wote. Kauli ya Cindy imekuja mara baada ya kuchukua na kujaza fomu ya kumuidhinisha kugombea tena wadhfa wa urais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda mapema wiki hii. Utakumbuka wasanii kama Daddy Andre na King Saha wametangaza kuwania urais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda na sasa watachuana na cindy sanyu ambaye pia ametia nia ya kutetea wadhfa wake kwa mara ya pili.

Read More
 MUUNGANO WA WANAMUZUKI UGANDA KUFANYA UCHAGUZI KWA NJIA YA MTANDAO

MUUNGANO WA WANAMUZUKI UGANDA KUFANYA UCHAGUZI KWA NJIA YA MTANDAO

Muungano wa wanamuziki nchini Uganda ambao unajiandaa kufanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya mwezi huu wa Aprili umesema utafanya uchaguzi huo kwa njia ya mtandao. Katika mahojiano yake hivi karibuni Rais wa Muungano huo Cindy Sanyu amesema wamechukua hatua hiyo kwa sababu hawana fedha za kutosha kufanya uchaguzi kwa mfumo wa kawaida ambao unatoa nafasi kwa wanachama wao kupiga kura moja kwa moja kwa kujiwasilisha wenye kwenye vituo vya kupigia kura. “Fedha nyingi inahitajika kuandaa uchaguzi kwa njia ya kawaida na kwa sasa hatuna pesa za kutosha,” alisema Cindy. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Local Man” amesema muungano wa wanamuziki nchini Uganda umekosolea vibaya na wasanii kwa hatua yake ya kuendesha uchaguzi kwa njia ya mtandao huku akieleza kuwa wana mpango wa kuandaa uchaguzi wa kawaida kama watapata pesa kutoka kwa wahisani. “Ndio nafahamu watu wengi wanachukulia kupiga kura mtandaoni sio sahihi ila ndio njia pekee ambayo tuko nayo kwa sasa. Lakini ikitokea tumepata pesa kutoka kwa hisani na washirika wengine wa maendeleo, tutafanya uchaguzi kwa njia ya kawaida,” aliongeza Cindy. Cindy Sanyu alichaguliwa kuwa rais wa muungano wa wanamuziki nchini Uganda mwezi Machi mwaka wa 2021 kujaza nafasi ya Ykee Benda ambaye alijiuzulu. Utakumbuka Ykee Benda alichukua nafasi ya Sophie Gombya ambaye alijiuzulu pia na kujiunga na siasa.

Read More
 CINDY SANYU AREJELEA MAJUKUMU YAKE KAMA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA BAADA YA LIKIZO FUPI

CINDY SANYU AREJELEA MAJUKUMU YAKE KAMA RAIS WA MUUNGANO WA WASANII UGANDA BAADA YA LIKIZO FUPI

Staa wa muziki nchini Uganda Cindy Sanyu ametangaza rasmi kurejea kwenye majukumu yake kama rais wa chama cha wanamuziki nchini humo baada ya kuchukua mapumziko mafupi. Kupitia ukurasa wake amepost picha akiwa katika afisi za chama cha wasanii nchini uganda UMA huku akidokeza kuwa yupo tayari kwa ajili ya kuwasimamia wasanii na pia kuweka mikakati ya kuandaa uchaguzi wa chama hicho mwaka huu. Kauli ya Cindy imekuja mara baada ya kukamilisha likizo aliyochukua kwa ajili kumlea mtoto wake aliyepata mwaka huu na mume wake Joel Atiku. Utakumbukwa kabla miezi miwilli kabla ya kujifungua Cindy Sanyu aliruhusiwa kuchukua likizo fupi kama rais wa chama cha wasanii nchini uganda jambo ambalo lilimpelekea kusitisha kufanya shows kama njia ya kujiandaa kumpokea mtoto wake.

Read More