KING KAKA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI NCHINI MAREKANI

KING KAKA ATANGAZA UJIO WA ZIARA YAKE YA MUZIKI NCHINI MAREKANI

Rapa King Kaka ametangaza ujio wa ziara yake ya muziki  nchini marekani  kwa kuanika mkeka wa miji ambayo atafanya shows zake. Kupitia ukurasa wao rasmi wa Instagram king kaka, ameipa ziara hiyo jina la  Coast To Coast Summer 2022  USA  Tour ambapo amesema itafanyika ndani ya miji 13. Ziara hiyo ambayo anafanya kwa ushirikiano na Rarequest Music Group inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Marekani ikiwemo Boston, Chicago, Minnesota, Atlanta, Dallas, na Los Angeles. Hata hivyo hajaweka tarehe na mwezi ambayo ataanza tour yake hiyo ila king kaka amewataka mashabiki zake kufuatilia mitandao yake ya kijamii kwani yupo mbioni kuweka mambo sawa.

Read More
 KING KAKA ATANGAZA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

KING KAKA ATANGAZA KUKAMILIKA KWA ALBUM YAKE MPYA

Rapper kutoka Nchini Kenya King Kaka ametusanua kuwa album yake mpya imekamilika. Mkali huyo wa ngoma ya “Fight” ameweka wazi hilo kwenye podcast ya jalang’o tv huku akiwataka Mashabiki zake wakae Mkao Wa Kuipokea Album Yake Mpya Itakayoingia Sokoni Hivi Karibuni. Hata hivyo King Kaka hajatuambia idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album hiyo wala tarehe rasmi ya album yenyewe kuingia sokoni ila ni jambo la kusubiriwa Hii itakuwa ni album ya sita kwa mtu mzima wa King Kaka tangu aanze safari yake muziki ikizingatiwa kuwa tayari ana album tano, mixtape 9 na EP moja.

Read More
 KING KAKA ALAMBA SHAVU YA UBALOZI ITEL KENYA

KING KAKA ALAMBA SHAVU YA UBALOZI ITEL KENYA

Rapa King Kaka amelamba dili nono la kuwa balozi wa kampuni ya Simu ya Itel kwa upande wa Kenya. King Kaka ametangaza habari njema kwa wafuasi wake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kusema kwamba ana furaha kubwa kujiunga na familia ya Itel inayojishughulisha na  uzalishaji na usambazaji wa simu na vifaa vingine vya kielectroniki “Mabibi na Mabwana, leo ni siku KUBWA SANA. Sasa unamtazama BALOZI MPYA wa @itelkenya @itelhome_kenya. Utukufu wote kwa Mungu. Ushindi kwa vijana wa Ghetto ambao wana imani, Ushindi kwa wabunifu, Ushindi kwa watumiaji wa Itel na Ushindi kwa Kenya!!! #KakaEmpireIsTheLifestyle.” King Kaka ameandika Kwa upande wao Itel Kenya wameeleza kuwa wamefurahi kumkaribisha King Kaka kuwa balozi wa kampuni hiyo kwa kuwa wana Imani rapa huyo atatumia ushawishi wake kwenye jamii kuwafikishia wateja wao bidhaa zao za simu. “Tunayofuraha kutangaza ushirikiano na King Kaka. Anaakisi maadili ya matumizi mengi, ukamilifu na uvumbuzi ambayo tunafuata kwa uthabiti katika itel. Karibu kwa familia ya itel” Kampuni ya itel imeandika Instagram King Kaka sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za itel kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuiongezea kampuni hiyo mauzo.

Read More
 KING KAKA ATANGAZA KUIHAMA MAN UNITED NA KWENDA ARSENAL

KING KAKA ATANGAZA KUIHAMA MAN UNITED NA KWENDA ARSENAL

Rapa kutoka nchini Kenya, King Kaka ametangaza rasmi kuwa kuanzia sasa atakuwa anashabikia timu ya Arsenal baada ya kuachana na Manchester United. King Kaka ambaye kwa miaka mingi amekuwa akishabikia Manchester United ameeleza kutoridhishwa kwake na matokeo ya timu hiyo kwa michezo ya hivi karibuni. “Nadhani ni wakati sahihi nianze kutafuta raha kwingineko, ni rasmi kwamba sasa nashabikia Arsenal,” amesema King Kaka. Utakumbuka hatua hii ya King Kaka inakuja muda mfupi baada ya Manchester United kulazwa magoli manne kwa moja na majirani wao Manchester City, huku Arsenal wakipata ushindi wa magoli matatu kwa mawili ugenini dhidi ya Watford.

Read More
 KHALIGRAPH JONES NA KING KAKA WAOMBOLEZA KIFO CHA RAPA RIKY RICK KUTOKA AFRIKA KUSINI

KHALIGRAPH JONES NA KING KAKA WAOMBOLEZA KIFO CHA RAPA RIKY RICK KUTOKA AFRIKA KUSINI

Rapa Khaligraph Jones ameungana na wapenzi wa muziki wa hiphop Barani Afrika kumuomboleza kifo cha rapa riky Rick ambaye alifariki februari 23 mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa instagram Papa Jones ameshare screen shot ya mazungumzo ya siri kati yake na rapa huyo ambapo amesema kuwa mwaka wa 2018 alikuwa na matamanio ya kufanya kazi ya pamoja na riky rick lakini hakufanikisha suala hilo kutokana na ugumu wa kumfikia. Kwa upande wake Rapa King Kaka amesema walikutana na Riky Rick miaka kadhaa iliyopita nchini ufaransa kwenye moja ya party ambapo alipata wasaa mzuri kubadilishana mawazo na rapa huyo ambaye kwa mujibu wake alikuwa mtu mkarimu zaidi kuwahi kukutana naye. Riky Rick alifariki dunia februari 23 mwaka huu baada ya kujitoa uhai nyumbani kwake kaskazini mwa Joburg Jumatano asubuhi. Chanzo cha Kifo chake hakijatajwa lakini baadhi ya vyombo vya habari nchini Afrika Kusini vinaripoti kwamba Riky Rick alijinyonga baada ya kusumbuliwa na msongo wa mawazo. Rapa huyo alianza kujipatia umaarufu mwaka 2015 kupitia ngoma yake iitwayo, Boss Zonke.

Read More
 RAPA KING KAKA ALAMBA SHAVU YA KUWA BALOZI WA KIMATAIFA WA SPORTS BET

RAPA KING KAKA ALAMBA SHAVU YA KUWA BALOZI WA KIMATAIFA WA SPORTS BET

Kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sportsbet.io imemtangaza Rapa King Kaka kuwa balozi wake mpya wa kimataifa. Katika taarifa Sportsbet.io imesema wamemchagua King Kaka kwa sababu rapa huyo anaendana na vigezo vya kampuni hiyo kwani ana uwezo mkubwa wa kuwafikishia vijana wengi ujumbe wa kuwekeza na sportsbet.io Akitangaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia mitandao yake ya kijamii King Kaka amesema ameweka historia ya kuwa mwaafrika wa kwanza kuwa balozi wa kimataifa wa Sportsbet.io huku akisema kwamba kampuni hiyo italeta mwamko mpya kwenye soko la michezo ya kubashiri Barani Afrika. King Kaka ambaye ni moja kati ya marapa wakali Afrika anatarajiwa kutumia ubunifu na umaarufu wake kuwashawishi wafuasi wake kushiriki kwenye mchezo wa kubashiri kupitia mtandai wa sportsbet.io kama njia ya kujikwamua kiuchumi. Utakumbuka Sportsbet.io ni kampuni ya michezo ya kubashiri kwa kutumia sarafu ya mtandaoni ya Crypto.

Read More