Rapa Diddy Kusomewa Hukumu Oktoba 3 kwa Kesi ya Ukahaba

Rapa Diddy Kusomewa Hukumu Oktoba 3 kwa Kesi ya Ukahaba

Rapa na mfanyabiashara maarufu wa Marekani, Sean Combs almaarufu Diddy, amepangiwa rasmi tarehe ya kusomewa hukumu yake kuhusiana na makosa ya biashara ya ukahaba. Jaji Arun Subramanian ametangaza kuwa hukumu hiyo itasomwa Oktoba 3 mwaka huu, ikiwa ni siku ile ile aliyopendekeza wiki iliyopita mara baada ya Diddy kupatikana na hatia kwa makosa mawili makuu yanayohusiana na kusafirisha watu kwa lengo la kujihusisha na ngono. Kulingana na vyanzo vya mahakama, Diddy atasalia kizuizini hadi siku hiyo ya hukumu, hali inayomaanisha kuwa atakuwa amekaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kufikia wakati huo. Muda aliokaa rumande unatarajiwa kuzingatiwa katika uamuzi wa mwisho wa kifungo chake. Hii inakuwa hatua nyingine kubwa katika sakata linalomkumba Diddy, ambaye kwa miaka mingi amekuwa mmoja wa majina makubwa katika tasnia ya burudani Marekani. Wadau mbalimbali wa muziki na mashabiki wake wameendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hii inayotikisa vichwa vya habari kimataifa.

Read More
 Mahakama Yatoa Uamuzi Mpya Kesi ya Diddy, Shtaka Kubwa Linasubiriwa

Mahakama Yatoa Uamuzi Mpya Kesi ya Diddy, Shtaka Kubwa Linasubiriwa

Mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu wa Marekani, Sean “Diddy” Combs, amepatikana na hatia ya kosa la ukahaba haramu lakini amesafishwa mashtaka mazito zaidi ya biashara haramu ya ngono (sex-trafficking) na uhalifu wa kupanga (racketeering), ambayo yangemuweka gerezani maisha. Kufuatia hukumu hiyo, mchakato wa kutoa adhabu rasmi umekamilika na sasa unatarajiwa kutangazwa rasmi hivi karibuni. Diddy anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 20 jela kwa kosa hilo la ukahaba haramu. Wanasheria wake wameshikilia kuwa anapaswa kuachiliwa kwa dhamana akisubiri kusikilizwa kwa hukumu yake rasmi, wakisisitiza kuwa hana historia ya kukimbia kesi. Hata hivyo, upande wa mashtaka unapinga vikali ombi hilo, ukionya kuwa Diddy ana ushawishi mkubwa wa kifedha na kijamii unaoweza kutumiwa kuingilia mchakato wa haki. Kesi hii imeibua mjadala mkubwa duniani kuhusu matumizi mabaya ya mamlaka, ushawishi wa mastaa katika vyombo vya sheria, na mapambano dhidi ya unyanyasaji wa kingono.

Read More
 Kesi ya Diddy Yaingia Hatua ya Mwisho Bila Shahidi wa Utetezi

Kesi ya Diddy Yaingia Hatua ya Mwisho Bila Shahidi wa Utetezi

Kesi ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono inayomkabili msanii maarufu wa muziki wa hip-hop, Diddy, inaonekana kufikia hatua ya mwisho huku upande wa utetezi ukibakia bila shahidi hata mmoja kuwasilisha ushahidi. Kwa mujibu wa ripoti ya CNN, upande wa mashtaka umepanga kumaliza uwasilishaji wa ushahidi wake mara baada ya shahidi wa mwisho wa mashtaka, wakala maalum Joseph Cerciello kutoka Idara ya Upelelezi wa Usalama wa Ndani (Homeland Security Investigations), kukamilisha ushahidi wake. Hii itahitimisha rasmi awamu ya uwasilishaji ushahidi kwa upande wa mashtaka. Timu ya mawakili wa utetezi imemjulisha mahakama kuwa hawatatoa mashahidi wala ushahidi wowote wa upande wa utetezi, na hata Diddy mwenyewe hatashuhudia. Kwa mujibu wa CNN, utetezi unatarajia kutoa ushahidi mdogo kabla ya kuanza kwa hoja za mwisho za kesi. Hatua hii inamaanisha kesi hiyo itakuwa imeingia katika hatua ya hoja za mwisho ambazo zitahitimisha mchakato wa maamuzi ya mahakama kuhusu kesi hiyo inayosababisha hisia na ushauri mkubwa katika tasnia ya muziki na jamii kwa ujumla.

Read More
 50 Cent Apinga Uwezekano wa Trump Kumsamehe Diddy

50 Cent Apinga Uwezekano wa Trump Kumsamehe Diddy

Rapa maarufu 50 Cent amejitokeza waziwazi kupinga kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu uwezekano wa kumsamehe Sean “Diddy” Combs, ambaye anakabiliwa na mashtaka mazito ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono na uhalifu wa kupanga. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, 50 Cent alionyesha kutoridhishwa na kauli ya Trump, akieleza kuwa Diddy amekuwa akiongea vibaya kuhusu Trump kwa muda mrefu, na hivyo si sahihi kwa kiongozi huyo wa zamani kufikiria kumsamehe mtu ambaye hakumuunga mkono.  “Alisema mambo mabaya sana kuhusu Trump, sio sawa. Nitawasiliana naye ili ajue jinsi ninavyohisi kuhusu mtu huyu.”  aliandika Instagram Kauli hii ya 50 Cent inakuja baada ya Trump kusema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba hajapokea ombi rasmi la msamaha kwa Diddy, lakini yuko tayari kuangalia ukweli wa kesi hiyo kabla ya kufanya uamuzi wowote. Diddy anakabiliwa na mashtaka mazito ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, njama ya uhalifu, na usafirishaji kwa ajili ya ukahaba.  Iwapo atapatikana na hatia, anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Uhusiano kati ya 50 Cent na Diddy umekuwa na mvutano kwa muda mrefu, na 50 Cent amekuwa akitoa maoni ya ukosoaji dhidi ya Diddy mara kwa mara.  Kauli yake ya sasa inaonyesha nia ya kuzuia msamaha wowote kutoka kwa Trump kwa Diddy.

Read More
 Ray J Amshambulia Suge Knight kwa Madai ya Uhusiano wa Kimapenzi na Diddy

Ray J Amshambulia Suge Knight kwa Madai ya Uhusiano wa Kimapenzi na Diddy

Msanii wa R&B na mfanyabiashara Ray J ameibuka kwa hasira na kumshambulia vikali Suge Knight baada ya madai ya kushangaza aliyoyatoa kwenye kipindi cha televisheni cha Piers Morgan, ambapo Suge alisema kuwa Ray J na Diddy walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. Madai haya yamezua hisia kali kwa Ray J na mashabiki wake. Ray J, ambaye awali alikuwa akimheshimu Rais huyo wa zamani wa Death Row Records, na kumtetea, alisema amevunjika moyo na kauli hizo zisizo na msingi. Alidai kuwa Suge amemshambulia kwa njia chafu na kuonyesha tabia ya kutojali, licha ya kuwa amekuwa akimuunga mkono katika nyakati ngumu. Aidha, Ray J alilalamikia namna Suge alivyoikosea heshima brand yake ya The Gaygency, inayosaidia wasanii wa jamii ya LGBTQIA+. Alisisitiza kuwa kuunga mkono jamii hiyo hakumaanishi kuwa yeye binafsi ni mpenzi wa jinsia moja, na ni aibu kwa Suge kutumia hilo kumshambulia. Ray J pia alimtuhumu Suge kuwa mtu anayeudhulumu watu wa karibu, ikiwemo wanaume na wanawake. Hadi sasa, Suge hajajibu madai hayo, huku mjadala ukiendelea kuenea mitandaoni kwa hisia kali kutoka kwa wafuasi wa pande zote.

Read More
 Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Rapa maarufu mwenye utata, Kanye West, ametoa hisia zake kuhusu hali inayoendelea kumkumba Sean Diddy Combs, akieleza masikitiko yake juu ya hatua ya Kid Cudi kutoa ushahidi dhidi ya Diddy. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Ye ameonekana kuzungumzia kile anachokiona kama mfumo wa haki unaowakandamiza watu weusi, akisisitiza haja ya jamii ya wasanii na Wamarekani Weusi kwa ujumla kujilinda na kushikamana badala ya kushirikiana na mifumo anayoamini kuwa ya kibaguzi. “I wish Cudi hadn’t testified against Puff. We need to not be locked in white systems. Praying for Puff and his family. Praying for Puff Daddy and the Family.”Aliandika X Kauli hiyo imeibua hisia mseto kutoka kwa mashabiki na wanamuziki wenzake, huku baadhi wakimtetea kwa msimamo wake wa kutaka mshikamano miongoni mwa wasanii wa asili ya Kiafrika, na wengine wakimkosoa kwa kudharau mchakato wa haki. Kid Cudi, ambaye zamani alikuwa rafiki wa karibu wa Ye, anatajwa kuwa miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi dhidi ya Diddy kufuatia madai mazito yanayomkabili kuhusu vitendo vya unyanyasaji na ukiukaji wa haki.

Read More
 Young Thug Amshambulia Kid Cudi kwa Madai ya Kutoa Ushahidi Dhidi ya Diddy

Young Thug Amshambulia Kid Cudi kwa Madai ya Kutoa Ushahidi Dhidi ya Diddy

Mastaa wawili wa muziki wa hip hop, Young Thug na Kid Cudi, wameingia kwenye mzozo wa wazi baada ya Cudi kuonekana mahakamani kutoa ushahidi unaomkabili rapa nguli Sean “Diddy” Combs, katika kesi inayohusisha tuhuma za unyanyasaji, ukatili na matumizi mabaya ya madaraka. Kupitia chapisho aliloliweka kwenye akaunti yake ya X (zamani Twitter), Young Thug aliandika neno “rat” huku akimtag Kid Cudi, kauli ambayo katika muktadha wa mitaani na muziki wa hip hop humaanisha msaliti au mtu anayewasaliti wenzake kwa kushirikiana na vyombo vya sheria. Ingawa Thug alifuta chapisho hilo muda mfupi baadaye, tayari liliwasha moto mitandaoni, huku mashabiki wakitofautiana kuhusu uhalali wa hatua hiyo. Kid Cudi alionekana kizimbani mwishoni wiki jana kutoa ushahidi katika kesi inayomkabili Diddy, msanii na mfanyabiashara mwenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya muziki wa Marekani. Taarifa zinasema ushahidi wa Cudi unahusiana na matukio ya zamani ambayo huenda yakawa na uzito mkubwa katika uamuzi wa mwisho wa kesi hiyo. Young Thug, ambaye kwa sasa naye anakabiliwa na kesi kubwa ya RICO (Racketeer Influenced and Corrupt Organizations Act) inayohusisha mashitaka ya uhalifu wa genge, ameonekana kuchukulia hatua ya Cudi kama ukiukaji wa kanuni za mtaa, zinazokataza kushirikiana na mamlaka au kutoa ushahidi dhidi ya wenzako. Wachambuzi wa masuala ya burudani wanasema huenda Thug anaangalia hali hiyo kwa jicho la mtu anayepitia mchakato wa kisheria na kuona kwamba hatua kama ya Cudi zinaweza kudhuru watu walioko kwenye mazingira kama yake. Kauli ya Thug imezua mijadala mikubwa, huku upande mmoja wa mashabiki ukimtetea Kid Cudi kwa kusema kwamba hatua yake ni ya kijasiri na inalenga kusaidia kutendeka kwa haki. Wengine wanasema Cudi amevunja misingi ya mshikamano katika jamii ya hip hop kwa “kuwageuka” wenzake. Mpaka sasa, Kid Cudi hajajibu moja kwa moja tuhuma au kejeli hizo kutoka kwa Young Thug. Vyanzo vya karibu na msanii huyo vinaeleza kuwa ameweka mkazo kwenye ukweli na kutafuta haki kwa waathirika.

Read More
 Meek Mill Azua Gumzo Mitandaoni Baada ya Tweets Zenye Msimamo Mkali

Meek Mill Azua Gumzo Mitandaoni Baada ya Tweets Zenye Msimamo Mkali

Msanii maarufu wa hip hop Meek Mill amezua gumzo mtandaoni baada ya kuchapisha mfululizo wa tweets zenye ujumbe mzito kuhusu shutuma mbalimbali, maisha ya anasa, na heshima ya jina lake. Katika ujumbe wake, Meek Mill amekanusha vikali madai kwamba aliwahi kushambuliwa au kuibiwa, akieleza kuwa alipokuwa Los Angeles alikutana na watu mashuhuri kama Suge Knight na Big U bila hofu yoyote. Anasema lengo lake lilikuwa kuonyesha vijana kuwa kuna maisha zaidi ya vurugu, hasa kwa jamii ya Weusi.  “Luce Cannon na kile kikao chake na Akademiks kilikuwa mtego mtupu… halafu huyu mtu hana jina, anasema eti alinivamia na kunipora.” Akaongeza: “Nilikuwa nakutana na Suge Knight na Big U nilipokuwa LA… bila kamera wala mbwembwe!” Akisisitiza kuwa madai ya kushambuliwa ni ya uongo. Meek pia ameeleza kutoridhishwa na mazingira ya sherehe za mastaa, akidai kuwa matumizi ya dawa za kulevya, hasa “coke”, ni jambo la kawaida. Hata hivyo, anasisitiza kuwa yeye hajawahi kulewa hata bangi na anaepuka utegemezi wa vitu hivyo licha ya kuwa na utajiri mkubwa tangu akiwa na miaka 23. “Kitu cha kushangaza zaidi nilichowahi kuona kwenye sherehe ya Puff ni ‘vibes za coke’… na hii hutokea kwenye hizi sherehe zote.” Akasisitiza msimamo wake kwa kusema: “Nimekuwa na mamilioni tangu nikiwa na miaka 23, sitaki hata kuwa mraibu wa bangi… Sihukumu, lakini naona mambo kwa jicho tofauti!” Aidha, amekosoa baadhi ya blogu kwa kumhusisha na kesi ya Lil Rod dhidi ya Diddy, akisema kuwa jina lake halikutajwa lakini mitandao imejaribu kumchafua. Anasisitiza kuwa jamii yake haikuamini tuhuma hizo, lakini bado ni shambulio dhidi ya chapa yake. “Wakati Diddy anakabiliwa na kesi ya FEDERAL, nataka kuibua tena suala la Lil Rod na kesi yake ambayo ilitupiliwa mbali. Hakuwahi kutaja jina langu, lakini blogu ziliendeleza ajenda nzima dhidi yangu.” Akaongeza: “Jamii yangu haikuamini lakini hii ni hujuma dhidi ya chapa yangu… nataka kujua ukweli wa yote haya!” Kauli hizi kutoka kwa Meek Mill zimezua hisia mseto miongoni mwa mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii. Baadhi wamempongeza kwa uwazi wake na msimamo thabiti, huku wengine wakimtaka awe makini na kauli zake, hasa wakati huu ambapo kesi ya Diddy bado iko kwenye mchakato wa kisheria.

Read More
 Watu Wanalipwa $50 kwa Saa Kuvaa T-Shirt za “Free Diddy”, Mwanamke Afichua Siri

Watu Wanalipwa $50 kwa Saa Kuvaa T-Shirt za “Free Diddy”, Mwanamke Afichua Siri

Taarifa mpya zimeibuka kuhusu watu waliokuwa wamevaa T-Shirt zenye maandishi “Free Diddy” nje ya mahakama, zikionesha kwamba si wote waliokuja kwa hiari yao. Mwanamke mmoja amefichua kuwa baadhi ya watu waliokuwa wamevalia T-Shirt hizo walikuwa wamelipwa hadi $50 kwa saa ili kushiriki katika kile kinachoonekana kuwa ni kampeni ya kumuunga mkono msanii maarufu, Diddy. Kwa mujibu wa vyanzo vya burudani nchini Marekani, mwanamke huyo alisema kuwa alikaribishwa kushiriki katika shughuli hiyo lakini alikataa kuvaa T-Shirt hizo licha ya kuahidiwa malipo ya $20 kwa saa mwanzoni, ambayo baadaye yaliripotiwa kuongezeka hadi $50 kwa saa kwa baadhi ya watu. “Nilijua siwezi kuvaa hiyo T-shirt. Siwezi kusimama nikimuunga mkono mtu ambaye sijui ukweli wake,” alisema mwanamke huyo. Kampeni ya Free Diddy imezua mjadala mkubwa mtandaoni, huku baadhi ya watu wakihisi kuwa inalenga kuonesha picha ya uungwaji mkono wa umma kwa Diddy wakati mashtaka dhidi yake bado yanaendelea kushughulikiwa mahakamani. Mpaka sasa, haijafahamika wazi ni nani aliyefadhili kampeni hiyo ya mavazi, lakini madai ya watu kulipwa kushiriki yamezua maswali kuhusu uhalisia na dhamira ya maandamano hayo ya kuunga mkono msanii huyo.

Read More
 Diddy Ataka Kesi ya Dawn Richard Itupiliwe Mbali, Asema Madai Ni ya Uongo

Diddy Ataka Kesi ya Dawn Richard Itupiliwe Mbali, Asema Madai Ni ya Uongo

Rapa na mfanyabiashara tajiri Sean “Diddy” Combs amepeleka ombi mahakamani kutaka kesi ya madai ya kiraia iliyofunguliwa dhidi yake na mwanamuziki Dawn Richard itupiliwe mbali, akisema madai hayo ni ya uongo na ya kupotosha. Ombi hilo linakuja siku hiyohiyo ambayo Dawn alifika mahakamani kutoa ushahidi dhidi ya Diddy katika kesi tofauti ya jinai. Katika kesi hiyo, Diddy anakabiliwa na tuhuma mbalimbali zinazohusiana na unyanyasaji wa kingono, matumizi mabaya ya mamlaka na vurugu ambapo Dawn ni mmoja wa mashahidi muhimu. Dawn Richard, aliyewahi kuwa mwanachama wa kundi la Danity Kane lililoanzishwa na Diddy kupitia kipindi cha Making the Band, alifungua kesi ya madai mapema mwaka huu, akimtuhumu Diddy kwa unyanyasaji wa kimwili na kihisia wakati alipokuwa chini ya usimamizi wake kisanii. Diddy, kupitia mawakili wake, amesisitiza kuwa madai hayo hayana msingi wowote na ni jaribio la makusudi la kumharibia jina, hasa wakati huu ambapo anakabiliwa na uchunguzi mkubwa wa umma na wa kisheria. Kwa mujibu wa taarifa za mahakama, ombi la Diddy la kutupilia mbali kesi hiyo litashughulikiwa katika kikao kijacho, huku kesi ya jinai ikiendelea kusikilizwa kwa kasi. Wachambuzi wa masuala ya sheria wanasema jinsi kesi hizi mbili zinavyohusiana huenda kukawa na athari kubwa kwa uamuzi wa mwisho, hasa endapo ushahidi wa Dawn utaonekana kuwa na uzito katika pande zote mbili. Kwa sasa, Diddy anapinga vikali madai yote dhidi yake na ameapa kujitetea hadi mwisho ili kulinda jina lake na kazi yake ya muda mrefu katika tasnia ya burudani.

Read More
 “Siku Moja Tutazungumza Kuhusu ‘Diddy’ wa Kenya” – Rapper Wangechi Afichua Mada Nzito Kuhusu Tasnia ya Muziki

“Siku Moja Tutazungumza Kuhusu ‘Diddy’ wa Kenya” – Rapper Wangechi Afichua Mada Nzito Kuhusu Tasnia ya Muziki

Msanii wa muziki wa rap nchini Kenya, Wangechi, ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuandika ujumbe wa kutatanisha unaoashiria kuwepo kwa unyonyaji na hujuma dhidi ya wasanii wa kike katika tasnia ya muziki humu nchini. Kupitia akaunti yake ya mtandao wa X, Wangechi alidokeza kuwa kuna mtu mashuhuri kwenye sekta ya muziki humu nchini anayefanana na mtayarishaji wa muziki wa Marekani, Diddy ambaye kwa miaka amezuia wasanii wa kike kutoka na kazi zao kutoka studio. “One day we shall speak about the Diddy of Kenya and how no female artist ever left that studio with their music.” (“Siku moja tutazungumza kuhusu Diddy wa Kenya na jinsi hakuna msanii wa kike aliyewahi kutoka katika studio hiyo na muziki wake.”) – aliandika Wangechi. Ingawa hakumtaja mtu yeyote kwa jina, kauli hiyo imeibua mijadala mikubwa kuhusu usalama, haki na usawa katika sekta ya muziki hasa kwa wasanii wa kike ambao kwa muda mrefu wamelalamikia ukosefu wa usaidizi wa haki na kuwepo kwa mazingira yenye unyanyasaji wa kiakili, kijinsia na kitaaluma. Mashabiki na wadau wa muziki wameanza kujiuliza ni nani “Diddy wa Kenya” anayetajwa, huku wengi wakihusisha ujumbe huo na visa vya awali vilivyoripotiwa na baadhi ya wanamuziki wachanga. Hadi kufikia wakati wa kuchapishwa kwa habari hii, Wangechi bado hajatoa maelezo zaidi, lakini ujumbe wake umeacha gumzo zito ambalo huenda likabadilisha mwelekeo wa mazungumzo kuhusu usalama, uhuru na haki za wasanii wa kike nchini Kenya.

Read More
 Mashabiki Wastushwa na Ushahidi Mpya wa Cassie Dhidi ya Diddy

Mashabiki Wastushwa na Ushahidi Mpya wa Cassie Dhidi ya Diddy

Katika kile kinachoendelea kuwa moja ya kesi kubwa zaidi kwenye burudani, siku ya nne ya kesi ya Sean “Diddy” Combs imeendelea kuvuta hisia za wengi, baada ya ushahidi wa kushangaza kutoka kwa Cassie, aliyekuwa mpenzi wa muda mrefu wa rapa huyo. Cassie, ambaye amefungua kesi dhidi ya Diddy akimtuhumu kwa unyanyasaji wa kingono, kihisia na kimwili, alieleza mahakamani kuwa aliendelea kushiriki katika kile alichokiita “freak-offs” yaani matukio ya kingono yaliyohusisha watu wengine hata alipokuwa katika mahusiano ya kimapenzi na msanii mwingine, Kid Cudi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka mahakamani, Cassie alidai kuwa aliendelea kushiriki matukio hayo kwa shinikizo la kisaikolojia kutoka kwa Diddy, akieleza kuwa ilikuwa ngumu kujinasua kutokana na udhibiti mkubwa aliokuwa nao Diddy juu ya maisha yake.  “Nilihisi nipo kwenye mtego. Hata nilipojaribu kuwa na mtu mwingine kama Kid Cudi, bado nilijikuta narudi kwenye mzunguko wa Diddy,” alisema Cassie kwa sauti ya huzuni. Ushuhuda huo uliibua minong’ono mahakamani na kufufua mjadala mpana mtandaoni kuhusu nguvu na ushawishi wa watu mashuhuri katika mahusiano yasiyo na usawa. Jina la Kid Cudi, ambalo halikutarajiwa kuhusishwa moja kwa moja na kesi hii, limeanza kutajwa katika vyombo vya habari, huku baadhi ya mashabiki wakijiuliza iwapo alijua kile kilichokuwa kikiendelea kati ya Cassie na Diddy wakati wa uhusiano wao. Mpaka sasa, Kid Cudi hajajibu wala kutoa tamko lolote kuhusu ushahidi huo, licha ya jina lake kutajwa wazi mahakamani. Mashabiki wake na wa Cassie wanasubiri kuona kama atachagua kuzungumza au kuendelea na kimya chake.

Read More