Bahati Atangaza Ndoa na Diana Marua Mwaka 2026

Bahati Atangaza Ndoa na Diana Marua Mwaka 2026

Msanii nyota wa muziki nchini Kenya, Bahati, amewapa mashabiki wake habari ya kusisimua baada ya kuashiria kuwa hatimaye anapanga kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Diana Marua, mwaka ujao. Kupitia ujumbe wa hisia aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Bahati alifichua kuwa mwaka 2026 utakua wa kipekee kwao, kwani wataadhimisha miaka 10 ya kuwa pamoja. Katika chapisho lake, Bahati alimweleza Diana kuwa amekuwa mvumilivu kwa miaka yote, akiahidi kuwa wakati wao wa kusherehekea upendo wao kwa njia ya ndoa umefika. Akitumia hashtagi ya #SikuKuuYaBahati, Bahati alionekana kuelekeza maandalizi ya tukio kubwa ambalo linaweza kuwa harusi yao rasmi. “Mpenzi wangu mrembo @Diana_Marua, najua tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu ndoa yetu. Mwaka ujao tutatimiza miaka 10 pamoja. Najua inaonekana kama ni muda mrefu lakini usiali, #SikuKuuYaBahati itakuwa ya kipekee.” Bahati pia alielezea jinsi harusi ya msanii wa Bongo Fleva kutoka Tanzania, Juma Jux, ilivyomgusa na kumtia moyo kama mwanaume. Akitumia alama ya reli #JP2025, alikiri kuwa harusi hiyo ilimfundisha thamani ya kumpenda na kumheshimu mwanamke.  “#JP2025 imenifundisha jinsi mwanaume anavyopaswa kumthamini na kumuenzi yule anayempenda. Kaka yetu wa Afrika Mashariki, Jux, ametuheshimisha. Hongera sana kaka yangu @Juma_Jux na mrembo @its.priscy. Nathibitisha wazi kuwa mimi ndiye ninayefuata #BD2025.” Baada ya chapisho hilo, mashabiki walimiminika kwenye sehemu ya maoni wakionyesha furaha, wakitoa pongezi na pia kuomba kuhudhuria harusi hiyo. Wengi walieleza kuwa wamekuwa wakisubiri muda mrefu kuona Bahati akimvalisha Diana pete ya ndoa madhabahuni. Ikiwa mipango hiyo itatimia, basi mwaka 2025 huenda ukawa mwaka wa kihistoria kwa Bahati na Diana, na huenda pia tukashuhudia harusi mojawapo ya kifahari zaidi katika burudani ya Afrika Mashariki.

Read More
 Diana Marua afunguka baada ya kupata ukosoaji mkubwa alipovalia mavazi ya Balenciaga

Diana Marua afunguka baada ya kupata ukosoaji mkubwa alipovalia mavazi ya Balenciaga

Msanii Diana Marua amefunguka kwa mara ya kwanza baaada ya watu kumkosoa mtandaoni kwa kuvalia vazi la Balenciaga licha ya kampuni hiyo kupata ukosoaji mkubwa kutokana na kufanya matangazo ambayo yanakiuka maadili ya watoto. Akizungumza na mume wake Bahati, Diana amesema kuwa hakuwa na ufahamu kuwa chapa ya Balenciaga ilikuwa na utata na ndio maana alivalia vazi lao akiwa tu kwenye shughuli zake za kawaida. Aidha bahati amemtaka awe makini anapochagua mavazi ya kuvaa kwani huenda ikamleta shida mitandaoni ikizingatiwa kuwa kuna baadhi ya makampuni ambayo hufanya matangazo ambayo yanakwenda kinyume na maadili ya jamii. Utakumbuka kampuni ya Balenciaga iliomba msamaha juu ya matangazo yenye baada ya kufanya photoshoot ya bidhaa zao mpya ambayo inadaiwa kuendekeza maudhui ya ponografia kwa watoto.

Read More
 Bahati adai wakosoaji wake mtandaoni wanampa nguvu ya kutia bidii kimuziki

Bahati adai wakosoaji wake mtandaoni wanampa nguvu ya kutia bidii kimuziki

Mwanamuziki kutoka Kenya Bahati amedai kwamba hana muda wa kuwajibu wanaomkosoa mtandaoni. Hitmaker huyo wa Adhiambo amewaambia watesi wake kuwa chuki anayoipata kwenye mitandao ya kijamii inampa changamoto ya kutia bidii kwenye kazi zake za muziki. “Guys thank you so much for your support. Like we wouldn’t be here without you without your love, without your criticism, negativity, we take them in”, Aliandika Instagram. Bahati alisema hayo alipokuwa akizindua tuzo ya Golden Plaque aliyotunukiwa na mtandao wa YouTube kwa ajili ya kupata wafutialiaji (Subscribers) milioni moja. Bahati na mke wake Diana B wamekuwa wakikosolewa mitandaoni mwaka mzima kwa matukio ambayo wamekuwa wakijihusisha nayo na hawajaathirika kwa namna yeyote kwenye shughuli zao.

Read More
 Diana B anyosha maelezo kuhusu video iliyosambaa mtandaoni akikiri kutoka kimapenzi na wanaume wengi

Diana B anyosha maelezo kuhusu video iliyosambaa mtandaoni akikiri kutoka kimapenzi na wanaume wengi

Msaniii na  mwanamitandao maarufu kutoka Kenya Diana Marua amefunguka juu ya video iliyosambaa mtandaoni akikiri kuwa alitembea na wanaume wengi kimapenzi kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake ya msingi. Kupitia ujumbe mrefu aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Diana amesema aliweka wazi suala hilo kwa umma kwa lengo la kuwapa moyo vijana wanaopitia masha magumu. Lakini pia amewahimiza watoto wa kike kutokata tamaa kwenye ndoto zao na badala yake watie bidii kwani muda wao wa kupata mafanikio utafiki. Diana Marua ameongeza kuwa kama balozi mwema katika jamii anapaswa kuzungumzia magumu aliyoyapitia kwenye maisha yake badala ya kuangazia mazuri tu. Diana alichapisha video hiyo kwenye mitandao yake ya kijamii  mwaka 2020 wakati alipokuwa akipokea gari jipya aina Mercedes Benz alilozawadi na mume wake Bahati. Alikumbuka kipindi alikuwa anaishi maisha ya uchochole ambapo alilazimika kutoka kimapenzi na wanaume tofauti kwa ajili ya kupata pesa lakini pia kuendesha magari ambayo hakuwa anaweza kumudu wakati huo. Kwa sasa Diana ana hesabu baraka zake kama Mama ya watoto watano, Mke na mtengeneza maudhui kwenye mitandao ya kijamii.

Read More
 BAHATI NA DIANA MARUA WATANGAZWA MABALOZI WA OPPO KENYA

BAHATI NA DIANA MARUA WATANGAZWA MABALOZI WA OPPO KENYA

Kampuni ya OPPO inayojishughulisha na  uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki imemtangaza rasmi  Bahati na mke wake Diana Marua kuwa mabalozi wake. Katika taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye mtandao wa instagram katika page ya Oppo Kenya imeeleza kuwa wamefurahi kumkaribisha Bahati pamoja na Diana Marua kuwa balozi wa Oppo. “We partnered with @wabosha_maxine @bahatikenya @diana_marua to officially introduce you all to our newest model, the OPPO Reno 7!”,  Imesema sehemu ya chapicho hilo. Kwa upande mwingine Bahati amethibitisha pia katika chapisho lake kwenye mtandao wa Instagram kwa kusema kwamba amejisikia faraja kuwa balozi  wa OPPO na kuahidi kuitendea kazi katika kutangaza kampuni hiyo kupitia bidhaa zao za simu. “ANNOUNCEMENT‼️ JUST SIGNED AS THE NEW OPPO Reno 7 BRAND AMBASSADORS 🔥 So excited to partner with @oppo_kenya @wabosha.maxine and Wifey @Diana_Marua as we officially introduce to you the new OPPO Reno 7!”,  imesema taarifa hiyo. Wakati huo huo Oppo imeitambulisha simu yake mpya ya Oppo Reno ambayo imeingia hivi karibuni sokoni, simu hiyo yenye 8GB RAM + 250 GB ROM inatarajiwa kuuzwa kwa bei nafuu zaidi ili kumsaidia kila Mkenya kumiliki smartphone.

Read More
 WILLY PAUL AOMBA RADHI FAMILIA YA BAHATI KUFUATIA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DIANA MARUA

WILLY PAUL AOMBA RADHI FAMILIA YA BAHATI KUFUATIA TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DIANA MARUA

Staa wa muziki nchini Willy Paul hatimaye ameiomba radhi familia ya Bahati baada ya kupewa makataa ya saa 24 kufanya hivyo la sivyo atafunguliwa mashtaka kwa madai ya kutoa matamshi ya chuki dhidi ya Diana Marua. Willy Paul awali alidai kuwa miaka kadhaa iliyopita alitoka  kimapenzi na mke wa Bahati japo hakubaka kama namna ambavyo Diana Marua alimtuhumu. Sasa kupitia screenshot ya ujumbe unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii willy paul ameonekana akimlilia Bahati amsamehe kutokana na kile kinachoendelea mtandao. Sanjari na hilo Willy Paul amemtumia Bahati Barua akisema kwamba madai yake ya kutoka kimapenzi na mke wake Diana Marua sio ya kweli kwani kiki tu,  hivyo Bahati anapaswa kuelewa kwani ni sehemu ya matukio ambayo utokea kwenye tasnia ya muziki. Hata hivyo haIjabainika kama kuna ukweli wowote kuhusiana na hilo ikizingatiwa kuwa Willy Paul wala Bahati hajatoa tamko lolote. Utakumbuka Januari 13 mwaka huu kuna barua ilikuwa inasambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa ni ya wakili wa Diana Marua ambapo kwenye barua Willy Paul alipewa makataa ya saa 24 aombe msamaha la sivyo afungulie kesi mahakamani kwa madai ya kumharibia jina diana marua kuwa aliwahi toka nae kimapenzi.

Read More
 DIANA MARUA AFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL YOUTUBE

DIANA MARUA AFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL YOUTUBE

Mwanamitandao aliyegeukia muziki  Diana Marua amefuta video aliyotengeneza akidai kuwa staa wa muziki nchini Willy Paul alijaribu kumbaka. Hii ni baada ya  mahakama ya Milimani kutoa amri  ikimtaka Diana Marua kufuta video ambayo alipakia YouTube mnamo Desemba 9  yenye jina la ‘My Untold Story, Willy Paul tried to rape me’ ikielezwa kuwa madai yake yameathiri kazi na afya ya Willy Paul . “Inaamriwa kuwa video ya mshtakiwa/mlalamikiwa na chapisho la mitandao ya kijamii lililochapishwa kwenye chaneli yake ya YouTube yenye jina la ‘My Untold Story, Willy Paul tried to rape me’, lfutwe ikusubiriwa kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake kwa vile linamuathiri mlalamishi, kumfanya apoteze fursa za biashara na kumfanya ateseke kiafya” Karatasi ya amri za mahakama iliyotiwa saini na hakimu mkuu mwandamizi D.W Mburu ilisomeka. Mahakama pia ilimtahadharisha Diana na washirika wake dhidi ya kumharibia jina Willy Paul ikisubiriwa kusikilizwa kwa kesi aliyowasilisha mahakamani. Onyo kali imetolewa kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ya mahakama ambayo ilitolewa tarehe 29 Desemba.

Read More
 MAHAKAMA YAMUAMURU DIANA MARUA KUFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL

MAHAKAMA YAMUAMURU DIANA MARUA KUFUTA VIDEO YA TUHUMA ZA UBAKAJI DHIDI YA WILLY PAUL

Mahakama ya Milimani nchini Kenya imemuamuru Diana Marua kufuta video aliyotengeneza akidai kuwa mwanamuziki Willy Paul alijaribu kumbaka. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Willy Paul alichapisha picha ya karatasi ya amri za mahakama iliyotiwa saini na hakimu mkuu mwandamizi D.W Mburu. Amri hiyo ya mahakama inamtaka Diana Marua kufuta video ambayo alipakia YouTube mnamo Desemba 9 ikielezwa kuwa madai yake yameathiri kazi na afya ya Willy Paul. “Inaamriwa kuwa video ya mshtakiwa/mlalamikiwa na chapisho la mitandao ya kijamii lililochapishwa kwenye chaneli yake ya YouTube yenye jina la ‘My Untold Story, Willy Paul tried to rape me’, lfutwe ikusubiriwa kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake kwa vile linamuathiri mlalamishi, kumfanya apoteze fursa za biashara na kumfanya ateseke kiafya” Karatasi hiyo ilisomeka. Mahakama pia imemtahadharisha Diana na washirika wake dhidi ya kumharibia jina Willy Paul ikisubiriwa kusikilizwa kwa kesi aliyowasilisha mahakamani. Onyo kali imetolewa kwa yeyote atakayekaidi amri hiyo ya mahakama ambayo ilitolewa tarehe 29 Desemba.

Read More
 WEEZDOM AMJIBU DIANA MARUA BAADA YA KUDAI UBALOZI WAKE NA LIMAVEST NI BANDIA

WEEZDOM AMJIBU DIANA MARUA BAADA YA KUDAI UBALOZI WAKE NA LIMAVEST NI BANDIA

Msanii wa muziki nchini Weezdom amemtolea uvivu mke wa Bahati, Diana Marua baada ya mrembo huyo kupuzilia mbali ubalozi wake na kampuni ya Limavest. Akipiga stori na mwana youtube presenter Ali, Weezdom amesema kwamba ameshangazwa na kauli ya chuki ambayo diana aliitoa dhidi ya dili alilopewa na kampuni ya Limavest akisisitiza kwamba mrembo huyo ana wivu na mafanikio yake kwani kipindi cha nyuma alinyang’anywa ubalozi wa kampuni hiyo baada ya kukiuka mkataba wa maelewano. Lakini pia ameeleza kwamba Diana ameiponda dili lake la ubalozi kutokana na hatua yake ya kumkingia kifua Willy Paul kwa tuhuma za uongo alizoziibua dhidi ya msanii huyo. Hata hivyo amesema ubalozi wake na kampuni ya Limavest ni halali na sio feki kama jinsi ambavyo Diana Marua amewaaminisha watu kwenye mitandao ya kijamii. Kauli ya Weezdom imekuja mara baada ya Diana Marua kudai kuwa taarifa za Weezdom kulamba dili la ubalozi  wa kampuni ya Limavest ni za uongo kwani msanii huyo anatumia jina la kampuni hiyo kutengeneza kiki ili azungumziwe.

Read More