LifeStyle

Kabuda Apuuza Ushauri wa Wafuasi wake Kuhusu Ulaji wa Junk Foods

Kabuda Apuuza Ushauri wa Wafuasi wake Kuhusu Ulaji wa Junk Foods

Mtengeneza maudhui wa vyakula mtandaoni, anayefahamika kama Kabuda, amepuzilia mbali miito ya baadhi ya wafuasi wake wanaomtaka apunguze ulaji wa junk food kutokana na athari za kiafya.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Kabuda amesisitiza kwamba hana mpango wa kubadili anavyokula na kwamba anaamini mwili mpya atapewa mbinguni.

Kwa muda mrefu, Kabuda amekuwa akivutia watazamaji kupitia video zake za kula vyakula vikubwa na vya mafuta, lakini wengi wameeleza wasiwasi kutokana na unene wake wa kupitiliza. Wanasema mtindo wake huo unaweza kumweka kwenye hatari ya magonjwa kama presha, kisukari na matatizo ya moyo.

Licha ya mijadala hiyo, Kabuda anaendelea kupakia video mpya za kula bila kuonyesha dalili za kupunguza kasi, na mjadala kuhusu usalama wa maudhui yake unaendelea kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *