RUFFTONE AZUA GUMZO MTANDAONI, AIBUA TUHUMA NZITO DHIDI YA DADDY OWEN

RUFFTONE AZUA GUMZO MTANDAONI, AIBUA TUHUMA NZITO DHIDI YA DADDY OWEN

Mgombea wa wadhfa wa useneta kaunti ya Nairobi msanii Rufftone amezua gumzo mtandaoni mara baada kuibuia madai mazito dhidi ya kaka yake Daddy Owen. Akiwa kwenye moja ya interview Rufftone amesema miaka kadhaa iliyopita Daddy Owen ambaye kwa wakati huo alikuwa mfuasi sugu wa Chama ODM alimkimbiza kwa panga nusra amkatekate na tangia kipindi hicho hajawahi kipenda chama hicho kwani anakihusisha na uhuni. Hitmaker huyo wa “Mungu Baba” alishindwa kueleza kwa kina mfumo wa uchumi wa bottom up ambao unaendesha na chama cha UDA  ambacho kinaongozwa na Naibu wa rais Dkt William Ruto. Hata hivyo ametoa wito kwa wakenya kuwachagua viongozi vijana ambao watabadilisha taifa  hili kwa kuleta maendeleo mashinani.

Read More
 DADDY OWEN AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA BRENDA WAIRIMU

DADDY OWEN AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA BRENDA WAIRIMU

Staa wa muziki nchini Daddy Owen amevunja kimya chake juu ya tuhuma za kumtaka kimapenzi mwiigizaji Brenda Wairimu kupitia mitandao yake ya kijamiii. Kupitia ukurasa wake wa instagram Daddy Owen ameonyesha kufurahishwa na namna watu walifsiri ujumbe wake kwenda kwa brenda wairimu huku akisema kwamba hana uhusiano wowote wa kimapenzi na mrembo huyo. Hitmaker “Vanity” ameenda mbali zaidi na kuahidi kumpeleka Brenda Wairimu kwenye mtoko mbele ya wanablogu ili kuzima tetesi za kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwiigizaji huyo, jambo ambalo lilimfanya mrembo huyo kushuka kwenye uwanja wa comment ya post ya Daddy Owen na kukubali ombi lake. Kauli ya Daddy Owen imekuja mara baada ya kuachia ujumbe kwenye picha ya Brenda Wairimu, ujumbe ambao uliibua maswali mengi miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao walihoji kwamba huenda wawili hao wanatoka kimapenzi.

Read More
 DADDY OWEN AWABARIKI MASHABIKI ZAKE NA CHAPTER 4 ALBUM

DADDY OWEN AWABARIKI MASHABIKI ZAKE NA CHAPTER 4 ALBUM

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Daddy Owen ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. Album hiyo inayokwenda kwa jina la Chapter 4 ina jumla ya singo 15 ya moto huku ikiwa na 6 collabo pekee. Daddy Owen amewashirikisha wasanii kama Nakaaya,Bella Kombo, Judy Stevens,Ivyln Mutua,Danco na Slejj. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chapter 4 album  Daddy Owen amesema safari ya kuandaa album yake mpya haikuwa rahisi ila anamshukuru mwenyezi mungu kwa kumwezesha kuikamilisha album hiyo licha ya changamoto alizokutana nazo. Chapter 4 ni album ya sita kwa mtu mzima Daddy Owen lakini pia inavunja ukimya wake wa miaka 5 tangu alipoachia album yake ya Vanity iliyotoka mwaka wa 2016.

Read More