Ndugu wa Gloria Ntazola Apata Ajira Mpya Baada ya Kukataliwa na Familia
Ndugu ya socialite Gloria Ntazola, ambaye hivi karibuni aliomba msamaha hadharani na kuomba asaidiwe kuanzisha biashara, sasa amepata ajira mpya licha ya kukataliwa na familia yake. Mdau wa Burudani Obidan Dela amethibitisha taarifa hizo, akisema kijana huyo ameajiriwa kwenye moja ya maduka ya kuuza mavazi jijini Nairobi. Kwa mujibu wa Dela, uamuzi huo umekuja kama juhudi za kumsaidia kijana huyo kuanza upya maisha bila kutegemea familia. Hatua hii inakuja siku moja baada ya Gloria Ntazola kuapa waziwazi kwamba hataweza tena kumsaidia ndugu yake huyo, akidai aliumizwa sana kihisia kutokana na matendo yake ya awali. Gloria alisema kwamba licha ya kumsaidia mara kadhaa, tabia za kijana huyo na kukosekana kwa mabadiliko vilimfanya kuamua kutompa nafasi nyingine.
Read More