Mwigizaji Terrence Howard afunguka kuwahi kuingiliwa kimwili na Diddy

Mwigizaji Terrence Howard afunguka kuwahi kuingiliwa kimwili na Diddy

Mwigizaji maarufu nchini Marekani Terrence Howard amefanya mahojiano na Podcast ya PBD na kumwaga sumu kali kuhusu rapa Diddy. Kwa mujibu wa Terrence Howard, anasema Diddy alitaka kumuingilia kimwili. Hii ni baada ya mwigizaji huyo kualikwa nyumbani kwa rapa huyo kwa lengo kumfundisha uigizaji kama ambavyo ombi lake lilikuwa linasema. Baada ya kufika, Terrence anasema alianza kuzungunza na Diddy lakini macho yake yalikuwa yakimtazama sana kiasi cha kugundua kwamba hakuna usalama mahali pale. Baadaye msaidizi wa Terrence ikabidi amchane boss wake kwamba, Diddy anataka kutoka na wewe wiki ijayo, na anataka kukuingilia kimwili. Aidha muigizaji huyo mkongwe amesema, vijana wengi wamekuwa wakiangukia kwenye mtego huo kwa sababu ya kutaka kufanikiwa kwenye vitu wanavyopenda.

Read More
 Diddy akingia kifua Yung Miami baada ya kuitwa mchepuko wake

Diddy akingia kifua Yung Miami baada ya kuitwa mchepuko wake

Baada ya Rapa Diddy kutangaza kuwa amepata mtoto wa kike, DJ Akademiks ameanzisha mjadala kupitia mtandao wa Twitter kuhusu uhusiano uliopo kati ya rapa huyo na mpenzi wake Yung Miami akidai kuwa Miami ni mpango wa kando wa Diddy baada ya kugundua sio mama wa mtoto huyo. Suala hilo halikumpendeza hata kidogo Diddy ambaye pia ametumia ukurasa wake wa Twitter kujibu kinacho endelea kwa kusema kuwa Yung Miami sio mchepuko wake,hajawahi na hatokua kwa kuwa ni mtu muhimu na wa kipekee kwake. “@yungmiami305 is not my side chick. Never has been, never will be. She’s very important and special to me, and I don’t play about my Shawty Wop. I don’t discuss things on the internet and I will not start today”, Aliandika. Mpaka sasa Mama wa mtoto wa Diddy hajawekwa wazi ni lini walibarikiwa kumpata mtoto lakini fununu za ndani zinadai kuwa mtoto huyo ambaye ni wa saba kwa Diddy alizaliwa mwezi Oktoba mwaka huu katika hospitali ya Newport Beach, California.

Read More
 DIDDY KUPOKEZWA TUZO YA MAFANIKIO YA MAISHA BET 2022

DIDDY KUPOKEZWA TUZO YA MAFANIKIO YA MAISHA BET 2022

Msanii wa Hip Hop Marekani, Sean Combs maarufu kama Diddy anatarajiwa kupokea Tuzo ya Heshima na Mafanikio ya Maisha kutoka BET zinazotarajiwa kutolewa Juni 26, 2022 katika ukumbi wa Microsoft Theater Jijini Los Angeles, Marekani. Tuzo hizi zinaandaliwa na Black Entertainment Television (BET) toka Juni 19, 2001 zinalenga kusheherekea mafanikio ya kazi za Wamarekani Weusi katika sanaa ya muziki, uigizaji na michezo. “Ni heshima kuwa sana kwa tasnia ambapo sio tu ametengeneza utamaduni kupitia kazi zake, lakini pia amekuwa kiongozi katika mabadiliko ambayo mara kwa mara yanahusisha vizazi kwa vizazi na kuchangia kuongeza ubora kwennye tasnia yetu hivyo anastahiki hili,” wamesema BET Ikumbukwe wasanii wa kwanza kukabidhiwa tuzo ya BET ni kundi la Outkast liloundwa mwaka 1992 na wasanii wawili (Andre ‘3000’ Benjamin na Antwan ‘Big Boi’ Patton) ambapo mwaka 2001 walishinda katika kipengele cha Best Group.

Read More
 DIDDY AMPA JAY Z MAUA YAKE AKIWA HAI,AMFANANISHA NA TUPAC PAMOJA NA BIGGIE

DIDDY AMPA JAY Z MAUA YAKE AKIWA HAI,AMFANANISHA NA TUPAC PAMOJA NA BIGGIE

Rapa kutoka Marekani P.Diddy ameamua kumpa Jay-Z maua yake akiwa angali hai. Bosi huyo wa lebo ya muziki ya “Love Records” amempongeza kwa kusema kwamba amefanikwa kuvaa viatu vya manguli wawili wa Hip Hop duniani, marehemu Tupac Shakur na Notorious B.I.G. Diddy amesema hayo kupitia Twitter Spaces iliyowakutanisha pamoja na Fat Joe kwenye Kumbukumbu ya miaka 50 ya Kuzaliwa kwa marehemu Notorious B.I.G. Utakumbuka Mei 21 mashabiki wa muziki wa HipHop duniani walisherekea kwa masikitiko kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Marehemu Notorious B.I.G. ambaye alizaliwa Mei 21 mwaka 1972. Notorious B.I.G. aliuawa Machi 9 mwaka 1997 akiwa kwenye gari lake na watu wengine wakati wakitoka kwenye sherehe ya tuzo za Soul Train huko Los Angles nchini Marekani.  

Read More
 DIDDY AFUNGUKA KUMKINGIA KIFUA TRAVIS SCOTT KWENYE TUZO ZA BILLBOARD

DIDDY AFUNGUKA KUMKINGIA KIFUA TRAVIS SCOTT KWENYE TUZO ZA BILLBOARD

Mkongwe wa muziki wa Hiphop kutoka Marekani P. Diddy anaendelea kuthibitisha kwa nini anajiita “LOVE”, amefunguka wazi kwamba ni yeye ndiye alimpambania Travis Scott kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye Tuzo za Billboard (BBMA’s) ambazo zitafanyika Mei 16 mwaka huu. “For the Billboard Music Awards this Sunday I made a request, I made a demand. I said ‘My brother Travis Scott has to perform. I’m executive producing, he has to perform,’ and NBC said ‘yes.’ It’s going down Sunday, Travis Scott will be performing… now that’s love.” amekaririwa Diddy ambaye ni Mtayarishaji Mkuu wa Tuzo hizo. Hii itakuwa show ya pili kwa mtu mzima Travis Scott kutumbuiza tangu onesho la Astroworld ambalo lilipelekea vifo vya watu 10 na wengine 4,900 kujeruhiwa.

Read More
 DIDDY AZINDUA RASMI LEBO YAKE YA MUZIKI

DIDDY AZINDUA RASMI LEBO YAKE YA MUZIKI

Rapa kutoka Marekani P. Diddy amezindua na kuitambulisha Lebo yake mpya ya muziki iitwayo “Love Records” ambayo maalum itasimamia na kufanya kazi na wasanii wa muziki wa R&B pekee. Lebo hiyo itafanya kazi chini ya ushirikiano na kampuni ya Motown Records. Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Diddy amesema ana furaha kuitambulisha lebo hiyo ambayo itafanya kazi na wasanii wapya wa muziki wa R&B pamoja na watayarishaji wenye uwezo mkubwa. Kwa upande wake ameichukulia kama ukurasa mpya wa maisha yake ya muziki kwani pia ameahidi kurudi kwenye muziki na ataachia Album chini ya lebo yake hiyo. Mwaka wa 1993 Diddy alianzisha lebo yake iitwayo “Bad Boy Records” na ilipata mafanikio makubwa ikifanya kazi na wakali wa dunia kama marehemu Notorious B.I.G, Faith Evans, 112, Mase, Cassie na wengine kibao.

Read More
 JAY Z, KANYE WEST & DIDDY WATAJWA KAMA MARAPA WALIOINGIZA MKWANJA MREFU MWAKA 2021

JAY Z, KANYE WEST & DIDDY WATAJWA KAMA MARAPA WALIOINGIZA MKWANJA MREFU MWAKA 2021

Orodha ya wasanii wa Hip Hop waliotengeneza pesa nyingi zaidi mwaka wa 2021 imetoka na jina la Jay-Z lipo namba 1. Jay Z ametajwa kuingiza kiasi cha shilling billion 51.2 za Kenya  ambazo zimetokana na pato la baada ya kuuza hisa zake nyingi za mtandao wa TIDAL kwa kampuni ya Square Ink, kwa takriban shilling billion kiasi cha shilling billion 34.4 za Kenya. Lakini pia Jay Z alikunja mkwanja mrefu mwaka jana baada ya kampuni ya LVMH kununua nusu ya hisa za Kinywaji chake, cha Armand de Brinac. Kwa upande wa Kanye west ambaye amekamata nafasi ya pili kwa shilling billion 28.5 za Kenya, pato lake kubwa limeendelea kuingia kupitia bidhaa za Yeezy. Wasanii wengine waliongiza pesa nyingi mwaka wa 2022 ni pamoja na Diddy ambaye alikamata nafasi ya tatu kwa shilling billion 8.5 akifuatwa na drake aliyeingiza kiasi cha shilling billion 5.7 huku tano bora ikifungwa na mtu mzima wiz khalifa ambaye aliingiza kiasi cha shilllingi billion 5.1 za Kenya. HIP-HOP’S TOP EARNERS 2021 JAY-Z – $470 million Kanye West – $250 million Diddy – $75 million Drake – $50 million Wiz Khalifa – $45 million Travis Scott – $38 million DJ Khaled – $35 million Eminem – $28 million J. Cole – $27 million Birdman – $25 million Doja Cat – $25 million Tech N9ne – $25 million

Read More