Penzi la Willy Paul lampa Jovial umaarufu mtandaoni

Penzi la Willy Paul lampa Jovial umaarufu mtandaoni

Msanii nyota nchini Jovial amekiri kupata mashabiki wengi wanaofuatilia kazi zake tangu atangaze kuingia kwenye mahusiano na Willy Paul. Kupitia insta story mrembo huyo ameshindwa kuficha furaha yake kwa kusema kwa kipindi chote cha maisha ya muziki hajawahi pata idadi kubwa ya watu wanaotazama nyimbo zake pamoja na kutembelea mitandao yake ya kijamii licha ya kushirikiana na wasanii mbali mbali kwenye suala la kuachia nyimbo kali. Katika hatua nyingine Mrembo huyo amesema ameshangazwa namna watu wanavyomshambulia  na Willy Paul kwa kujihusisha na kiki mtandaoni ilhali hawaungi mkono kazi za wasanii wachanga wanaotoa muziki mzuri bila kutengeneza matukio. Hata hivyo amemaliza kwa kuachia Wakenya swali kama wanaunga mkono muziki mzuri au umbea ambapo mashabiki wengi wameonekana kusisitiza umuhimu wa wasanii kutoa muziki mzuri sambamba na kutengeneza matukio yatakayowafanya wazungumziwe mtandaoni kama njia ya kujitangaza kimuziki.

Read More
 Vdeo ya wimbo wa Willy Paul “Lalala” yafutwa Youtube

Vdeo ya wimbo wa Willy Paul “Lalala” yafutwa Youtube

Video ya wimbo wa Willy Paul ‘Lalala ambao amemshirikisha Jovial imeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na malalamiko ya hakimiliki. Kwa sasa video hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya view laki 3 haipatikani kwenye mtandao huo kufuatia malalamiko ya hakimiliki kutoka kwa King Jones Official. Hata hivyo Willy Paul hajatoa tamko lolote kuhusu kufutwa kwa video ya wimbo wa mambo yote youtube. Ikumbukwe mtandao wa Youtube hauruhusu kutumia kazi au kionjo cha mtu mwengine bila makubaliano.

Read More
 ERIC OMONDI AKOSHWA NA MATUKIO YA WILLY PAUL NA JOVIAL, ATAKA WASANII WAFUATE NYAYO ZAO

ERIC OMONDI AKOSHWA NA MATUKIO YA WILLY PAUL NA JOVIAL, ATAKA WASANII WAFUATE NYAYO ZAO

Mchekeshaji kutoka Kenya Eric Omondi amekoshwa na kile kinachoendelea mtandaoni kati ya msanii Willy Paul na Jovial. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi amewapongeza wawili hao kwa hatua ya kuhalalisha mahusiano mtandaoni kitendo ambacho amehoji ni ubunifu wa hali ya juu wa kutengeneza matukio yatakayowasaidia kutangaza muziki wao mtandaoni. Mchekeshaji huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipigana kwa udi na uvumba kutetea muziki wa Kenya, amesema kuwa kwa sasa ni vigumu kwa msanii kupata mafanikio makubwa pasi na kuwa na matukio yatakao mfanya awe gumzo kwa mashabiki zake. Hata hivyo amewapa changamoto wasanii kuwa wabunifu ili kutengeneza maudhui ya burudani yatakayo jenga gumzo kwa mashabiki wao na kupitia njia hiyo wataweza kushinda na wasanii wa kimataifa.

Read More
 JOVIAL AWAJIBU WANAOMTAKA KUTOA MSAADA KWA JAMII

JOVIAL AWAJIBU WANAOMTAKA KUTOA MSAADA KWA JAMII

Mkali wa sauti na maandishi ya muziki, Jovial, amewatolea uvivu baadhi ya watu wanaomshinikiza kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji kwenye jamii. Kupitia instastory yake, Hitmaker huyo wa ‘Mi Amor’ amefichua kwamba amekuwa akipokea jumbe nyingi (DM) kutoka kwa mashabiki, wakihoji kwa nini hawasaidii watu wenye uhitaji na wasanii chipukizi wakati ana mafanikio makubwa kwenye muziki. Akipuzilia mbali pendekezo hilo, Jovial amesema kumsaini msanii kwenye lebo ya muziki ni biashara yenye athari za kisheria huku akisisitiza kuwa suala la kutoa misaada kwa jamii sio la kutangazwa au kuonyeshwa kwenye mitandao ya kijamii bali ni siri kati yake na mwenyezi Mungu. “The emotional blackmail on DM, about giving back to the society, specifically signing new artistes. Well giving back is a secret between me and my God, I do not do the social media parade,” Jovial alisema. “And please let us be exposed, signing an artist is not giving back to the community, it is business. I sign you, and you bring me money, You screw up, and I take you to court,” aliongeza.

Read More
 JOVIAL ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA EP YAKE MPYA

JOVIAL ATHIBITISHA KUKAMILIKA KWA EP YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini Jovial kwa mara ya kwanza ametusanua kuhusu maendeleo ya EP yake mpya ambayo itaingia sokoni ndani ya mwaka huu. Kupitia Inststory yake kwenye mtandao wa Instagram yake Jovial amethibitisha kukamilika kwa EP hiyo ambayo amedai kuwa ni ya kitofauti kwa sababu imebeba nyimbo ambazo ameimba kwenye mitindo mbali mbali. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Jeraha” amesema kutayarisha EP hiyo haijakuwa jambo rahisi kwake kwa kuwa amepitia changamoto nyingi ambazo amedai nusra zimekatishe tamaa ila kwa sasa anamshukuru kwa kumsimamia hadi kukamilika kwa EP yake mpya. Mrembo huyo amewashukuru maprodyuza waliohusika kwenye uandaji wa EP yake kwa kusema bado anafanya marekebisho kwa baadhi ya nyimbo kabla ya kuachia rasmi ep yake. Hata hivyo hajatuambia jina ya EP, idadi ya ngoma itakayopatikana kwenye ep hiyo na tarehe rasmi ambayo ataachia kazi hiyo kwa mashabiki zake ila ni jambo la kusubiriwa.

Read More
 JOVIAL ADOKEZA UJIO WA EP YAKE MPYA

JOVIAL ADOKEZA UJIO WA EP YAKE MPYA

Msanii nyota nchini Jovial amedokeza ujio wa EP yake mpya ambayo itaiachia ndani ya mwaka huu wa 2022. Katika mahojiano na Mungai Eve, Jovial amesema kwa sasa yupo chimbo anaanda EP mpya ambayo amedai kuwa itakuwa na ladha ya kitofauti sana kutokana na wasanii atakaowashirikisha kwenye kazi hiyo. Licha ya kutoweka wazi idadi ya ngoma na tarehe ambayo  Ep yake hiyo itaingia sokoni, Jovial amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kupokea ujio wake mpya ambao utakuwa wa moto wa kuotea mbali sana. Utakuwa mapema mwaka wa 2020 Jovial aliahidi mashabiki zake kwamba ataachia EP mpya lakini hakufanikiwa kufanya hivyo kutokana msala wa Corona jambo ambalo lilimpelekea kusitisha mchakato mzima wa kutayarisha project hiyo.

Read More
 JOVIAL AWACHANA WANAOKOSOA KWA KUCHEZA KIMAHABA NA RASHID ABDALLA

JOVIAL AWACHANA WANAOKOSOA KWA KUCHEZA KIMAHABA NA RASHID ABDALLA

Msanii wa kike nchini Jovial amewatolea uvivu wanaomkosoa kwa kucheza kimahaba na Rashid Abdalla ambaye ni mume wa mwanahabari maarufu nchini Lulu Hassana kwenye birthday yake juzi kati. Kupitia instastory kwenye mtandao wa Instagram Jovial amesema ameshangazwa na hatua ya wanawake kumshambulia mitandaoni kwa kitendo cha kucheza kimahaba na rashid abdalla huku akisema jambo hilo inaonyesha ni jinsi gani wanawake wanamuonea wivu mitandaoni wana matatizo mengi kwenye ndoa zao. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mi Amor” amesema hakuwa na nia ya kumnyanganya lulu hassan mume wake kama wengi wanavyodai kwenye mitandao ya kijamii kwani alikuwa anatoa tu burudani kwa watu waliokuwa wamehudhuria hafla ya kusherekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa mwanahabari huyo. Hata hivyo amewataka wanawake wanaomkosoa kutatua changamoto zinazowakumba kwenye ndoa zao badala ya kumzushia madai ambayo hayana msingi wote mitandaoni akiwa kwenye shughuli inayomuingizia riziki. Kauli Jovial imekuja mara kupata ukosoaji mkubwa kutoka kwa walimwengu kutokana na video inayosambaa mtandaoni ikimuonyesha akicheza kimahaba na Rashid Abdalla kwenye  birthday yake kitendo kilichomfanya Lulu hassan aingilie kati kumzuia msanii huyo asiendelee kucheza na mume wake kimahaba zaidi kwenye performance yake.

Read More
 JOVIAL AKOSESHWA AMANI NA SHABIKI KISA MAPENZI

JOVIAL AKOSESHWA AMANI NA SHABIKI KISA MAPENZI

Staa wa muziki nchini Jovial ameshindwa kumvumilia shabiki yake mmoja ambaye amemkosesha amani kwa kudai kuwa ana mapenzi dhati kwake. Kupitia instastory kwenye mtandao wa instagram jovial amesema shabiki huyo ameenda mbali zaidi na kuanza kuwalipa watu kumfuatilia sehemu anayoishi na maeneo anayotembea. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pita Nawe Remix” amesema amejaribu kumu-block mtu huyo na hata kumtishia atampeleka polisi lakini ameshindwa kubadilisha mienendo ya shabiki huyo ambaye anadai anampenda kwa dhati. Hata hivyo amewataka mashabiki zake wamsaidie kumkomesha shabiki huyo msumbufu huku akisema amechoka kukaa kimya kwani jambo hilo limeanza kumpa uwoga katika maisha yake.  

Read More
 JOVIAL AWEKA WAZI MATAMANIO YA KUFANYA KAZI NA OXLADE KUTOKA NIGERIA

JOVIAL AWEKA WAZI MATAMANIO YA KUFANYA KAZI NA OXLADE KUTOKA NIGERIA

Msanii wa kike nchini Jovial amedokeza mpango wa kufanya kazi ya pamoja na mwanamuziki kutoka nigeria Oxlade. Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Jovial amesema anatamani kushirikiana na Oxlade kwenye wimbo wa pamoja kwa kuwa  yeye ni shabiki mkubwa wa hitmaker huyo wa ngoma ya Ojuju . Ujumbe ambao umewaaminisha watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii huenda wawili hao wana wimbo wa pamoja ambao utatoka hivi karibuni. Utakumbuka mapema mwaka huu Jovial aliweka wazi kwamba hatofanya kolabo na msanii yeyote kwa kuwa ameshashirikisha na wasanii wengine kwenye nyimbo zao hivyo ni wakati wake wa kuachia nyimbo zake mwenyewe kama msanii wa kujitegemea licha ya kupokea maombi mengi. Hata hivyo alienda mbali zaidi na kusema kolabo ambazo zitatoka mwaka huu alizoshirikishwa na wasanii wengine ni zile alizofanya mwaka jana. Jovial ambaye anafanya vizuri na wimbo wa Mi Amor alioshirikishwa na Marioo tayari ameshirikiana na wasanii kama Mejja, Khaligraph Jones, Arrow Boy, Otile Brown na wengine wengi.

Read More
 JOVIAL ATOA ONYO ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE

JOVIAL ATOA ONYO ANGALIZO KWA MASHABIKI ZAKE

Msanii kike nchini Jovial ametoa onyo kwa mashabiki zake ambao kwa njia moja au nyingine wana mpango wa kumdhalalisha kijinsia akiwa jukwaani. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram msanii huyo amesema kuanzia sasa atakuwa anapambana moja kwa moja na shabiki atakayejaribu kumshika vibaya akiwa jukwaani anatambuiza huku akisisitiza kuwa atamshushia kichapo kabla walinzi wake awajaingilia kati Kauli yake Jovial imekuja mara baada ya shabiki yake mmoja wikiendi hii iliyopita kwenye performance kumvamia akiwa jukwaani na kumshika makalio pasi na idhini jambo ambalo lilimfanya kusitisha show yake kwa muda. Hata hivyo mashabiki walionekana kwa kughabishwa na kisa hicho ambapo wamewataka waandaji wa matamasha ya muziki kuwapa ulinzi wa kutosha wasanii wanapoalikwa kufanya shows kwenye matamasha yao

Read More
 JOVIAL AKIRI KUTOMSAMEHE MWANAUME ANAYEMKIMBIA MKE WAKE AKIWA MJA MZITO

JOVIAL AKIRI KUTOMSAMEHE MWANAUME ANAYEMKIMBIA MKE WAKE AKIWA MJA MZITO

Female singer kutoka Kenya Jovial amefunguka na kudai kwamba hatokuja kumsamehe mwanaume yeyote anayemtelekeza mwanamke akiwa mja mzito kwani ujauzito ni kama ugonjwa. Kupitia Whatsapp Story yake Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pita Nawe” ameandika ujumbe unaosomeka “Siwezi msamehe mwanaume anayemtelekeza mwanamke mjamzito mimba ni kama ungojwa asikuambie mtu unahitaji upendo wote mshukuru Mungu “ Kauli yake Jovial imekuja mara baada ya chapisho la mwanamke mmoja kusambaa mtandaoni akieleeza namna alivyotelekezwa na mpenzi wake akiwa mjamzito na baada ya kupata usaidizi kutoka kwa mwanaume mwingine,mpenzi wake wa zamani sasa anataka warudiane tena ikiwa ni miaka mitano tangu amkimbie.

Read More
 JOVIAL AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA DJ SAMI FLINCH

JOVIAL AKANUSHA KUTOKA KIMAPENZI NA DJ SAMI FLINCH

Female singer kutoka Kenya Jovial amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa anatoka kimapenzi na DJ maarufu nchini Sami Flinch. Katika kikao cha maswali na mashabiki zake kwenye mtandao wa Instagram Jovial amesema madai hayo hayana msingi wowote huku akisema ukaribu wao ulitokana na shughuli za kikazi ambazo walikuwa nayo kipindi cha nyuma. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Pita Nawe” amesema kwa ngazi aliyofika kwa sasa anahitaji zaidi pesa kuliko mpenzi huku akithibitisha kuwa hayupo kwenye mahusiano. Hata hivyo amesema skendo za mtandaoni hazina nafasi kwa sasa katika maisha yake kwani anahitaji kuacha mashabiki wake wapate wanachostahili kupitia muziki wake.

Read More