Kanye West Apigwa Marufuku na Kim Kuwakaribia Watoto Wao

Kanye West Apigwa Marufuku na Kim Kuwakaribia Watoto Wao

Mwanamitindo maarufu Kim Kardashian ametoa onyo kali kwa aliyekuwa mume wake, msanii Kanye West, akimtaka akae mbali na watoto wao, licha ya kuwa wanashirikiana kwenye ulezi wa pamoja (joint custody). Taarifa hiyo imesababisha gumzo kubwa mitandaoni huku mashabiki wakigawanyika kuhusu hatua hiyo ya Kim. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na familia hiyo, Kim ameweka wazi kwamba hataki Kanye awe karibu na watoto wao bila ruhusa maalum, akidai kuwa vitendo na tabia za hivi karibuni za rapa huyo ni zisizotabirika na huenda zikahatarisha utulivu wa watoto. Hali hiyo inazua maswali kuhusu mustakabali wa mpango wao wa ulezi wa pamoja, hasa ikizingatiwa kuwa Kim na Kanye walikubaliana kushirikiana kulea watoto wao wanne baada ya talaka yao mwaka wa 2022. Mashabiki mitandaoni wametoa maoni mseto, wengine wakimuunga mkono Kim kwa kutanguliza maslahi ya watoto, huku wengine wakimtetea Kanye na kusema anapaswa kuruhusiwa kuwa sehemu ya maisha ya watoto wake. Mpaka sasa, Kanye hajatoa kauli rasmi kuhusu tishio hilo, lakini wengi wanatarajia majibu yake, hasa kutokana na historia yake ya kujibu hadharani kupitia mitandao ya kijamii.

Read More
 Kim Kardashian anunua mkufu wa msalaba uliowahi kumilikiwa na Princess Diana

Kim Kardashian anunua mkufu wa msalaba uliowahi kumilikiwa na Princess Diana

Baby Mama wa Rapa Kanye West, Kim Kardashian ameongeza mkufu wa mamilioni ya fedha kwenye orodha ya vito vyake vya thamani na vya kukumbukwa. Tovuti ya TMZ imeripoti kwamba, Mwanamama huyo amenunua mkufu huo wenye umbo la msalaba ambao ulikuwa mali ya Princess Diana miaka ya 1980. Mwakilishi wa Kampuni iliyopiga mnada mkufu huo amesema, Kim ameununua kwa zaidi ya KSh. milioni 24

Read More
 Kim Kardashian afunguka kuhusu imani yake kwa Mungu

Kim Kardashian afunguka kuhusu imani yake kwa Mungu

Mwanamitindo maarufu nchini Marekani Kim Kardashian amefunguka kuhusu imani yake kwa Mungu na jinsi anavyoshiriki jambo hilo na watoto wake. Katika kipindi maalumu cha Angie Martinez IRL Podcast, Kardashian aliulizwa ikiwa huwa na kawaida ya kufanya maombi(anasali), alisema; “Mimi ninasali kila usiku na watoto wangu. Hata kama niko nje ya mji, lazima wanipigie simu, na tunasali pamoja kupitia FaceTime,” aliendelea. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 42 alisema mara nyingi anasali na kuomba kwa ajili ya Afya na furaha ya familia yake na alipoulizwa kuhusu maisha yake ya kimahusiano, alisema anaamini katika Mungu, upendo, imani katika yote, na anaamini Mungu atamletea mtu sahihi kwenye maisha yake. Mnamo 2021, Kardashian aliomba talaka kutoka kwa rapa Kanye West, kufuatia miaka sita ya ndoa yao hii ikiwa ni ndoa yake ya tatu.

Read More
 Kim Kardashian akiri kupata ugumu kulea watoto na Kanye West

Kim Kardashian akiri kupata ugumu kulea watoto na Kanye West

Rapa Kanye West anampa wakati mgumu sana Baby Mama wake Kim Kardashian hasa kwenye malezi ya watoto wao baada ya kuachana. Kwenye mahojiano na Podcast ya Mtangazaji Angie Martinez, Kim amesema kushiriki kwenye suala la malezi na YE ni jambo gumu sana. “It’s hard. Co-parenting, it’s really fu**ing hard.”, Alisema kwa masikitiko. Aidha Kim Kardashian amedai kuwa hataki tofauti zake na Kanye West ziwaathiri watoto na namna wanavyomchukulia Baba yao. “Ninaweza kuwa napitia magumu mengi, lakini kama nipo kwenye gari ninawapeleka shule na wanataka kusikiliza nyimbo za Baba yao, haijalishi ni yapi tunapitia, inabidi nitabasamu na niweke nyimbo zake na nicheze kama hakuna kibaya kilichotokea. Nikiwashusha tu nakurudi nyumbani, naangua kilio.” alieleza Kim Kardashian

Read More
 Kanye West ampatia Kim Kardashian nyumba baada ya mchakato wa talaka kukamilika

Kanye West ampatia Kim Kardashian nyumba baada ya mchakato wa talaka kukamilika

Rapa Kanye West amelazimika kumpatia Kim Kardashian nyumba ambayo aliinunua mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya makubaliano yao ya Talaka ambayo yamefikia mwisho. Rapa huyo kutoka Marekani atahamisha umiliki wa nyumba hiyo kutoka kwenye jina lake kwenda kwa Kim. YE alinunua Jumba hilo Desemba 2021 kwa ($4.5 million) zaidi ya KSh. Milioni 551 likiwa pembeni ya makazi ya Kim Kardashian eneo la Hidden Hills ambapo alifanya hivyo kwa lengo la kuwa karibu na familia yake baada ya kuachana na mkewe.

Read More
 Kanye West na Kim Kardashian wafikia muafaka wa Talaka yao

Kanye West na Kim Kardashian wafikia muafaka wa Talaka yao

Rapa Kanye West na Kim Kardashian hatimaye wamefikia maridhiano ya Talaka na sasa YE atatakiwa kumlipa Kim Kardashian kiasi cha ($200k) zaidi ya Sh. Milioni 22 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya watoto yaani Child support. Kubwa zaidi lililofikiwa muafaka ni haki sawa katika malezi ya watoto (equal access) ambapo awali ilikuwa ngumu kwa YE kupata nafasi ya hata kuwaona watoto wake. Japo imeelezwa kwamba watoto watatumia muda wao mwingi kwa Mama yao, jambo ambalo hata YE aliwahi kulipitisha. Itakumbukwa, Mwanamama Kim Kardashian mwezi Februari, mwaka jana alifungua shauri mahakamani la kudai Talaka baada ya kuwa kwenye ndoa kwa takribani miaka 7 na Kanye West.

Read More
 Kim Kardashian akasirishwa na kauli za Kanye West

Kim Kardashian akasirishwa na kauli za Kanye West

Mwanamitindo na aliyekuwa mke wa rapa Kanye West, Kim Kardashian ameonyesha kukasirishwa na kauli za aliyekuwa mume wake kuhusiana na tuhuma alizozitoa juu ya watu wenye asili ya kiyahudi. Kupitia ukurasa wake wa twitter Kim Krdashian ameandika “Hotuba ya chuki siyo sawa au yenye udhuru, Nasimama pamoja na jamii ya watu wa kiyahudi na naomba kauli hizo za kigomvi na zenye chuki kuelekea kwa wayahudi zifikie mwisho haraka” – Kim Kardshian Wiki iliyopita rapa Kanye West alitoa maneno ya chuki juu ya watu wenye asili ya kiyahudi huku akisema kuwa vyombo vya habari vya watu wa jamii ya kiyahudi vimekuwa vikitoa habari za kichonganishi zenye lengo la kuharibu jamii ya watu wa Marekani. Watu wa jamii ya kiyahudi wamekasirishwa na kauli hizo za rapa huyo, huku wengi wakitishia kufungua kesi dhidi ya Kanye West

Read More
 Kim Kardashian ahimarisha ulinzi wa watoto wake kutokana na vitisho vya Kanye West

Kim Kardashian ahimarisha ulinzi wa watoto wake kutokana na vitisho vya Kanye West

Mwanamama Kim Kardashian ameripotiwa kuongeza pesa zaidi kwenye ulinzi lakini pia kuimarisha usalama wa watoto wake kufuatia Kanye West kuanika hadharani Jina la shule ambayo watoto wanasoma. Kanye West alijikuta akifunguka hadharani na kutaja Jina la shule hiyo kwenye mfululizo wa post zake kwenye mitandao ya kijamii wakati akipambana kuwajibu wakosoaji wake kwenye sakata la “White Lives Matter” ambalo lilishika vichwa vya habari kwa kuwakera watu weusi duniani kote.

Read More
 KANYE WEST AMTANIA PET DAVIDSON KWA KUACHANA KIM KARDASHIAN

KANYE WEST AMTANIA PET DAVIDSON KWA KUACHANA KIM KARDASHIAN

Rapa kutoka Marekani Kanye West amerejea Instagram na kumtolea uvivu Pete Davidson ambaye hivi karibuni ametajwa kuachana na Kim Kardashian. YE ameibuka na mfano wa taarifa kwenye gazeti la The New York Times ikidai Pete “Skete” Davidson kama ambavyo humtania, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 28. Hii imekuja baada ya Mtangazaji huyo na Mchekeshaji kuripotiwa kubwagana na Kim Kardashian baada ya penzi lao kudumu kwa miezi 9. YE aliingia kwenye mvutano wa mitandaoni na Pete baada ya kuingia penzini na Kim baada tu ya ndoa yao kuingia doa jeusi.

Read More
 KIM KARDASHIAN ATISHIWA KULIPULIWA NA BOMU

KIM KARDASHIAN ATISHIWA KULIPULIWA NA BOMU

Baby Mama wa Rapa Kanye West, Kim Kardashian ameripotiwa kupokea vitisho vya bomu na kifo kutoka kwa mtu asiyejulikana. Kwa mujibu wa TMZ, Kim anadai kuwa maisha yake pamoja na watoto wake yapo hatarini, hii ni baada ya kupokea barua kadhaa zinazotishia kuondoa uhai wake, ambapo mwandishi wa barua hizo ametishia kulipua ofisi ya Kim kwa bomu. Kim amedai kupata barua kutoka kwa jamaa anayefahamika kama David Resindez, ambaye ana anuani zake za nyumbani na biashara, na tayari ameshatuma barua zaidi ya 80 za kumtishia yeye pamoja na watoto wake wa nne. Hata hivyo, mwanasheria wa Kim, Shawn Holley anatajwa tayari kufanya utaratibu wa kupata zuio la mahakama juu ya mtu huyo kutoendelea kutoa vitisho hivyo.

Read More
 KANYE WEST AMFANANISHA KIM KARDASHIAN NA KATUNI  MARGE SIMPSON

KANYE WEST AMFANANISHA KIM KARDASHIAN NA KATUNI MARGE SIMPSON

Mwanamama Kim Kardashian amefunguka kwamba baada ya kumalizika kwa Tuzo za Wall Street Journal’s Innovator Awards (WSJ), Kanye West alimuita pembeni na kumwambia kwamba amefanana na katuni “Marge Simpson” ambaye ni mhusika kwenye animation maarufu nchini Marekani, The Simpsons. Kanye West hakuishia hapo, alienda mbali zaidi na kumwambia Kim kuwa amekwisha, jambo ambalo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wamehoji kuwa huenda Kanye ametoa maneno hayo kutokana na namna ambavyo baby mama wake kim amekuwa akivalia kwenye matukio mbali mbali Kauli ya Kim Kardashian imekuja siku chache baada ya kuweka wazi kuwa siku hizi amekuwa akipaniki hasa linapokuja suala la kupangilia mavazi tangu aachane na Kanye West. Kama unakumbuka, Kanye West ndio alikuwa stylist wa Kim Kardashian na mara ya mwisho kumvalisha ilikuwa ni kwenye kipindi cha Saturday Night Live (SNL)

Read More
 MAMA MZAZI WA KIM KARDASHIAN AKANUSHA KUVUJISHA MKANDA WA NGONO WA BINTI YAKE

MAMA MZAZI WA KIM KARDASHIAN AKANUSHA KUVUJISHA MKANDA WA NGONO WA BINTI YAKE

Mwanamama Kris Jenner amekanusha kuhusika kwenye biashara ya kusambaza mkanda wa ngono ambao ulimuhusisha binti yake Kim Kardashian na Ray J mwaka 2007. Kris Jenner amekanusha tuhuma hizo ambazo zilitolewa na Ray J wiki hii ambaye alidai kwamba video ile ya ngono haikuvuja bali ilikuwa ni makubaliano ya Kibiashara baina yake, Kim Kardashian pamoja na Kris Jenner. Utakumbuka kuwa Oktoba mwaka 2002 Kim Kardashian na Ray J walirekodi mkanda wa Ngono wakiwa mapumzikoni nchini Mexico. Mwaka 2007 kampuni ya Vivid Entertainment iliripotiwa kununua haki za mkanda huo kwa $1 million  na ndio ulikuwa mwanzo wa Kim Kardashian kupata umaarufu duniani kote.

Read More