Jovial Aonya Wasichana Kuhusu Safari ya Uzazi
Nyota wa muziki kutoka Kenya, Jovial, amewapa changamoto mabinti wenye mioyo dhaifu kufikiria mara mbili kabla ya kuingia kwenye safari ya ujauzito na kujifungua. Kupitia Instastory, Jovial amefunguka kuhusu changamoto ambazo amekutana nazo wakati wa ujauzito na hata baada ya kujifungua, akisema kuwa ni safari yenye kuhitaji nguvu za mwili na akili. Amesema amekosa usingizi kutokana na usumbufu wa mtoto mchanga, hali ambayo imemfanya atambue kwa undani ugumu wa safari ya uzazi. Lakini pia kipindi hiki kimempa mtazamo mpya juu ya nguvu na uvumilivu unaohitajika na mama katika malezi ya mtoto. Kwa mujibu wake, pamoja na furaha kubwa ya kumpakata mtoto, hatua ya uzazi huambatana na changamoto ngumu kama uchovu wa mwili, mabadiliko ya homoni, na msongo wa mawazo unaoweza kuathiri afya ya mama. Hata hivyo amesema kuwa lengo lake si kuwatisha wasichana, bali ni kuwasisitizia umuhimu wa maandalizi ya kisaikolojia na kifedha kabla ya kuingia kwenye hatua ya uzazi.
Read More