DESIRE LUZINDA ATANGAZA KUREJEA KWENYE MUZIKI

DESIRE LUZINDA ATANGAZA KUREJEA KWENYE MUZIKI

Msanii kutoka uganda Desire Luzinda, ametangaza kurejea muziki baada ya kukaa kimya kwa takriban miaka minne. Kupitia mitandao yake ya kijamii Desire Luzinda amethibitisha kuachia wimbo mpya wa Injili kutoka kwenye EP yake mpya “ALABASTER HEART” ambayo amekuwa akiifanyia kazi. “Mabibi na mabwana, kila kitu kina msimu na wakati wake. Baada ya miaka minne ya ukimya, ninafurahi kutangaza kwamba nitatoa wimbo wangu wa kwanza kutoka kwenye EP yangu ya ALABASTER HEART EP Hivi karibuni. Nimefurahia sana kile ambacho Bwana anakaribia kufanya,” aliandika. Luzinda hajakuwa akiachia nyimbo tangu alipoacha muziki wa kidunia mwaka wa 2019 na kugeukia muziki wa injili. Kwa sasa anaishi nchini Marekani lakini amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na watayarishaji na wasanii wa Uganda hasa Levixone ambaye alimsaidia kwenye project yake mpya.

Read More
 SAKATA LA NDOA YA MSANII LEVIXONE NA DESIRE LUZINDA LACHUKUA SURA MPYA

SAKATA LA NDOA YA MSANII LEVIXONE NA DESIRE LUZINDA LACHUKUA SURA MPYA

Msanii aliyegeuki muziki wa Injili nchini Uganda Desire Luzinda inadaiwa kuwa hajafunga ndoa na mwimbaji mwenzake Levixone kwa nia njema kwani anamtumia kwa ajili ya kupata msaada wa kifedha kutoka kwa wafadhili. Chanzo cha karibu na mrembo huyo kinasema kipindi Desire anaanzisha wakfu wake Desire Luzinda Foundation alijaribu kuomba msaada kwa kanisa ambalo anashiriki nchini Marekani lakini alikataliwa kwa sababu hakuwa ameolewa. Uongozi wa kanisa hilo ulimshauri kuingia kwenye ndoa kwanza kama mkristo kamali ili aweze kupewa msaada wa kufadhili wakfu wake. Sasa rafiki yake wa zamani mwimbaji Levixone ndiye alikuwa kimbilio kwake na inatajwa hiyo ndio sababu ya mrembo huyo kuficha mahusiano yake ya kimapenzi. Hata hivyo wawili hao hawajatoa tamko lolote dhidi ya tuhuma hizo ila ni jambo la kusubiriwa. Utakumbuka video ya Levixone akiwa anatambulishwa kwa wazazi wa Desire Luzinda ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kitendo ambacho kiliwaacha walimwengu na maswali  juu ya wawili hao kuhalalisha mahusiano yao. Hii ilikuja mara baada ya uvumi wa wawili hao kutoka kimapenzi kuzungumziwa sana mtandaoni kwa kipindi cha miezi miwili.

Read More