Tiktoker Kabuda Ajitetea Kuhusu Tabia ya Kula Chakula Kingi Kupitia Wimbo

Tiktoker Kabuda Ajitetea Kuhusu Tabia ya Kula Chakula Kingi Kupitia Wimbo

Tiktoker kutoka Kenya aitwaye Kabuda ameibua gumzo mitandaoni baada ya kujibu wakosoaji wake kwa kutumia wimbo “Sipangwingwi” wa msanii Exray. Kabuda, ambaye mara kwa mara hukosolewa kuhusu tabia yake ya kupenda kula chakula kingi, ameamua kujitetea kwa njia ya ubunifu na ucheshi kupitia video aliyochapisha mtandaoni. Katika video hiyo ambayo imeanza kusambaa kwa kasi, Kabuda anaonekana akivibe na kuimba kwa hisia kipande cha wimbo huo maarufu, akisisitiza kauli kwamba maisha ni yake na hakuna mtu anayepaswa kumwelekeza cha kufanya. Ujumbe huo umeonekana kama jibu la moja kwa moja kwa watu wanaomshauri kupunguza kula au kubadili tabia zake, huku akionyesha kwamba haungi mkono shinikizo la mitandaoni kuhusu mwonekano au mtindo wa maisha.

Read More
 Kabuda Apuuza Ushauri wa Wafuasi wake Kuhusu Ulaji wa Junk Foods

Kabuda Apuuza Ushauri wa Wafuasi wake Kuhusu Ulaji wa Junk Foods

Mtengeneza maudhui wa vyakula mtandaoni, anayefahamika kama Kabuda, amepuzilia mbali miito ya baadhi ya wafuasi wake wanaomtaka apunguze ulaji wa junk food kutokana na athari za kiafya. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Kabuda amesisitiza kwamba hana mpango wa kubadili anavyokula na kwamba anaamini mwili mpya atapewa mbinguni. Kwa muda mrefu, Kabuda amekuwa akivutia watazamaji kupitia video zake za kula vyakula vikubwa na vya mafuta, lakini wengi wameeleza wasiwasi kutokana na unene wake wa kupitiliza. Wanasema mtindo wake huo unaweza kumweka kwenye hatari ya magonjwa kama presha, kisukari na matatizo ya moyo. Licha ya mijadala hiyo, Kabuda anaendelea kupakia video mpya za kula bila kuonyesha dalili za kupunguza kasi, na mjadala kuhusu usalama wa maudhui yake unaendelea kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Read More