KING MICHAEL KUANDAA UCHAGUZI MWINGINE WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA

KING MICHAEL KUANDAA UCHAGUZI MWINGINE WA CHAMA CHA WANAMUZIKI UGANDA

Mwanamuziki kutoka Uganda King Micheal ameapa kufadhili mchakato wa kuandaa uchaguzi  mwingine wa Chama cha Wanamuziki Uganda (UMA) baada ya uchaguzi wa chama hicho kuahirishwa ghafla juma lilopita. King Michael ambaye anawakilishi wasanii wa dancehall katika chama  cha UMA amesema kuwa watu walioandaa zoezi la upigaji kura kwa njia ya mtandao katika chama hicho walifeli kwenye majukumu yao. “Sidhani kama uchaguzi wa mtandaoni utafanya kazi hapa Uganda. Nitaandaa uchaguzi  mwingine kwa kuwa mimi pia ni kiongozi katika UMA,” alidai. Msanii huyo amesema uchaguzi ambao atauandaa utafanyika kwa mfumo wa kawaida ambao utatoa nafasi kwa watu kupanga foleni kwenye vituo vya kupigia kura huku akiwasihi wanaounga mkono wazo lake kumtafuta ili waweze kuweka mikakati zaidi. “Chaguzi zangu zitakuwa za watu kupanga foleni kwenye vituo vya kupigia kura. Ninawaalika wanaounga mkono wazo hilo kunifikia,” alimalizia. Utakumbuka uchaguzi wa UMA ulifutwa siku ya jumatatu wiki iliyopita baada ya king  Saha na wafuasi wake kudai mfumo wa upigaji kura ulidukuliwa na mchakato mzima wa uchaguzi ulikumbwa na dosari.

Read More
 KING MICHAEL AMCHANA BEBE COOL KWA KUMUUNGA MKONO CINDY SANYU

KING MICHAEL AMCHANA BEBE COOL KWA KUMUUNGA MKONO CINDY SANYU

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Michael amedai kuwa Bebe Cool anataka kumtumia Cindy kwa manufaa yake binafsi. Katika mahojiano yake King Michael amesema inashangaza kumuona Bebe Cool anamuunga mkono Cindy Sanyu kwenye azma yake ya kuwania urais wa chama cha wanamuziki nchini uganda UMA ikizingatiwa kipindi cha nyuma alikuwa anampinga akiwa anaendeleza harakati zake za kuwatetea wasanii kupitia chama cha UMA. Utakumbuka Bebe Cool alitangaza hadharani kumuunga mkono Cindy Sanyu kuwania urais chama cha wanamuziki nchini Uganda UMA baada ya Maurice Kirya kushindwa kwenye mchujo wa kuwachagua wagombea wa urais.

Read More