WILLY PAUL AFUNGUKA SABABU ZA KUTOACHIA WIMBO WAKE NA GUCHI

WILLY PAUL AFUNGUKA SABABU ZA KUTOACHIA WIMBO WAKE NA GUCHI

Staa wa muziki nchini Willy Paul amefunguka sababu za kutoachia wimbo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki kati yake na msanii wa Nigeria Guchi. Kwenye mahojiano na Mungai Eve Willy Paul amesema video ya ngoma hiyo ilivuja mtandaoni, kitendo ambacho kilimkasirisha na kuamua kufutilia mbali mchakato wa kuachia wimbo huo. Lakini pia ameweka wazi chanzo cha kufuta video ya wimbo wake wa “Moyo” kwenye mtandao wa Youtube kwa kusema kuwa video ya wimbo huo haikuwa na ubora aliouhitaji, hivyo aliogopa itamshushia chapa au brand yake ya muziki. Willy paul ambaye amegonga vichwa vya habari kwa wiki moja sasa baada ya kuwekeza kwenye sekta ya matatu, anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Kesho.

Read More
 MR SEED ADOKEZA KOLABO NA GUCHI KUTOKA NIGERIA

MR SEED ADOKEZA KOLABO NA GUCHI KUTOKA NIGERIA

Mwimbaji nyota nchini Mr. Seed licha ya kuwa anaendela kufanya vizuri na wimbo wake “Pressure”, mkali huyo hataki kupoa, ametumia wikiendi hii iliyopita kurekodi ngoma mpya. Mr. Seed amepost misururu ya picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa studio na Guchi wakiwa wanarekodi, hali inayoashiria kuwa wawili hao wapo mbioni kuachia wimbo wa pamoja. Guchi amekuwa nchini kwa ajili ya tamasha lakr la kimuziki ambalo limekamilika wikindi iliyopita.

Read More
 GUCHI AKANUSHA KUFUNGIWA HOTELINI NAIROBI

GUCHI AKANUSHA KUFUNGIWA HOTELINI NAIROBI

Mwanamuziki wa Nigeria Guchi amekanusha madai yanayosambaa mtandaoni kuwa amefungiwa kwwnye moja ya hoteli jijini Nairobi kutokana na kushindwa kulipa pesa za chakula na malezi. Akizungumza na Nairobi Gossip Guchi amesema madai ya kufukuzwa kwenye hoteli alimokuwa anaishi kwa kusema kwamba promota ambaye alimleta Kenya anamweka vizuri huku akidokeza kuwa amehamia kwenye hoteli kubwa kutokana na wingi wa watu wanaomsimamia kimuziki. Hitmaker huyo wa ngoma ya Jeniffer amewataka mashabiki zake kupuzilia mbali madai hayo kwa kuwa promota wake ana uwezo wa kumpa kila kitu anachokihitaji. Kauli yake imekuja mara baada ya mmoja waandaji wa onesho lake hapa Kenya kudai kuwa Promota aliyempa mwaliko amefulia kiuchumi kiasi cha kushindwa kugharamia mahitaji ya msingi ya msanii wake Guchi. Jamaa huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa Guchi amekuwa akilala njaa lakini pia amekosa sehemu ya kulala. Guchi anatarajiwa kutumbuiza usiku wa leo nchini Kenya kwenye tamasha lake.

Read More