Mwanamitandao anayesuasua kimuziki nchini Kenya, Diana Marua, amejipata katika matatizo ya kisheria baada ya kutumia biti ya wimbo wa marehemu E-Sir bila idhini katika wimbo wake “Bibi ya Tajiri.”
Prodyuza nguli wa Ogopa DJs, Lucas Bikedo, amethibitisha kuwa anapanga kumfungulia kesi Marua kwa ukiukaji wa hakimiliki (copyright infringement). Bikedo anadai kuwa Marua alitumia instrumental ya wimbo wa E-Sir bila kupata ruhusa rasmi kutoka kwake kama mmiliki halali wa kazi hiyo ya muziki.
Kwa mujibu wa ripoti, ikiwa atapatikana na hatia, Diana Marua anaweza kulazimika kulipa faini kubwa au kufidia hasara kwa kutumia kazi ya mtu mwingine bila idhini.
Diana Marua, ambaye amekuwa akijaribu kujijengea jina kama mwanamuziki, bado hajatoa tamko rasmi kuhusu tuhuma hizo.