Colonel Mustafa Adai Kuwasaidia Huddah na Noti Flow Kufikia Umaarufu

Colonel Mustafa Adai Kuwasaidia Huddah na Noti Flow Kufikia Umaarufu

Msanii mkongwe wa muziki nchini Kenya,Colonel Mustafa, amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa muda aliowahi kutumia na mastaa wa kike kama Huddah Monroe na Noti Flow uliwasaidia kupenya kwenye anga la umaarufu, wakati walipokuwa bado hawajatambulika sana katika tasnia ya burudani. Akizungumza kwenye podcast ya Alex Mwakideu Live, alisema kwamba mahusiano yake na wanawake hao yalimsaidia kuwapa mwanga wa mafanikio waliokuwa bado hawajaufikia kwa wakati huo. Kwa mujibu wa msanii huyo, jina lake lilihusishwa na mastaa hao kabla ya wao kung’aa, na hivyo mchango wake haupaswi kupuuzwa. Kauli hiyo imeibua hisia mseto mitandaoni. Wapo wanaoamini kuwa Mustafa alikuwa sehemu ya safari ya mafanikio ya Huddah na Noti Flow, huku wengine wakimtuhumu kwa kujitafutia kiki na kutumia majina ya watu maarufu kurudi kwenye ramani ya burudani. Hadi sasa, Huddah Monroe na Noti Flow hawajajibu madai hayo, lakini mashabiki wanazidi kufuatilia kwa makini endapo wahusika watajitokeza kuweka wazi upande wao wa simulizi hii. Mustafa, anayekumbukwa kwa kazi zake akiwa na kundi la Deux Vultures, anaonekana kurejea tena kwenye vyombo vya habari si kwa muziki, bali kwa matamshi yenye utata kuhusu mahusiano ya zamani.

Read More
 COLONEL MUSTAFA ATOA YA MOYONI KUHUSU LEBO YA MUZIKI YA OGOPA DEEJAYS

COLONEL MUSTAFA ATOA YA MOYONI KUHUSU LEBO YA MUZIKI YA OGOPA DEEJAYS

Msanii mkongwe kwenye muziki wa Kenya Colonel Mustafa anazidi kufunguka tusiyoyajua kuhusu lebo yake ya zamani ya Ogopa Deejays. Katika mahojiano yake  hivi karibuni amesema karibu maamuzi magumu ya kuacha muziki baada ya lebo hiyo kuchukua umiliki wa nyimbo zake zote alizowahi kufanya kipindi cha nyuma. Hitmaker huyo wa Katika amesema kitendo hicho kilimuingiza kwenye msongo wa mawazo kutokana na kutofaidi na mirahaba ya nyimbo zake. Lakini pia amemchana dj mkongwe DJ Piye kwa kumbania kucheza nyimbo zake kwenye kipindi cha the beat ambapo ameanda mbali zaidi na kumtaja prezzo kuwa  moja kati ya watu walioua muziki wa kenya kutokana na yeye kutengeneza matabaka miongoni mwa wasnii wa kenya. Hata hivyo amekiri kuwahi kuingia kwenye ugomvi na msanii mwenzake Prezzo kwa sababu ya wanawake ambapo amemuomba  radhi msanii huyo  kutokana na kile kilichotokea kati ya yao. Mustafa kwa sasa yupo mbioni kuachia album yake mpya ambayo hajaweka wazi idadi ya ngoma wala tarehe ya kuingia rasmi sokoni ila ni jambo la kusubiriwa.

Read More
 COLONEL MUSTAFA AMVUA NGUO EX WAKE NOTI FLOW, AMWITA MWIZI

COLONEL MUSTAFA AMVUA NGUO EX WAKE NOTI FLOW, AMWITA MWIZI

Msanii mwenye utata nchini  Colonel Mustafa kwa mara nyingine amedai kuwa aliyekuwa mpenzi wake Noti Flow alimuibia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram. Hitmaker huyo wa ngoma ya ‘Hey Baby’ amedai noti flow alichukua akaunti yake ya Instagram kwa njia ya mabavu kipindi wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi. Akizungumza kwenye the Trend ya NTV  Mustafa amefichua kuwa masaibu yake yalianza wakati alitumia simu ya Noti Flow kuingia kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu alikuwa amepoteza simu yake. Kulingana Mustafa Noti Flow alichukua maamuzi ya kubadilisha kila kitu kwenye ukurasa wake wa instagram bila ridhaa yake na akaanza kuchapisha vitu vyake binafsi jambo lilompelekea kufungua akaunti nyingine. “She stole my Instagram account. Nililog in kwa simu yake, at that time I had lost my phone for  like 2 to 3 weeks, so she wanted to post something aka change email address and everything so akaanza kupost vitu zengine zenye hazinihusu so nikaona hapa tu nikuchorea,” Amesema. “She did not return the account, she took it, she changed it to her fan page so I had to find another one.” Ameongeza Mustafa amesema kitendo cha kuachana na noti flow iliathiri maisha yake kiasi cha kuwafanya wasanii aliokuwa anafanya nao muziki kumpita kisanaa. “I was not in peace…yaani ilifika point nikaona inanirudisha nyuma instead ya kuenda mbele…ata watu nilikuwa nao niliona wananipita,” amesema Mustafa. Hata hivyo ameongeza kuwa yeye na noti flow sio marafiki kwa sasa na hajazungumza nae kwa muda mrefu.  

Read More
 COLONEL MUSTAFA ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA.

COLONEL MUSTAFA ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA.

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Colonel Mustafa amerejea rasmi kwenye tasnia ya muziki baada ya ukimya wa miaka mitano. Rapa huyo mwenye Asili ya Tanzania na Kenya amefichua kuwa yupo mbioni kuachia album yake mpya na tayari ameshaachia wimbo wake wa kwanza kutoka kwenye album hiyo iitwayo  Maloko ambao ameufanya na Prodyuza   Motif Di Don. Akizungumza na NIAJE NIAJE rapa huyo amefunguka sababu za kuandika nyimbo zake mwenyewe kwa kusema kwamba huwa anajisikia mwenye faraja anapojiandikia nyimbo kwa sababu huwa anajieleza vizuri kupitia ubunifu wake binafsi. “When someone else writes a songs for me, they don’t do as well as they do when I write them myself and they don’t get to express my thoughts fully. They will only write what is fit for them,” he says. Hitmaker huyo wa Hey Baby amedokeza mpango wa kufanya remix ya wimbo wake Lenga Stress na wasanii wapya kwenye game kwani anaamini kizazi cha sasa kina uwezo mkubwa wa kumtoa sehemu na kupeleka kwingine kwenye muziki wake. Utakumbuka Colonel Mustafa alitamba sana kipindi cha nyuma na nyimbo zake kali kama Monalisa, Adhiambo C, Mtaani dot com, Kinyau nyau na nyingine kibao.

Read More