KIM KARDASHIAN MBIONI KUFUNGA NDOA NYINGINE

KIM KARDASHIAN MBIONI KUFUNGA NDOA NYINGINE

Licha ya kutalikiana na Kanye West, Kim Kardashian bado anaamini kwenye kuolewa. Ameweka wazi kuwa atafunga ndoa nyingine ambayo itakuwa ya Nne kwenye maisha yake. Kwenye episode ya Keeping Up with The Kardashians, Kim alisema “Naamini kwenye mapenzi, ndio maana natumai kutakuwa na ndoa nyingine kwangu. Kwa mara ya Nne. Kim Kardashian alifunga ndoa ya kwanza na Damon Thomas mwaka 2000 na ilivunjika mwaka 2004, ya pili alifunga Kris Humpries mwaka 2011 na ilivunjika 2013. Ndoa yake ya tatu ilikuwa na Kanye West 2014 hadi 2022.

Read More
 KIM KARDASHIAN NA HOFU JUU YA ‘SEX TAPE’ YAKE NYINGINE KUVUJA

KIM KARDASHIAN NA HOFU JUU YA ‘SEX TAPE’ YAKE NYINGINE KUVUJA

Staa wa vipindi vya Tv na mwanamitindo Kim Kardashian, ameripotiwa kuajiri wakili mwingine ili kumzuia Ray J ambaye ni mpenzi wake wa zamani asivujishe mkanda wake mwingine wa ngono. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Kim Kardashian amewaita mawakili wafanye jitihada za kuzuia kanda nyingine ya ngono kuwekwa hadharani. Kim anahofia Ray J ambaye alishiriki naye kwenye video hizo kuzivujisha, amedai mpenzi wake huyo wa zamani anapanga kutengeneza mamilioni kwa kuachia video zingine hivi karibuni. Chanzo kimoja kilisema: “Kim anajua kuwa Ray J alitengeneza kanda hizo wakiwa pamoja, baadhi ya video zitakuwa ziko karibu sana kutoka. Ikumbukwe Kim Kardashian alirekodi video hizo akiwa na miaka 27, akiwa na Ray J.

Read More
 KANYE WEST NA KIM WAMEACHANA RASMI, MCHAKATO WA TALAKA WAKAMILIKA

KANYE WEST NA KIM WAMEACHANA RASMI, MCHAKATO WA TALAKA WAKAMILIKA

Ndoa ya Kim Kardashian na Kanye West imevunjika rasmi baada ya miaka 8. Mchakato wa talaka umekamilika Machi 3 na Jaji wa mahakama ya mjini Los Angeles ametangaza rasmi kwamba Kim Kardashian anaweza kuendelea na maisha yake ya U-single lakini pia ameondoa jina la ‘West’ kwenye majina yake matatu. Tovuti ya TMZ imebaini kwamba hakuna tumaini lolote kwa Kim na Kanye West  kurudiana kwani Kim amepigilia msumari kwenye maandishi kwamba jambo hilo haliwezekani kwa sasa. Kim Kardashian amesema alifanya kila awezalo kuyamaliza na Kanye West tangu afungue shauri la talaka mwezi Februari mwaka 2021 lakini Ye hakuonesha ushirikiano. Ikumbukwe Kim na rapa Kanye West wamedumu kwenye ndoa kwa takriban miaka 7 na amejaliwa watoto wanne ambao ni Psalm, Saint, Chicago na North.

Read More
 RAPA KANYE WEST AMRUDIA MUNGU KUINUSURU FAMILIA YAKE AMBAYO IMESAMBARATIKA

RAPA KANYE WEST AMRUDIA MUNGU KUINUSURU FAMILIA YAKE AMBAYO IMESAMBARATIKA

Rapa Kanye West ni kama bado anatamani kurudiana na baby mama wake Kim Kardashian kwa sababu anazidi kuja na matukio mbalimbali kila kukicha. Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram rapa huyo ameshare picha ya watoto wake wakiwa pamoja na mama yao, Kim Kardashian na kuandika kuwa mungu asaidie familia yake irudi kuwa pamoja. Baada ya Kanye West kuonesha kuwa bado anatamani familia yake irudi kama zamani, mpenzi wa sasa wa Kanye West, Julia Fox anasema hana wasiwasi kwa sababu anachojua kwa sasa Kanye West ni wa kwake na anajua kuwa bado ana mabaki ya hisia kwa mrembo Kim kardashian ila yeye anachukulia ni hali ya kibinadamu kumkumbuka ulietengana nae. Siku kadhaa zilizopita tuliona kupitia mitandao ya kijamii kanye west akimchana baby mama wake Kim kwa mambo mbalimbali ikiwemo kumuunganisha mtoto wao North West kwenye mtandao wa Tiktok bila idhini yake.  

Read More
 KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN WARUSHIANA MANENO MAKALI KWENYE MTANDAO WA INSTAGRAM

KANYE WEST NA KIM KARDASHIAN WARUSHIANA MANENO MAKALI KWENYE MTANDAO WA INSTAGRAM

Rapa kutoka Marekani Kanye West ameonesha kutokupendezwa na kitendo cha Mwanae wa kike North West aliyezaa na mrembo Kim Kardashian kujiunga katika mtandao wa TikTok. Kupitia instagram page yake Kanye West ameibuka na kuomba ushauri ni kitu gani afanye juu ya hili la mwanae kuungwa kwenye mtandao huo maarufu wa TikTok “Hii Ni Talaka Yangu Ya Kwanza, Nahitaji Kufahamu Ni Kipi Nifanye Kuhusu Mwanangu Kuunganishwa Katika Mtandao Wa Tiktok Kinyume Na Mapendekezo Yangu” Baada ya Kanye West kuhoji na kuomba ushauri nini afanye baada ya mwanae kuwepo kwenye mtandao maarufu wa TIKTOK sasa mama wa North ambaye ni Kim Kardashian ameamua kumjibu Kanye West juu ya hilo. Kupitia Insta story ya Kim Kardashian amemjibu kudai kuwa Kanye West anawaumiza watoto kwa kuleta tofauti zao kwenye mitandao ya kijamii. “Mashambulizi ya Kanye West juu yangu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni mabaya na yanaumiza zaidi kuliko mtoto kutumia mtandao wa TikTok. “Kama Mzazi na Muangalizi wa Mtoto wetu , nahakikisha nampa malezi bora huku nikimpa uhuru wa kuonyesha Vipaji Vyake Mbalimbali alivyonavyo . Talaka ni kitu kibaya kwa watoto wetu , Lakini vitendo vya Kanye West Kutoka kutuendesha vinaongeza maumivu zaidi kwenye Maisha yetu ” Hata hivyo bado Rapa Kanye West amelishikilia swala la Mwanae North kuwepo kwenye mtandao wa TikTok ambapo ameweka Taratibu na Sheria za kujiunga na mtandao huo. YE ameweka maelezo ya kujiunga na mtandao huo ambapo moja ya sheria ni mtoto mwenye umri wa miaka 13 na kushuka chini inabidi ajisajili kwa umri wake ili apate kuona maudhui yanayomfaa tu.

Read More
 KIM KARDASHIAN AKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA KANYE WEST KUHUSU UWEPO WA SEXTAPE YAKE NA RAY J

KIM KARDASHIAN AKANUSHA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA KANYE WEST KUHUSU UWEPO WA SEXTAPE YAKE NA RAY J

Kanye West ameiambia Hollywood Unlocked kwamba alifanikiwa kuupata mkanda wa ngono kutoka kwa Ray J, ikiwa ni sehemu ya pili ya ule ambao ulivuja mwaka 2007 ukimuonesha Ray J na Kim Kardashian wakifanya mapenzi. Kwenye mahojiano ambayo ameyafanya na Hollywood Unlocked, YE amesema Kim alitokwa na machozi baada ya kufikishiwa mkanda huo. “Nilikwenda na kuchukua laptop mwenyewe kwa Ray J, na nilimpatia Kim Kardashian kwenye saa mbili asubuhi. Alilia sana baada ya kuona Laptop, unajua kwanini? Ni kwa sababu iliwakilisha namna gani watu walikuwa wanamtumia na kumchukulia kama bidhaa” alisema YE kwenye mahojiano hayo. Wack 100 aliyekuwa meneja wa Ray J ndiye alitusanua uwepo wa sehemu ya pili ya mkanda huo wa ngono. Masaa machache baada ya kutoka taarifa hiyo, upande wa Kim Kardashian umeibuka na kukanusha taarifa hiyo ikisema hakukuwa na maudhui yoyote ya ngono na hakuna sehemu ya pili ya mkanda huo. Aidha kwenye laptop hiyo kulikutwa video za Kim na Ray J wakiwa kwenye ndege wakielekea nchini Mexico na zingine wakiwa kwenye kumbi za starehe na migawaha.

Read More
 KANYE WEST AWEKEWA VIKWAZO KUINGIA KWENYE BIRTHDAY  PARTY YA BINTI YAKE, CHICAGO WEST

KANYE WEST AWEKEWA VIKWAZO KUINGIA KWENYE BIRTHDAY PARTY YA BINTI YAKE, CHICAGO WEST

Kanye West ameamua kuanika wazi kila kitu ambacho kinaendelea baina yake na Kim Kardashian, usiku wa kuamkia leo ameeleza namna ambavyo aliwekewa vikwazo kuingia kwenye birthday party ya binti yake, Chicago West. YE anadai kwamba hakupewa kabisa location ya wapi party hiyo itafanyika,ila juhudi za Travis Scott zilisaidia kwani alimtumia location na alifika eneo hilo ambapo kulikuwa na party pia ya Stormi Webster. Stori kubwa ni kwamba baada ya kufika, walinzi wa Kim Kardashian walimzuia YE kuingia ndani ya party hiyo kitendo ambacho kilimkasirisha sana. Shukrani kwa Kylie Jenner kwani alimpambania hadi akafanikiwa kuingia na kufurahi pamoja na binti yake. Kwenye video ambayo anaonekana akizungumzia sakata hilo, YE anasema Kim anatengeneza mazingira watoto wake wamuone kama baba asiyejali. Hata hivyo sakata la Kanye kuzuiwa kuwa karibu na watoto wake halijaanza jana, kwenye mahojiano na Hollywood Unlocked, Kanye West alisema Jumatatu iliyopita aliwafata watoto wake shule ili kuwapeleka nyumbani, alipofika shuleni walinzi wa Kim Kardashian walimzuia getini. Hakubishana nao, siku nyingine alifanikiwa na kuwafikisha hadi nyumbani na North alimtaka aingie ndani lakini walinzi walimzuia, inadaiwa kuwa Pete Davidson ambaye ni mpenzi mpya wa Kim, alikuwepo ndani.

Read More