Daddy Awashauri Wanaume Kutoziweka Hisia Zote kwa Wanawake
Mwanamuziki wa Injili, Daddy Owen, ameibua mjadala mtandaoni baada ya kutoa ushauri mkali kwa wanaume kuhusu namna wanavyopaswa kujihusisha kimapenzi na wanawake. Kupitia mitandao ya kijamii, Daddy Owen amewataka wanaume kutoziweka hisia zao zote kwa wanawake, akisema kufanya hivyo kunawafanya kuwa rahisi kudhibitiwa kihisia. Kwa mujibu wa ujumbe wake, wanaume wanaoweka mapenzi na hisia zao bila mipaka hujikuta wakitumia nguvu nyingi kupenda kuliko wanavyopendwa, hali ambayo huweza kuwafanya kuumizwa kwa urahisi. Msanii huyo, ameonya kuwa baadhi ya wanawake hutumia mapungufu hayo kama njia ya kuwapata na kuwadhibiti wanaume katika mahusiano. Kauli hiyo imezua mijadala mikubwa mtandaoni, baadhi ya watu wakikubaliana naye wakisema wanaume wengi huwa wanapoteza uthabiti wao pale wanapopenda kupita kiasi, huku wengine wakimkosoa kwa madai kuwa maoni yake yanachochea mgawanyiko katika mahusiano.
Read More