Meta Yazindua Instagram Kwenye TV
Kampuni ya Meta imetangaza rasmi kuanza kuweka app ya Instagram kwa watumiaji wa televisheni. Hatua hii inalenga kuwapa watumiaji fursa ya kutazama video za Reels kupitia screen kubwa za TV, badala ya kutegemea simu pekee. Kwa mujibu wa Meta, utekelezaji wa mpango huu umeanza kwa kushirikiana na Amazon Fire TV, huku ikipangwa kupanua huduma hiyo na kuipeleka kwenye majukwaa mengine ya televisheni siku zijazo. Instagram kwenye TV itakuwa na muonekano wa Channels, unaowezesha watazamaji kufuatilia maudhui mbalimbali yakiwemo michezo, burudani na muziki. Meta imesema mfumo huo utaruhusu watu wengi kutazama kwa pamoja kwenye TV moja bila kuonyesha taarifa binafsi kama mazungumzo ya faragha au data za mtumiaji. Hatua hii inalenga kulinda faragha na kufanya matumizi yawe salama kwa familia, hali inayofanana na majukwaa ya YouTube na Netflix. Hatua ya Meta inafuatia mwelekeo wa mitandao ya kijamii kuingia kwenye soko la televisheni na video streaming. Ikumbukwe kuwa TikTok ilianza kupatikana kwenye TV tangu mwaka elfu mbili na ishirini.
Read More