King Kaka Afurahia Uwepo Wake Katika Tuzo za BET 2025, Afichua Kuwa Maisha Yake Yamebadilika

King Kaka Afurahia Uwepo Wake Katika Tuzo za BET 2025, Afichua Kuwa Maisha Yake Yamebadilika

Msanii maarufu wa Kenya, King Kaka, ameonyesha furaha isiyo kifani baada ya kuhudhuria hafla ya tuzo za BET Awards 2025 iliyoandaliwa katika ukumbi wa Peacock Theater jijini Los Angeles, California. Kupitia video aliyoipakia kwenye Instagram, ikimuonesha mwanamuziki wa kimataifa Lil Wayne akitumbuiza, King Kaka anaonekana kushangazwa na kuwa karibu sana na mastaa waliomtia motisha tangu akiwa mtoto, akisisitiza kuwa tukio hilo limemfungua macho na kumpa msukumo mpya katika safari yake ya muziki na maisha kwa ujumla. “Sijawahi kuhamasika hivi maishani mwangu wote!!! Naahidi maisha yangu yamebadilika kabisa.Kumbukumbu zote za utotoni ziko mstari wa nne kutoka hapa, hapa tu!!! Na bado tuna safari ndefu sana mbele yetu. Kwa njia, wewe unaona nani?,” King Kaka aliandika ujumbe uliogusa hisia za mashabiki wake. Mashabiki wake walimpongeza kwa hatua hiyo, wakimtia moyo kuendelea kuwakilisha Kenya na Afrika Mashariki kwenye majukwaa ya kimataifa. Tukio hilo limeonekana kama ushahidi wa jinsi sanaa ya Afrika inavyozidi kutambuliwa kimataifa.

Read More
 King Kaka Afichua Siri ya Kuweza Kusawazisha Majukumu ya Uongozi, Muziki na Upishi

King Kaka Afichua Siri ya Kuweza Kusawazisha Majukumu ya Uongozi, Muziki na Upishi

Msanii maarufu wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Kennedy Ombima almaarufu King Kaka, amewashangaza mashabiki wake kwa mara nyingine baada ya kufichua jinsi anavyoweza kusawazisha majukumu yake mengi, akiwa Mkurugenzi Mtendaji (CEO), Mkurugenzi wa miradi, msanii wa muziki na hivi karibuni, mpishi (chef). Katika mahojiano maalum, King Kaka alieleza kuwa utaratibu madhubuti, nidhamu ya hali ya juu, na moyo wa kujifunza ndiyo nguzo kuu zinazomsaidia kudhibiti maisha yake yenye shughuli nyingi. “Watu wengi hufikiri ni ngumu, lakini nikikupenda kitu, utakipa muda. Mimi hupanga siku yangu kwa makini, kuna muda wa familia, kazi, na burudani,” alisema. Mbali na kuendesha kampuni yake ya usimamizi wa wasanii na miradi ya kijamii, King Kaka bado anaendelea kutoa muziki wa kiwango cha juu na sasa ameanza safari mpya ya upishi, akionyesha ujuzi wake jikoni kupitia mitandao ya kijamii. Alisema kuwa mapishi ni moja ya njia zake za kujieleza na kupumzika. “Upishi ni sanaa kama muziki. Ukiwa jikoni, unatengeneza ladha na hisia, ni kama kuandika beti kali kwenye wimbo,” aliongeza kwa tabasamu. Katika hatua nyingine, amefichua kuwa kwa sasa yuko kwenye mazungumzo na mchekeshaji Crazy Kennar kwa ajili ya kushirikiana kwenye mradi wa filamu. Amedokeza kuwa ndani ya mwaka huu, mashabiki wanaweza kutarajia uzinduzi wa filamu pamoja na mfululizo wa tamthilia (series) zitakazogusa maisha halisi na kutoa burudani ya hali ya juu. Kwa King Kaka, mafanikio yanatokana na nidhamu, ratiba thabiti, na kutoruhusu presha ya nje kumzuia kufanya kile anachopenda. Anaendelea kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengi wanaotamani kuingia katika sekta mbalimbali na kufaulu bila kupoteza mwelekeo.

Read More
 King Saha aahirisha tamasha lake kutokana na matatizo ya kiafya

King Saha aahirisha tamasha lake kutokana na matatizo ya kiafya

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha ameripotiwa kuahirisha tamasha lake la muziki ambalo lilipaswa kufanyika siku ya wapendanao duniani, Februari 14 mwaka 2023. Duru za kuaminika zidai kuwa mratibu wa tamasha hilo, Promota Musa Kavuma maarufu KT Promotions, pamoja na King Saha walianda mkutano wa faragha ambapo kwa kauli moja waliridhia kuahirisha tamasha hilo hadi pale itakapotangazwa tena. “Haitatokea. Imeahirishwa,” msemaji wa KT Promotions, Eddie Ssendi alithibitisha. Mabadiliko ya Tamasha la King Saha yamehusishwa na hali ya kiafya ya msaniii huyo ambaye alishauriwa na madaktari apumzike kabla ya kuanza tena shughuli zake za muziki.

Read More
 King Kaka afunguka namna alivyopona kimiujiza baada ya kuugua

King Kaka afunguka namna alivyopona kimiujiza baada ya kuugua

Rapa King Kaka amebainisha kuwa yeye kuwa hai na kuweza kufanya mambo kadhaa ya kawaida kama vile kula na kutembea ni muujiza. Katika mahojiano na Oga Obinna kwenye Kula Cooler Show, mwanamuziki huyo alifichua kuwa alipiga hatua ya kuenda hospitali baada ya ugonjwa kumlemea zaidi hadi kiwango alihisi kama angekufa. “Siku moja mke wangu alitoka kazini nikamwambia naona kama nitatolewa hapo ndani ya mfuko wa kubebea mwili na sitaki watoto waone hilo. Nilimwambia tuchague hospitali yoyote ile nitalala huko.” alisimulia. Alisema baada ya kufika hospitali alilazwa na madaktari wakaanza kumfanyia vipimo kadhaa bila kupata ugonjwa wowote. Miongoni mwa magonjwa aliyopimwa ni TB, UKIMWI, Saratani miongoni mwa mengine. “Ilifika wakati nilikuwa naomba ugonjwa.” alisema. King Kaka alifichua kwamba mchakato wa uponyaji wake ulianza usiku mmoja wakati bado akiwa amelazwa katika hospitali ambapo alianza kuona mambo yasiyo ya kawaida mwendo wa saa tisa usiku. “Nilianza kuona vitu sijui. Nilianza kuona mwangaza, nikaona giza. Niliona ni wakati wangu wa kuishia. Niliambia Mungu kama wakati wangu niko tayari. Huwa inafika mahali hata unakubali kifo.” alisimulia. Alisema baada ya kufichuliwa mambo ya ajabu alimuomba Mungu na kufanya amani naye kwani alihisi anakaribia kufa. Kiajabu, asubuhi iliyofuata alipata kifungua kinywa kwa mara ya kwanza baada ya siku tano hivi. Pia alikunywa supu baadaye, na baada ya siku Tano aliruhusiwa kuondoka hospitali. Mwishoni mwa mwaka 2021, King Kaka aliugua sana baada ya kufanyiwa vipimo vya afya vibaya. Alipoteza zaidi ya kilo 30 katika kipindi cha miezi minne ambacho alikuwa akipambana na ugonjwa usiotambuliwa.

Read More
 King Kaka atoa wito kwa wakenya kushabikia wanamichezo wao bila kushinikizwa

King Kaka atoa wito kwa wakenya kushabikia wanamichezo wao bila kushinikizwa

Rapa King Kaka ametoa changamoto kwa wakenya kuanza kuwashabikia wanamichezo wao badala ya kushawishiwa kufanya hivyo na watu wa mataifa ya nje. Kupitia miitandao ya kijamii King Kaka amesema ameshangzwa na namna wakenya walijitokeza kumshangilia bondia wa Tanzania mandonga mtu kazi ilhali kuna wana michezo wengi wanaofanya vizuri kwenye nyanja mbali mbali. Hitmaker huyo wa “Wajinga Nyinyi” amewataka wakenya kuwa wazalendo kwani hawahitaji shinikizo za watu wa nje kuwafanya kufuatilia matukio mbali mbali ya michezo nchini. Hata hivyo wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na rapa huyo wakisema michezo nchini Kenya imekosa mvuto na mbwembwe kutokana wawekezaji duni.

Read More
 Ringtone awakosoa mapromota wa muziki wa Injili kwa kumlipa King Kaka shillingi laki mbili kwa show

Ringtone awakosoa mapromota wa muziki wa Injili kwa kumlipa King Kaka shillingi laki mbili kwa show

Mwanamuziki Ringtone Apoko ameamua kutoa ya moyoni, amewachana wadau wa muziki wa injili nchini DJ Moz na Njugush kwa kitendo cha kutowazingitia wasanii wa Gospel kwenye hafla ya mkesha wa mwaka mpya. Kupitia video aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram Ringtone ameonesha kutofurahishwa na hatua ya wawili hao kumpa kipau mbele rapa King Kaka kwenye hafla hiyo ambayo kwa mujibu wake ilipaswa kuongozwa na wasanii wa nyimbo za injili. Hitmaker huyo wa “Omba” amesema kitendo cha msanii huyo wa kidunia kulipwa shilling laki mbili kutumbuiza kwenye shoo hiyo ambayo imefadhiliwa na hisani ni njia ya kuivunjia heshima tasnia ya muziki wa injili ikizingatiwa kuwa wasanii wengi wa gospel siku huyo hawakuwa na shughuli ya kufanya. “Maze nimejam,nimejam , nimejam sana,nimejam can you imagine ati King Kaka aliperform kwa event ya gospel akalipwa 200 thousand shillings na wasanii wa gospel siku hiyo walilala nyumbani hawana pahali pa kwenda kuimba!.,” Alisema kwenye video hiyo.

Read More
 Rapa King Kaka aachia rasmi Album yake mpya

Rapa King Kaka aachia rasmi Album yake mpya

Rapa King Kaka ameachia Album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. Album aliyoipa jina la “2nd Life” ina jumla ya mikwaju 17 ya moto huku akiwa amewashirikisha wakali kama Wanavokali, Femi One, Iyaniii, Kanambo Dede,Solomon Mkubwa, Goodluck Gozbert na wengine wengi. 2nd Life ambayo ni Album ya sita kwa King Kaka, na tayari inapatikana kwenye mitandao yote ya ku-stream muziki duniani. Ikumbukwe King Kaka ameachia Album kwa ajili ya kumrudishia Mwenyezi Mungu fadhila kwa kumpa nafasi nyingine ya kuishi duniani ikizingatiwa kuwa mwaka 2021 nusra ampoteze maisha yake baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana uliofanya kupoteza uzani wa kilo 33.

Read More
 Rapa King Kaka ahirisha kuachia ya Album yake mpya

Rapa King Kaka ahirisha kuachia ya Album yake mpya

Rapa kutoka nchini Kenya King Kaka ametangaza kutoachia Album yake mpya kama alivyoahidi hapo awali kuwa itatoka Desemba 25. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bosi huyo wa Kaka Empire, amesema kutokana na ukubwa wa Album hiyo Uongozi wake umependelea itoke mwaka 2023 kwa sababu kuna wimbo wa msanii kutoka Jamaica ambao unapaswa kujumuisha kwenye album yake mpya. Rapa huyo amewaomba radhi mashabiki zake kwa kuchelewesha mchakato wa kuachia Album yake aliyoipa jina la “2nd Life” huku akiwashukuru kwa upendo ambao wamekuwa wakimuonyesha kwa miaka mingi. Album hiyo ambayo ni ya tano katika safari yake ya muziki ina jumla ya mikwaju 17 ya moto kutoka kwa wakali kama Wanavokali, Femi One, Iyaniii, Kanambo Dede,Solomon Mkubwa, Goodluck Gozbert na wengine wengi. 2nd Life ni Album ambayo King Kaka ameamua kuachia kwa ajili ya kumrudishia Mwenyezi Mungu fadhila kwa kumpa nafasi nyingine ya kuishi duniani ikizingatiwa kuwa mwaka 2021 nusra ampoteze maisha yake baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana uliofanya kupoteza uzani wa kilo 33.

Read More
 Rapa King Kaka atangaza kuachia Album yake mpya Disemba 2022

Rapa King Kaka atangaza kuachia Album yake mpya Disemba 2022

Rapa kutoka nchini Kenya King Kaka ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo ameipa jina la 2nd life kabla mwaka huu 2022 haujaisha. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bosi huyo wa Kaka Empire amesema ameamua kuja na album hiyo kwa ajili ya kumrudishia Mwenyezi Mungu fadhila kwa kumpa nafasi nyingine ya kuishi duniani ikizingatiwa kuwa mwaka 2021 nusra ampoteze maisha yake baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana uliofanya kupoteza uzani wa kilo 33. Hitmaker huyo wa Diana amesema album ambayo ni ya tano katika safari yake ya muziki itaingia sokoni Disemba 24 mwaka huu ikiwa na jumla ya mikwaju 17 ya moto. “One promise I made was to give gratitude, something we often take for granted. Inspired by what I’ve been through I am officially announcing my next body of work , my 5th album Titled #2ndLife that drops this 24th December.” Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa tayari amekamilisha video za nyimbo ambazo zinapatikana kwenye album yake ya 2nd Life, na ataachia rasmi video ya kwanza Novemba 20 mwaka huu huku akiwashukuru mashabiki kwa upendo ambao wamekuwa wakimuonyesha kwa miaka mingi. “I am excited , genuinely excited. 17 Music Videos!! Weuh 17! The journey begins. We release the 1st one this 20th. Asanteni for loving me over the many years.”,

Read More
 KING KAKA ASAINI DILI LA USHIRIKIANO NA JUKWAA LA MTANDAONI LA AFYA REKOD

KING KAKA ASAINI DILI LA USHIRIKIANO NA JUKWAA LA MTANDAONI LA AFYA REKOD

Hakika huu ni mwaka wa Neema kwa rapa kutoka Kenya King Kaka, hii ni baada ya kutangaza kuingia ubia wa kufanya kazi na jukwaa la kuto huduma za kimatibabu kwa njia ya kidijitali, Afya Rekod. Kupitia mitandao yake ya kijamii King Kaka amesema kuwa ushirikiano huo utasaidia kuendeleza ukuaji wa matibabu wa kidijitali nchini na hata kuwapunguzia wagojwa mzigo wa kusafiri kutafuta matibabu. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Fight” amesema  ushirikiano huo pia unalenga kuhamasisha umma kuhusu matibabu kupitia mfumo wa kidijitali huku akisema kuna haja kwa hospitali au vituo vya afya kukumbatia mfumo wa kidijitali hasa katika kufuatilia hali ya wagonjwa waliolazwa. Kampuni ya Afya Rekod inajishughulisha na masuala ya kuhifadhi maelezo ya kibinafsi ya mgonjwa, taarifa kamili kuhusu aina ya ugonjwa anayougua mhusika kwa njia ya mtandao. Huduma zinazotolewa kupitia programu hizo ni upendekezaji wa tiba na ushirikiano na mawasiliano ya karibu kati ya mgonjwa na daktari wake. King Kaka ni mmoja wa mastaa wa humu nchini ambao kati siku za hivi karibu wamepata ubalozi wa makampuni mbali mbali kutokana na ushawishi wao mkubwa kwenye jamii, wiki kadhaa zilizopata alilamba dili nono la kuwa balozi wa  kampuni ya simu ya mkononi ya Itel.

Read More
 KING KAKA AMJENGEA MAMA YAKE MZAZI MJENGO WA KIFAHARI

KING KAKA AMJENGEA MAMA YAKE MZAZI MJENGO WA KIFAHARI

Rapa wa Kenya King Kaka anazidi Kujipakulia Baraka Za Wazazi wake,hii ni baada ya kumjengea mamake mzazi mjengo wa kifahari. Kusindikiza taarifa hiyo, King Kaka amesimulia kisa kimoja ambacho kilimsukuma kutafuta hela ili kuja kumsaidia mama yake. “Siku moja nilifika nyumbani nikitoka shule, Askari wa Jiji alikuwa alikuwa ameweka kufuli kubwa sana mlangoni kwetu kwa sababu tulishindwa kulipa Kodi ya nyumba ya shilling 500. Nilimuahidi Mama yangu kwamba baadaye nitakuja kumnunulia nyumba. Sasa siku Nne zilizopita, tulifanya maombi tukiwa kwenye sebule ya nyumba hii ambayo nimemjengea.” ameandika King Kaka. Ni post ambayo imeshabikiwa na wafuasi wake kwenye mtandao wa instagram wakimpongeza kwa hatua ya kuwafanyia wazazi wake vitu vikubwa ambavyo vijana wengi wameshindwa kufanya.

Read More
 KING KAKA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI NCHINI MAREKANI

KING KAKA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI NCHINI MAREKANI

Rapa King Kaka ametangaza ujio wa ziara yake ya muziki  nchini marekani  kwa kuanika mkeka wa miji ambayo atafanya shows zake. Kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram king kaka, ameipa ziara hiyo jina la  Coast To Coast Summer 2022  USA  Tour ambapo amesema itafanyika ndani ya miji 13. Ziara hiyo ambayo anafanya kwa ushirikiano na Rarequest Music Group inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Marekani ikiwemo Boston, Chicago, Minnesota, Atlanta, Dallas, na Los Angeles. Hata hivyo hajaweka tarehe na mwezi ambayo ataanza tour yake hiyo ila king kaka amewataka mashabiki zake kufuatilia mitandao yake ya kijamii kwani yupo mbioni kuweka mambo sawa.

Read More