GRAVITY OMUTUJJU AKIRI KUKATAA TAMAA KWENYE MAANDALIZI YA TAMASHA LAKE

GRAVITY OMUTUJJU AKIRI KUKATAA TAMAA KWENYE MAANDALIZI YA TAMASHA LAKE

Rapa Gravity Omutujju amefunguka na kudai kwamba nusura ajiondoe kwenye tamasha lake lijalo kutokana na changamoto za promota wake anayejulikana kama Norbert. Katika mahojiano yake hivi karibuni Omutujju amesema Promota huyo amekuwa akihujumu tamasha lake kwa kuamini maneno ya watu kuwa amekuwa akitoa tiketi za bure kwa mashabiki, jambo lililomfanya Nobert kutofanya maandalizi mazuri ya onesho hilo. Hitmaker huyo wa “Tusimbudde” amesema alilazimika kumrejesha promota huyo baadhi ya pesa za maandalizi ya tamasha lake ambapo amedai kwamba kwa sasa anafanya kazi na promota Balaam Barugahare ambaye aliingilia kati kumsaidia kwani angehairisha onesho lake ingeathiri chapa yake ya muziki, Tamasha la Gravity linatarajiwa kufanyika Oktoba mosi mwaka wa 2022 huko Cricket Oval, Lugogo.

Read More
 GRAVITY OMUTUJJU AMTOLEA UVIVU WINNIE NWAGI

GRAVITY OMUTUJJU AMTOLEA UVIVU WINNIE NWAGI

Rapa Gravity Omutujju amesema msanii wa Swangz Avenue Winnie Nwagi anahitaji kusaidia kimawazo kabla ya utundu wake kumuaharibu chapa yake za muziki. Katika mahojiano yake Omutujju amesema mrembo huyo anahitaji kufunzwa namna atakavyobadili miendo yake ya maisha kama kweli anataka kudumu kwa muda mrefu kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda. Kauli yake inakuja kipindi hiki Winnie Nwagi anasuasua kwenye suala la kuwatafuta wafadhili wa onesho lake la muziki ambalo litafanyika mapema mwezi Septemba mwaka huu. Inadaiwa kuwa baadhi ya makampuni hayataki kujihusisha na mrembo huyo kutokana na tabia yake mbaya. Winnie nwagi ni moja kati ya wasanii watundu nchini Uganda ikizingatiwa kuwa amekuwa akihusishwa na kashfa mbali mbali za ukosefu wa nidhamu ikiwemo kuwatusi na kuwapiga mashabiki zake.

Read More
 GRAVITY OMUTUJJU ATANGAZA KUMFADHILI KING SAHA KUSAMBARATISHA UCHAGUZI WA UMA

GRAVITY OMUTUJJU ATANGAZA KUMFADHILI KING SAHA KUSAMBARATISHA UCHAGUZI WA UMA

Rapa Gravity Omutujju amejiungana na orodha ya wasanii wanaopinga upigaji kura katika chama cha wanamuziki UMA kura kufanyika kwa njia ya mtandao. Katika mahojiano yake hivi karibuni Omutujju ametaka wapiga kura kushiriki kwenye uchaguzi wa chama hicho kwa mfumo wa kawaida wa kupanga foleni kwenye vituo vya kupigia kura. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Tusimbudde” ameahidi kumfadhili king saha kifedha ili aweze kusambaratisha juhudi za uongozi wa UMA kufanya uchaguzi kwa njia ya mtandao. Hata hivyo amesema ana imani kuwa King Saha atamshinda Cindy kwenye uchaguzi ujao wa chama cha UMA kwa kuwa ana wafuasi wengi ambao wanamuunga mkono.

Read More
 GRAVITY OMUTUJJU APINGA HATUA YA SPICE DIANA NA SHEEBAH KUMALIZA UGOMVI WAO

GRAVITY OMUTUJJU APINGA HATUA YA SPICE DIANA NA SHEEBAH KUMALIZA UGOMVI WAO

Rapa kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju amepuzilia mbali suala la msanii Spice Diana na Sheebah Karungi kutangaza kumaliza ugomvi wao kwenye listening party ya Stargal EP mwishoni mwa juma lilopita. Katika mahojiano na Galaxy FM Omutujju amesema wawili hao walitumia jambo hilo kutafuta mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni kwani haamini kama kweli warembo hao walizika tofauti zao kutoka kwa mioyo yao. Haikushia hapo Hitmaker huyo wa ngoma ya “Big Boys” ameenda mbali zaidi na kumtolea uvivu Spice Diana na meneja wake Roger Lubega kwa kusema kwamba ni wanafiki kwa sababu hawajawahi watakia mema wasanii wengine kwenye shughuli zao za kimuziki. Hata hivyo amehapa kuanika maovu yote ambayo Spice Diana na Roger Lubega wanafanya nyuma ya pazia hivi karibuni.

Read More
 RAPA GRAVITY OMUTUJJU AMSHUSHIA KICHAPO SHABIKI ALIYEMWAGIA DANCER WAKE KINYWAJI AKIWA JUKWAANI

RAPA GRAVITY OMUTUJJU AMSHUSHIA KICHAPO SHABIKI ALIYEMWAGIA DANCER WAKE KINYWAJI AKIWA JUKWAANI

Rapper kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju ameingia kwenye headlines mara baada ya kujikuta akimpiga teke shabiki yake kwenye moja ya performance yake wikiendi hii iliyopita. Shabiki huyo alimwagia kinywaji dancer wake Trisha Woodz akiwa jukwaani akiwaburudisha mashabiki, kitendo ambacho kilimkasirisha Gravity Omutujju ambaye alihamua kurusha teke kwa shabiki aliyehusika na kitendo hicho huku akimtolea maneno makali. Hata hivyo jambo hilo limezua mjadala mtandaoni ambapo baadhi ya watu wamehoji kuwa Gravity Omutujju alishusha brandy yake ya muziki kwa kitendo cha kumpiga teke shabiki yake huku wengine wakimuunga mkono kwa hatua ya kutaka kumuadhibu shabiki yake huyo.

Read More
 GRAVITY OMUTUJJU ATAJA ORODHA YA WASANII WA KIUME ANAOWAKUBALI NCHINI UGANDA, JINA LA NAVIO LAKOSEKANA

GRAVITY OMUTUJJU ATAJA ORODHA YA WASANII WA KIUME ANAOWAKUBALI NCHINI UGANDA, JINA LA NAVIO LAKOSEKANA

Rapper kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju amezua gumzo kwenye mutndao ya kijamii baada ya kuachia orodha ya wasanii bora wa kiume anaowakubali kwenye kiwanda cha muziki nchini humo. Kwenye bango ambalo ameshare kwenye mitandao yake ya kijamii kuitangaza ngoma yake mpya iitwayo Big Boys Omutujju amejitaja kama msanii bora akifutwa na Bebe Cool, Bobi Wine, Jose Chameleone, King Saha, Eddy Kenzo, Fik Fameika, Pallaso, David Lutalo, na Ziza Bafana lakini jina la Mpinzani wake kwenye muziki wa hiphop Navio limekosekana kwenye orodha hiyo. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Tusimbudde” ameenda mbali zaidi na kujinasibu kuwa wasanii ambao wamekosekana kwenye list yake hiyo sio wakubwa kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda na hivyo wanatakiwa kutia bidii kwenye kazi zao. Kama ilivyo kwa orodha ya wasanii yenye utata inayotolewa na msanii Bebe Cool, list hiyo ya Gravity Omutujju imezua gumzo miongoni mwa mashabiki wa wasanii waliokosekana kwenye orodha hiyo ambapo wamepuzilia mbali list hiyo kuwa batili kwa kusema kwamba ni ya kibaguzi. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameikubali orodha hiyo ya wasanii bora wa kiume iliyotolewa na Gravity Omutujju ambapo wamemtaka rapa huyo. Ikumbukwe Gravity Omutujju katika siku za hivi karibuni amekuwa akijiita mfalme wa  wa muziki wa Hiphop nchini Uganda, kitu ambacho wadau wa muziki nchini humo wanaamini kuwa Navio ndiye mfalme wa muziki wa hiphop kwani ndiye alianzisha utamaduni wakurap kwa lugha ya Luganda.

Read More
 RAPPER GRAVITY OMUTUJJU AKIRI HADHARANI KUACHA MUZIKI KWA AJILI YA KUINGIA KIFUA NDOA YAKE

RAPPER GRAVITY OMUTUJJU AKIRI HADHARANI KUACHA MUZIKI KWA AJILI YA KUINGIA KIFUA NDOA YAKE

Rapper asiyeishiwa na vituko kila leo kutoka nchini Uganda Gravity Omutujju amekiri kuwa ni heri aache muziki badala kumpa talaka mke wake. Akizungumza kuhusu familia yake katika mahojiano yake ya hivi karibuni Omutujju amesema anathimini sana mke wake na hawezi kumfanyia kitu kibaya kitakacho muumiza kiasaikolojia. Hitmaker huyo wa ngoma “Tusimbudde” amesema Mke wake alisamama nae kipindi chote alichokuwa amevulia kiuchumi hivyo ni vigumu kwake kumsaliti kutokana na kujitolea kwake kuhakikisha familia yake inasimama imara licha ya changamoto ya maisha. Hata hivyo amesema mewekeza pesa zake nyingi kwenye biashara ya ujenzi wa nyumba na shughuli zingine kuhakikisha ana ana kitega uchumi cha kustosha kwa ajili ya familia yake katika siku za usoni ambapo pia amedokeza mpango wake wa kuhalalisha ndoa yake hivi karibuni pindi tu atakapopata kipato kizuri. Utakumbuka Gravity Omutujju na mke wake Sharua Nakanyike wamekuwa kwenye ndoa tangu mwaka wa 2013 na wamejaliwa watoto watatu kwa pamoja.

Read More
 NINCE HENRY AMCHANA GRAVITTY OMUTUJJU KISA KUJIGAMBA KUWA AMEINGIZA PESA NYINGI KUMLIKO MSANII YEYOTE UGANDA

NINCE HENRY AMCHANA GRAVITTY OMUTUJJU KISA KUJIGAMBA KUWA AMEINGIZA PESA NYINGI KUMLIKO MSANII YEYOTE UGANDA

Msanii na mwandishi wa nyimbo kutoka nchini Uganda Nince Henry amemtolea uvivu rapa Gravitty Omutujju mara baada ya rapa huyo kujinasibu kuwa yeye ni moja kati ya wasanii waliopata shows nyingi baada ya uchumi wa nchi ya uganda kufunguliwa. Katika mahojiano yake na Galaxy FM Nince Henry amesema ameshangazwa na kitendo cha omuttujju kujigamba mitandaoni ambapo amesema  hakutarijia msanii huyo anaweza fanya jambo kama hilo ikizingatiwa kuwa umri wake hamruhusu kujihususha na mambo ya kijinga. Hitmaker huyo wa “Cinderella” amehoji kuwa baadhi ya wasanii wamepata shows nyingi kutokana na tasnia ya muziki nchini Uganda kufungwa kwa miaka miwili kufuatia janga la Corona, hivyo haoni kitu cha maana ambacho Gravitty Omutujju anajigamba nayo. Utakumbuka wiki iliyopita rapa Gravitty Omutujju alitangaza kuwa ameingiza pesa nyingi kutokana na shows ambazo amezipata licha ya watu kuubeza muziki wake ambapo alienda mbali na kusema kuwa haoni wasanii wanaodai muziki wao ni mzuri wakipata shows. Jambo hilo lilizua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii huku kila mtu akitoa maoni tofauti juu ya suala hilo.

Read More
 RAPA GRAVITY OMUTUJJU ATISHIA KUJITOA UHAI KISA MUZIKI

RAPA GRAVITY OMUTUJJU ATISHIA KUJITOA UHAI KISA MUZIKI

Rapa kutoka Uganda Gravity Omutujju ametoa wito kwa Rais Yoweri Museveni kutofunga tena uchumi wa taifa hilo kutokana na Corona. Rapa huyo ametishia kujitoa uhai kama rais wa Uganda Yoweri Museveni atasitisha tena matamasha ya muziki mara baada ya kufungwa kwa kipindi cha miaka miwili. Omutujju amesema ana mpango wa kuandaa shoo katika eneo la Cricket Oval jijini Kampala mwezi Februari mwaka huu ili aweze kupata pesa za kulipa madeni ambayo aliyapata kipindi cha Corona Kauli ya Omutujju imekuja mara baada ya rais Yoweri Museveni kutangaza kufungua tasnia ya muziki nchini humo tarehe 24 mwezi huu baada ya kusitishwa  kutokana na katazo la kuzuia msambao wa Corona.

Read More