Socialite anayesuasua mtandaoni, Gloria Ntazola ameibua mjadala mkali mtandaoni baada ya kuwakosoa wanaume wa Kenya hasa Nairobi kwa kile alichokitaja kama tabia ya kujibana wanapopeleka warembo kwenye miadi ya kimapenzi (Dates).
Katika ujumbe wake uliosambaa mitandaoni, Gloria ameeleza kuwa wanaume wengi jijini Nairobi hawapendi kutumia pesa zao kununua chakula kizuri kwa wapenzi wao, badala yake hukimbilia vyakula vya bei rahisi kama chips na mayai.
Mrembo huyo amesisitiza kuwa wanaume wanapaswa kuwa wakarimu zaidi na kujifunza kuwathamini wanawake wanaowaalika kwenye miadi mbalimbali.
Hata hivyo ametoa changamoto kwa wanaume kukoma kuwaalika wanawake kwenye shughuli hizo kama hawana pesa za kutosha za kukimu mahitaji yao ya msingi.
Gloria Ntazola amejizolea umaarufu kutokana na matamshi yake yenye utata kuhusu masuala ya mahusiano na mitindo ya maisha, na mara kadhaa amekuwa akizua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii.