Kim Kardashian akiri kupata ugumu kulea watoto na Kanye West
Rapa Kanye West anampa wakati mgumu sana Baby Mama wake Kim Kardashian hasa kwenye malezi ya watoto wao baada ya kuachana. Kwenye mahojiano na Podcast ya Mtangazaji Angie Martinez, Kim amesema kushiriki kwenye suala la malezi na YE ni jambo gumu sana. “It’s hard. Co-parenting, it’s really fu**ing hard.”, Alisema kwa masikitiko. Aidha Kim Kardashian amedai kuwa hataki tofauti zake na Kanye West ziwaathiri watoto na namna wanavyomchukulia Baba yao. “Ninaweza kuwa napitia magumu mengi, lakini kama nipo kwenye gari ninawapeleka shule na wanataka kusikiliza nyimbo za Baba yao, haijalishi ni yapi tunapitia, inabidi nitabasamu na niweke nyimbo zake na nicheze kama hakuna kibaya kilichotokea. Nikiwashusha tu nakurudi nyumbani, naangua kilio.” alieleza Kim Kardashian
Read More