Mashabiki wa Kanye West Wadai Pesa Zao Baada ya Onyesho la Aibu Shanghai

Mashabiki wa Kanye West Wadai Pesa Zao Baada ya Onyesho la Aibu Shanghai

Mashabiki wa mwanamuziki Kanye West wamelalamikia vikali onyesho lake lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Shanghai, wakimtuhumu kwa kuwasaliti na kudai warejeshewe pesa zao. Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo kwenye tamasha hilo, Kanye alichelewa kuingia jukwaani kwa zaidi ya dakika 45 na alipoanza kutumbuiza, alionekana kulip-synch kwa sehemu kubwa ya onyesho hilo badala ya kuimba moja kwa moja. Tukio hilo liliwakasirisha mashabiki waliokuwa wamelipia tiketi kwa matarajio ya kumuona msanii huyo kwa ubora wake wa kawaida. Baadhi yao walionekana wakipaza sauti kwa pamoja wakisema “refund! refund!” wakiashiria kutoridhishwa kwao na maonesho hayo. Hadi sasa, Kanye West bado hajatoa tamko lolote rasmi kuhusu tukio hilo ambalo limezua mjadala mkali mitandaoni, huku wengine wakisema hali hiyo ni mwendelezo wa tabia zisizoeleweka kutoka kwa rapa huyo ambaye amekumbwa na migogoro mingi ya kipekee miaka ya hivi karibuni.

Read More
 Lauren Pisciotta Aibuka na Madai Mapya Dhidi ya Kanye West

Lauren Pisciotta Aibuka na Madai Mapya Dhidi ya Kanye West

Aliyekuwa Msaidizi wa rapa Kanye West, Lauren Pisciotta ameibuka tena na tuhuma nzito za unyanyasaji dhidi ya rapa huyo na safari hii amedai kuwa Kanye alimfanyia mambo mengi mazito kuliko hata yale aliyowahi kuyaeleza mwaka jana. Katika malalamiko mapya Pisciotta anadai Kanye alimfanyia mambo mengi mabaya, ikiwemo shambulio la ngono, unyanyasaji wa kijinsia, uviziaji na mengine mengi pamoja na tukio la kumbusu mdomoni kwa lazima na kumuuliza jinsi sehemu zake za siri zilivyo wakati wakiwa hotelini kwenye safari ya kikazi huko San Francisco. Itakumbukwa kuwa mwaka jana mwadada huyo aliibuka kwa mara ya kwanza kumshtaki Kanye West kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na kumsimamisha kazi kinyume cha sheria ingawa msanii huyo aliyapuuza na kuyakejeli madai hayo kupitia mitandao ya kijamii.

Read More
 Kanye West Azuiliwa Kuingia Australia Kufuatia Wimbo Unaomsifu Adolf Hitler

Kanye West Azuiliwa Kuingia Australia Kufuatia Wimbo Unaomsifu Adolf Hitler

Rapa maarufu wa Marekani, Kanye West, amezuiliwa kuingia nchini Australia kufuatia wimbo wake mpya unaodaiwa kumsifu kiongozi wa zamani wa kinazi, Adolf Hitler. Maamuzi hayo yamezua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, huku viongozi wa Australia wakisisitiza msimamo wa nchi hiyo dhidi ya misimamo ya chuki na itikadi kali. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, mamlaka ya uhamiaji ya Australia ilikataa ombi la West la kuingia nchini humo kwa kile walichokitaja kama “tabia na matamshi yanayokiuka maadili ya taifa.”  Wimbo huo wa Kanye ‘Heil Hitler’, uliotoka mapema mwezi wa Mei, umekosolewa vikali kwa kile kinachoonekana kuwa ni kusifia au kupuuza maovu ya utawala wa Hitler. Waziri wa Uhamiaji wa Australia, Andrew Giles, alisema katika taarifa kwamba taifa hilo lina sera kali dhidi ya hotuba za chuki na kwamba yeyote anayehusishwa na misimamo ya chuki au ushawishi wa kiitikadi za kikandamizaji hatakaribishwa. “Hatutaruhusu mtu yeyote kuingia nchini mwetu ambaye anahatarisha mshikamano wa kijamii au anayepuuza historia ya mateso ambayo watu wengi duniani walipitia,” alisema Giles. Kanye West, ambaye amekuwa kwenye mzozo wa mara kwa mara na vyombo vya habari na mashirika mbalimbali kutokana na kauli tata kuhusu Uyahudi na historia ya Holocaust, amekuwa akilaumiwa kwa kutumia jukwaa lake la muziki kusambaza ujumbe wa mgawanyiko. Hadi sasa, West hajatoa taarifa rasmi kuhusu hatua hiyo ya Australia, lakini wasimamizi wake wametaja kuwa wanapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Read More
 Kanye West Aonyesha Furaha Baada ya Larry Hoover Kumpunguzia Kifungo, Atoa Shukrani kwa Drake

Kanye West Aonyesha Furaha Baada ya Larry Hoover Kumpunguzia Kifungo, Atoa Shukrani kwa Drake

Msanii maarufu wa Marekani, Ye (Kanye West), ameonyesha furaha yake baada ya Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump, kupunguza kifungo cha aliyekuwa kiongozi wa genge kutoka Chicago, Larry Hoover. Ye alionyesha shukrani kwa msanii mwenzake Drake kwa mchango wake katika juhudi za kumkomboa Hoover, akitambua ushirikiano wao kama sehemu muhimu ya mafanikio haya. “THANK YOU DRAKE FOR HELPING TO BRING LARRY HOOVER HOME.”, Aliandika X Ye na Drake waliweka tofauti zao kando na kuungana kwa tamasha la pamoja mnamo mwaka 2021, likiwa ni sehemu ya kampeni ya kumtetea Hoover na kushinikiza kuachiliwa kwake. Tamasha hilo liliitwa Free Larry Hoover Benefit Concert na lilileta msukumo mkubwa kwa umma na viongozi kuhusu kesi ya Hoover. Larry Hoover alikuwa akitumikia kifungo cha maisha kwa makosa ya uhalifu wa genge, lakini amekuwa akihusishwa na mabadiliko chanya akiwa gerezani. Uamuzi wa kupunguziwa kifungo wake umetajwa na baadhi ya watu kama hatua ya kihistoria katika juhudi za mageuzi ya mfumo wa haki nchini Marekani. Kwa Ye, huu ni ushindi mkubwa kwa familia ya Hoover na kwa wale wanaoamini katika nafasi ya pili na msamaha wa kweli.

Read More
 Kanye West Apigwa Marufuku na Kim Kuwakaribia Watoto Wao

Kanye West Apigwa Marufuku na Kim Kuwakaribia Watoto Wao

Mwanamitindo maarufu Kim Kardashian ametoa onyo kali kwa aliyekuwa mume wake, msanii Kanye West, akimtaka akae mbali na watoto wao, licha ya kuwa wanashirikiana kwenye ulezi wa pamoja (joint custody). Taarifa hiyo imesababisha gumzo kubwa mitandaoni huku mashabiki wakigawanyika kuhusu hatua hiyo ya Kim. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na familia hiyo, Kim ameweka wazi kwamba hataki Kanye awe karibu na watoto wao bila ruhusa maalum, akidai kuwa vitendo na tabia za hivi karibuni za rapa huyo ni zisizotabirika na huenda zikahatarisha utulivu wa watoto. Hali hiyo inazua maswali kuhusu mustakabali wa mpango wao wa ulezi wa pamoja, hasa ikizingatiwa kuwa Kim na Kanye walikubaliana kushirikiana kulea watoto wao wanne baada ya talaka yao mwaka wa 2022. Mashabiki mitandaoni wametoa maoni mseto, wengine wakimuunga mkono Kim kwa kutanguliza maslahi ya watoto, huku wengine wakimtetea Kanye na kusema anapaswa kuruhusiwa kuwa sehemu ya maisha ya watoto wake. Mpaka sasa, Kanye hajatoa kauli rasmi kuhusu tishio hilo, lakini wengi wanatarajia majibu yake, hasa kutokana na historia yake ya kujibu hadharani kupitia mitandao ya kijamii.

Read More
 Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Ushahidi wa Kid Cudi Dhidi ya Diddy Wamvunja Moyo Kanye West

Rapa maarufu mwenye utata, Kanye West, ametoa hisia zake kuhusu hali inayoendelea kumkumba Sean Diddy Combs, akieleza masikitiko yake juu ya hatua ya Kid Cudi kutoa ushahidi dhidi ya Diddy. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Ye ameonekana kuzungumzia kile anachokiona kama mfumo wa haki unaowakandamiza watu weusi, akisisitiza haja ya jamii ya wasanii na Wamarekani Weusi kwa ujumla kujilinda na kushikamana badala ya kushirikiana na mifumo anayoamini kuwa ya kibaguzi. “I wish Cudi hadn’t testified against Puff. We need to not be locked in white systems. Praying for Puff and his family. Praying for Puff Daddy and the Family.”Aliandika X Kauli hiyo imeibua hisia mseto kutoka kwa mashabiki na wanamuziki wenzake, huku baadhi wakimtetea kwa msimamo wake wa kutaka mshikamano miongoni mwa wasanii wa asili ya Kiafrika, na wengine wakimkosoa kwa kudharau mchakato wa haki. Kid Cudi, ambaye zamani alikuwa rafiki wa karibu wa Ye, anatajwa kuwa miongoni mwa mashahidi waliotoa ushahidi dhidi ya Diddy kufuatia madai mazito yanayomkabili kuhusu vitendo vya unyanyasaji na ukiukaji wa haki.

Read More
 Ye Aomba Msamaha kwa Mungu, Atangaza Kuachana na Chuki Dhidi ya Wayahudi

Ye Aomba Msamaha kwa Mungu, Atangaza Kuachana na Chuki Dhidi ya Wayahudi

Rapa mwenye utata na mabadiliko ya ghafla, Kanye West, anayejulikana pia kama Ye, ameandika ujumbe mzito wa toba kupitia mtandao wa X (zamani Twitter), akiomba msamaha kwa Mungu kwa maumivu aliyowahi kusababisha, huku akitangaza kuwa amewasamehe wote waliomuumiza. Katika ujumbe huo uliojaa hisia, Ye alisema ameacha kabisa chuki aliyokuwa nayo dhidi ya Wayahudi, na sasa anawapenda watu wote bila ubaguzi. “Nimeomba msamaha kwa Mungu. Nimewasamehe waliotenda mabaya dhidi yangu, na sasa nawafurahia wanadamu wote,” aliandika rapa huyo. Ye pia aligusia mawasiliano ya karibu na watoto wake, akieleza kuwa waliwasiliana naye kwa FaceTime tu,kio lililomgusa sana na kuonekana kuwa na nafasi maalum katika mabadiliko yake ya kiroho na kibinadamu. Ujumbe wake umezua maoni mseto miongoni mwa mashabiki. Wengine wamepokea hatua hiyo kama mwanzo mpya kwa msanii huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa matamshi yenye utata na msimamo mkali kuhusu masuala ya kidini, kisiasa na kijamii. Tangazo hili linakuja baada ya kipindi kirefu cha shutuma nzito kutokana na matamshi yake yaliyotafsiriwa kama chuki dhidi ya Wayahudi, na hata kusababisha kupoteza mikataba mikubwa ya kibiashara. Toba yake sasa imechukuliwa kama jaribio la kurejesha uhusiano na jamii na pia kurekebisha taswira yake kwa umma. Hadi sasa, ujumbe huo tayari umepata maelfu ya likes na maoni, wengi wakisubiri kuona kama mabadiliko haya ni ya kudumu au ni sehemu nyingine ya mzunguko wa tabia za Ye ambazo mara nyingi husababisha taharuki mitandaoni.

Read More
 Kanye West atuhumiwa kuvunja simu ya shabiki

Kanye West atuhumiwa kuvunja simu ya shabiki

Rapa Kanye West ametajwa kama mtuhumiwa katika uchunguzi wa tukio la kihalifu. Hii inakuja mara baada ya kusambaa kwa video ikimuonesha Kanye akijibizana na paparazzi pamoja na shabiki. Video hiyo ilionesha kuwa kanye ni kama aliweuka ambapo alimjia juu shabiki huyo wa kike akidai kuwa amekuwa akimfuatilia na baada ya hapo alionekana akimpora simu shabiki huyo na kuitupilia mbali. Lakini pia kanye anaoneshwa kukerwa sana sehemu mbalimbali na tabia za paparazzi ambao wamekuwa wakimfuatilia mpaka kwenye maisha yake binafsi. Sasa kwenye video hiyo pia Kanye anaonekana akiwaambia paparazzi kwamba anataka kuwaona watoto wake bila ya wao kumpiga picha. Kanye alikuwa anaenda kuwaona watoto wake kwenye mchezo wa basketball.

Read More
 Kanye West amjia juu Paparazzi kwa kumpiga picha bila ridhaa yake

Kanye West amjia juu Paparazzi kwa kumpiga picha bila ridhaa yake

Rapa Kanye West ameamua kuwa mstaarabu kwa paparazzi ambao wamekuwa wakinasa matukio yake hasa akiwa kwenye mishe zake. Sasa Jana alionekana akimzuia Paparazzi mmoja ambaye alijaribu kumrekodi akiwa na mkewe Bianca Censori. Kanye alimwambia Paparazzi huyo aache anachokifanya na kusema kwamba inabidi watu maarufu wawe wanapata asilimia fulani ya malipo kutoka kwenye picha na maudhui ambayo Paparazzi wamekuwa wakiyachukua kwao na kuuza au kuyatumia kwenye vyombo vyao vya habari.

Read More
 Kanye West kupewa taarifa kupitia gazeti

Kanye West kupewa taarifa kupitia gazeti

Timu ya wanasheria wa Kanye West wamepanga kutumia njia ya Gazeti kumfikishia taarifa rapa huyo kuwa wamemtema rasmi na hawatamuwakilisha tena kwenye masuala yake ya kimahakama. Kwa mujibu wa TMZ, timu hiyo ya wanasheria imesema kwamba, kumekuwa na tatizo la mawasiliano kati yao ambapo YE ame-deactivate namba yake ya simu ambayo walikuwa wakiwasiliana naye awali.

Read More
 Kanye West afunga ndoa ya siri na mfanyikazi wake

Kanye West afunga ndoa ya siri na mfanyikazi wake

Rapa kutoka Marekani Kanye West ameripotiwa kufunga ndoa tena baada ya kuachana na Baby Mama wake Kim Kardashian. Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, YE amefunga ndoa na mwanamke aitwaye Bianca Censori ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yake ya Yeezy, akihudumu kama mbunifu wa usanifu yaani Architectural designer. Mapaparazzi wa TMZ wamekinasa kidole cha YE kikiwa na Pete ya ndoa, ambapo inatajwa ndoa hiyo ilikuwa ya siri. Mapema wiki hii Kanye West alionekana na mwanamke huyo ambaye alikuwa ametia nywele za blonde kichwani, wakipata chakula kwenye mgahawa mmoja mjini Beverly Hills.

Read More
 Rapa Kanye West aripotiwa kutoonekana kwa wiki kadhaa

Rapa Kanye West aripotiwa kutoonekana kwa wiki kadhaa

Rapa Kanye West ameripotiwa kutoonekana kwa wiki kadhaa na hata kwenye mawasiliano yake hapatikani. Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizodakwa na Radaronline.com, meneja wake wa zamani, Thomas St. John amenukuliwa akisema kuwa amepata shida ya kumtafuta rapa huyo kwa kipindi cha wiki mbili sasa . Kwa mujibu wa mtando wa TMZ, vyanzo vya karibu na familia ya Kanye West vimedai kuwa rapa huyo anasumbuliwa tena na matatizo ya akili, ambayo awali mwenyewe amewahi kuthibitishwa kuwa nayo. Inadhaniwa kuwa matatizo hayo yanaweza yakawa ndio chanzo kilichopelekea kutoa kauli za utata katika siku za hivi karibuni. Utakumbuka mwaka wa 2016, Kanye West alilazimika kusitisha show zake 21 baada ya kulazwa hospitalini kwa matatizo ya kiakili.

Read More