Msanii wa Jamaica Konshens Aomboleza Kifo cha Raila Odinga, Awapa Pole Wakenya
Staa wa muziki kutoka Jamaica, Konshens, ameungana na mashabiki zake kuomboleza kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Amollo Odinga. Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Konshens ametuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Kenya, akiwatia moyo katika kipindi hiki kigumu na kuwaomba wabaki imara licha ya huzuni iliyoikumba nchi hiyo ambayo imekuwa na nafasi maalum moyoni mwake kutokana na uhusiano wa karibu alioujenga kupitia muziki wake. Msanii huyo wa Dancehall, amesema anaungana na Wakenya katika majonzi, akiwapa pole kwa kumpoteza kiongozi ambaye amekuwa sauti ya haki na umoja kwa miaka mingi. Ujumbe wa Konshens unakuja siku moja tu baada ya nyota mwenzake kutoka Jamaica, Vybz Kartel, pia kutuma salamu za pole kwa Wakenya kufuatia kifo hicho. Hatua hiyo imeonyesha jinsi Raila Odinga alivyoenziwa si tu barani Afrika bali pia kimataifa, na namna muziki unavyoendelea kuwa daraja la kuunganisha watu katika nyakati za huzuni.
Read More