Davido Atoa Sababu za Kutoshiriki Tamasha la London

Davido Atoa Sababu za Kutoshiriki Tamasha la London

Msanii maarufu wa muziki wa Afrobeats kutoka Nigeria, Davido, ametangaza kujiondoa rasmi katika tamasha kubwa la muziki lililopangwa kufanyika katika uwanja wa Tottenham Hotspur jijini London, ambalo lilitarajiwa kufanyika Julai 2025. Tamasha hilo lilikuwa linamjumuisha pamoja na wakali wa muziki kutoka Marekani, 50 Cent na Mary J. Blige. Kupitia taarifa aliyoitoa kwenye mitandao ya kijamii, Davido alieleza kuwa licha ya tamasha hilo kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa mashabiki pamoja na mafanikio katika mauzo ya tiketi, kulikuwepo na matatizo ya msingi katika maandalizi na uendeshaji wa tukio hilo Katika maelezo yake, Davido alionyesha kutoridhishwa na mchakato mzima wa maandalizi na kuonyesha kuwa uamuzi huu umetolewa baada ya mazungumzo yaliyoshindikana kati ya pande mbili, jambo lililomfanya asisitize kutoshiriki kwenye tamasha hilo. Uamuzi huo umewashtua mashabiki wengi waliokuwa na matarajio makubwa ya kumuona msanii huyo akitumbuiza sambamba na majina makubwa ya muziki wa kimataifa. Hadi sasa, waandaaji wa tamasha hilo hawajatoa tamko lolote rasmi kuhusu kujiondoa kwa Davido au hatua watakazochukua baada ya mabadiliko hayo.

Read More
 Davido Afichua: “Kama Sisingekuwa Msanii, Ningekuwa Mwandishi wa Habari”

Davido Afichua: “Kama Sisingekuwa Msanii, Ningekuwa Mwandishi wa Habari”

Msanii nyota wa Afrobeats kutoka Nigeria, Davido, amewashangaza mashabiki wake kwa kufichua kwamba angekuwa mwandishi wa habari kama hangejikita kwenye muziki. Kauli hiyo ya kushangaza ilitolewa wakati wa mahojiano ya moja kwa moja kwenye Beat 96.1FM, ambako msanii huyo alizungumza kwa undani kuhusu maisha yake nje ya jukwaa. Katika mahojiano hayo, Davido alieleza jinsi ambavyo kampeni ya kutangaza albamu yake mpya imekuwa ya kuchosha, lakini kwa upande mwingine, anafurahia sana mazungumzo na mikutano na wanahabari, tofauti na wasanii wengi wa kiwango chake.  “Nimekuwa nikifanya promo kali kwa ajili ya albamu yangu – si kazi rahisi. Sina haja ya kufanya promo lakini napenda. Napenda kuongea. Watu wengi hawajui kwamba mbali na kusomea usimamizi wa biashara, pia nimesomea masoko. Kwa hiyo napenda mazungumzo. Kama ningekuwa na podcast, ningeweza kuzungumza siku tatu au nne mfululizo.” Tofauti na wasanii wengi wanaoepuka kamera na mahojiano, Davido anaamini kuwa mazungumzo ni sehemu ya sanaa, na kwamba huwa anajihusisha sana na taarifa mbalimbali za kijamii na kisiasa. “Ni sehemu ya kuwa msanii, kwa mtazamo wangu. Si kila mtu hupenda kuzungumza, lakini mimi napenda. Nikikutana na mtu, napenda kuongea. Napenda habari. Ukiingia nyumbani kwangu, kila mara mimi huhakikisha kuna taarifa – huwezi kukosa CNN kwenye runinga ya sebuleni.” Akiendelea kufunguka, Davido alieleza kuwa mara nyingi akiwa nyumbani hujikuta akifanya utafiti kuhusu mambo mbalimbali, ishara kuwa ana kiu ya maarifa na kujua yanayoendelea duniani. Kwa msingi wa mapenzi yake makubwa kwa mawasiliano, Davido alisema kwamba kama hangekuwa msanii, basi angekuwa mtangazaji au mwanahabari. “Mimi ni mtu ninayependa taarifa. Naona kama nisingekuwa kikamilifu kwenye muziki, basi ningekuwa kwenye kitu kama uandishi wa habari. Napenda kuwaeleza watu kile ninachofanya.” Aidha, alizungumzia kuhusu umaarufu wake mitandaoni, akisema kuwa sababu mojawapo ni kujishughulisha, kushiriki, na kuwasiliana moja kwa moja na mashabiki wake. “Watu huuliza kwa nini nina followers wengi – ni kwa sababu najihusisha na watu, na ninafanya kazi kila wakati.” Kwa kauli zake, Davido anaonesha kuwa yeye si msanii wa kawaida tu, bali ni msomi wa mawasiliano, mpenzi wa taarifa, na mtu anayeamini kuwa muziki na mawasiliano vinaenda pamoja. Hali hii huenda ikamfungulia milango ya vipindi vya podcast au mahojiano ya runinga siku za usoni.

Read More
 Davido ashinda tuzo 5 AFRIMA

Davido ashinda tuzo 5 AFRIMA

Mwaka 2023 umeanza vyema kwa Davido baada kushinda tuzo 5 za AFRIMA (All Africa Music Awards) 2023 zilizotolewa usiku wa kuamkia leo huko Dakar, Senegal. Davido amebeba tuzo ya (Best Male Arist African Inspirational Music) kupitia wimbo wake StandStrong. Tuzo ya PILI ni (Best Duo/Group in African Electro) kupitia wimbo wake ChampionSound aliomshirikisha Focalistic na Tuzo yake ya TATU ni (Best Act in the Diaspora Male) kupitia wimbo Who’sTrue alioshirikishwa na Tion Wayne. Nyota huyo ambaye alifunga mwaka 2022 kwa kutoa performance kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar, tuzo yake ya NNE aliyoshinda ni (Best African Collaboration) kupitia wimbo wake ChampionSound aliomshirikisha Focalistic na ya TANO ni (Best Duo/ Group in African Pop) kupitia wimbo High alioshirikishwa na msanii Adekunle Gold. Wakali wengine waliobeba tuzo kwenye usiku huo ni pamoja na Wizkid, Asake, Adekunle Gold.

Read More
 Davido na Chioma wafunga ndoa

Davido na Chioma wafunga ndoa

Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido ameripotiwa kufunga ndoa na mpenzi wake Chioma ambaye ni mzazi mwenza wa mtoto wao aliyefariki dunia “Ifeanyi”. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari toka Nigeria. Ndoa hiyo inayotajwa kuwa ya kitamaduni ilifungwa nyumbani kwa baba yake Davido na ilihudhuriwa na watu wa familia za wawili hao pekee. Katika hafla hiyo, inaelezwa hakuna aliyekubaliwa kupiga picha wala kuchukua video. Pia inaelezwa, mahari ya Chioma ililipwa yote ingawaje alikuwa amekataa kuolewa na Davido kufuatia kifo cha mwanae ambaye alimtizamia kama ndiye aliyewaleta pamoja. Ndoa hiyo ilikuwa sharti ifungwe ili Ifeanyi ambaye alifariki kwenye swimming pool nyumbani kwao, aweze kuzikwa kama mmoja wa familia ya Davido, kulingana na tamaduni za jamii ya Igbo. Aidha, kabla ya kifo cha Ifeanyi, Davido na Chioma walikuwa tayari wametangaza rasmi kwamba watafunga ndoa mwakani 2023.

Read More
 Davido ahairisha tamasha lake la muziki nchini Marekani

Davido ahairisha tamasha lake la muziki nchini Marekani

Mwanamuziki wa Nigeria Davido hatafanya tena tamasha lake “AWAY” la nchini Marekani ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu, hii ni kufuatia kifo cha mwanaye ambaye alifariki dunia wiki iliyopita. Menejimenti ya Davido imetoa taarifa rasmi kwamba Tamasha la msanii huyo ambalo lilikuwa lifanyike Novemba 18 mwaka huu katika uwanja wa State Farm Arena Jijini Atlanta Georgia, limeahirishwa hadi Novemba 18, mwaka 2023 Menejimenti yake imesema ni muhimu kwa Davido kutumia muda huu na familia yake pamoja na wapendwa wake. Kwa wote waliokuwa tayari wamenunua tiketi, basi zitatumika mwakani siku ya onesho hilo. Bado Davido na Chioma hawajazungumza chochote tangu tukio la kumpoteza mtoto wao

Read More
 Davido mbioni kufunga ndoa mwaka 2023

Davido mbioni kufunga ndoa mwaka 2023

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Davido ameahidi kuwa mwaka 2023 atafunga ndoa na mpenzi wake Chioma. Davido amebainisha hayo akiwa na baby mama wake huyo pamoja na mchungaji wake Tobi Adegboyega huko Uingereza, alipoenda kumtambulisha Chioma kwa mchungaji huyo. “Our wife, our real wife,” anasikika Mchungaji Tobi akieleza, na Davido akaongezea, “Hundred per cent, going down 2023.” Mbali na hilo kupitia instastory ya Staa davido ameshare picha na video zikionesha mpenzi wake Chioma akipewa zawadi ya Mkoba na Mchungaji tobiadegboyega_Ambapo mkoba huo unatajwa kuwa na Thamani ya $90,000 zaidi ya million 9 za Kenya. Ikumbukwe, Davido na Chioma walianza mahusiano yao tangu mwaka 2017, na 2019 Davido alimvisha pete ya uchumba Chioma. Hata hivyo wakaja kuachana mwaka 2020, wakabaki kuwa walezi wa mtoto wao. Julai mwaka huu wakawa wanahusishwa kurudiana, kisha baadae wakathibitisha na sasa wamepanga kufunga pingu za maisha ifikapo mwakani.

Read More
 Meek Mill aomba kolabo tena na Davido baada ya kumtoza shillingi millioni 20

Meek Mill aomba kolabo tena na Davido baada ya kumtoza shillingi millioni 20

Rapper kutoka Marekani Meek Mill ameamua kuweka wazi kuhusu kumtaka mwanamuziki davido kufanya naye kazi kwa mara nyingine tena ,baada ya kudai amekua akipata simu nyingi sana za show kutoka Afrika na davido ndi mtu anaeweza kukamilisha na kusimamia mchongo huo licha ya kutokua sawa kipindi hicho. Wawili hao tayari wamewahi kufanya kazi mwaka 2015 na kuachia wimbo uitwao “Fan’s Me” kollabo ambayo Davido aliweka wazi kumgharimu zaidi ya shillingi million 20 huku rapper huyo akishindwa kuisapoti baada ya ngoma hiyo kutoka rasmi. Hivi karibuni kumekua na trend ya wanamuziki nyota kutoka Marekani kutaka kufanya kazi na wanamuziki wa Afrika ,jambo linaloashiria mziki wa afrika unaendelea kuteka soko la dunia.

Read More
 DAVIDO NA DJ MAPHORISA WARUSHIANA MANENO MAKALI MTANDAONI KISA AMAPIANO

DAVIDO NA DJ MAPHORISA WARUSHIANA MANENO MAKALI MTANDAONI KISA AMAPIANO

Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido amemjibu DJ Maphorisa kufuatia mjadala uliozuka kwenye mtandao wa twitter juu ya msanii aliyeutangaza zaidi muziki wa Amapiano kimataifa. Kupitia moja ya watumiaji wa twitter alishare ujumbe kuwa msanii Davido ndio msanii aliyeutangaza muziki wa Amapiano Afrika na kimataifa na kudai kuwa kwa sasa msanii Wizkid ndio anajaribu kufanya kama alivyofanya Davido huku akidai kuwa msanii huyo amekuwa akianza kufanya vitu na wasanii wengine wanaiga kwake. Baada ya ujumbe huo mkali kutoka nchini Afrika Kusini DJ Maphorisa aliijibu tweet hiyo na kusema kuwa yeye na Kabelo Motha walianza kuwashirikisha wasanii Wizkid na Burna Boy kwenye wimbo wa Amapiano wa Sponono miaka mitatu nyuma, hivyo sio Davido aliyeutangaza muziki huo. Kauli hiyo imemuibua Davido ambaye ameshindwa kukaa kimya kuhusu mjadala huo na kuandika kuwa DJ Maphorisa hajawahi kumpenda licha ya kuwa mtu mwema kwake, hivyo ameamua kujiweka mbali naye.

Read More
 DAVIDO AMTAMBULISHA MTOTO ALIYEZAA NA MREMBO WA ENGLAND LARISSA LONDON

DAVIDO AMTAMBULISHA MTOTO ALIYEZAA NA MREMBO WA ENGLAND LARISSA LONDON

Kwa mara ya kwanza mwimbaji Davido ameonekana hadharani na mtoto wake wa miaka miwili, Dawson ambaye alizaa na Makeup artist Larissa London mwenye makazi yake nchini Uingereza. Davido ambaye yupo nchini Uingereza alipata nafasi ya kuhudhuria ibada Jana Jumapili (August 7) akiwa mtoto wake huyo wa Kiume. Kulikuwepo taarifa kuwa ni mwanaye lakini tofauti na watoto wengine, Davido hakuwahi kuonekana na Dawson hadharani. Mkali huyo wa Nigeria ana watoto wanne Imade, Hailey, Ifeanyi na Dawson toka kwa Wanawake wanne tofauti.

Read More
 DIAMOND PLATINUMZ MBIONI KUAACHIA KOLABO NA DAVIDO

DIAMOND PLATINUMZ MBIONI KUAACHIA KOLABO NA DAVIDO

Kolabo mpya ya nyota wa muziki barani Afrika yaani Davido na diamondplatnumz inanukia, hii ni baada ya mtayarishaji lizer classic wa lebo ya WCB ambaye ni mtayarishaji wa kazi nyingi za Diamond kuonyesha sehemu ya project hiyo. Lizer anathibisha kwamba kazi mpya kutoka kwa wawili hao ipo na itakuja. Ame-share kupitia insta story yake akionekana akiiandaa kazi hiyo. Diamond na davido ambao hawana dogo kwenye kazi zao, ni wakali wa hitsong “My Number One Remix” iliyotoka zaidi ya miaka 8 iliyopita ikiwa ndio kolabo yao ya kwanza.

Read More
 DAVIDO NA KIZZ DANIEL MBIONI KUACHIA EP YA PAMOJA

DAVIDO NA KIZZ DANIEL MBIONI KUACHIA EP YA PAMOJA

Mastaa kutoka Nigeria Davido na Kizz Daniel wamewadokezea mashabiki wa muziki wao juu ya ujio wa EP ya pamoja. Kupitia twitter wamethibitisha taarifa hiyo huku Davido akitamba kwamba EP hiyo itauza nakala milioni kwenye wiki ya kwanza. “Nani yuko tayari kwa ajili ya Ep ya 0.B.O X KIZZ?? Tutauza zaidi ya Milioni 1 katika wiki ya kwanza tu” ametweet Davido. Hata hivyo wawili hao hawajaweka wazi tarehe rasmi ya kuachia EP hiyo wala jina lake. Mara ya mwisho Wakali hao kukutana ilikuwa kwenye singo iitwayo “One Ticket” kutoka kwenye Album ya Kizz Daniel “No Bad Songz” ya mwaka 2018.

Read More
 DAVIDO AFIKISHA SUBSCRIBERS MILLIONI 3 YOUTUBE

DAVIDO AFIKISHA SUBSCRIBERS MILLIONI 3 YOUTUBE

Staa kutoka Nigeria Davido amefanikiwa kufikisha jumla ya wafuatiliaji (Subscribers) Milioni 3 katika channel yake ya youtube. Davido anakuwa msanii wa pili kwa nchini Nigeria kuwa na subscribers wengi katika mtandao wa youtube. Nafasi ya kwanza inashikwa na mwimbaji nyota CKay mwenye subscribers Milioni 3.16 akiwaacha mbali Burna Boy mwenye subscribers million 2.54 huku Wizkid akiwa na Subscribers million 2.41.

Read More