Msanii Levixone Amefunguka Sababu za Kukatiza Honeymoon na Desire Luzinda

Msanii Levixone Amefunguka Sababu za Kukatiza Honeymoon na Desire Luzinda

Msanii wa injili maarufu, Levixone, amefunguka sababu za yeye na mkewe mpya Desire Luzinda kukatiza honeymoon yao mapema, jambo lililowashangaza mashabiki waliotarajia waende kwenye mapumziko ya kifahari baada ya harusi. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, ameeleza kuwa sababu kuu ni ratiba ngumu ya kazi. Levixone alisema mara tu baada ya ndoa alikuwa na mialiko mingi ya huduma na shoo nchini kote, na hakuweza kuipuuza kwa ajili ya honeymoon ndefu. Hali hiyo ilisababisha safari yao ya mapumziko kufutika mapema kuliko walivyopanga. Kwa upande wa Desire Luzinda, naye alilazimika kurejea Marekani mara moja kuendelea na kazi zake, jambo lililoathiri zaidi mipango ya honeymoon yao. Hata hivyo, Levixone amesema changamoto hiyo haijawavunja moyo, kwani kwa sasa wanatazamia hatua kubwa zaidi, kuanzisha familia. Ameweka wazi kuwa anawaomba Mungu baraka za kupata watoto, akisisitiza kuwa idadi ya watoto si jambo analoweza kupanga, bali ni mapenzi ya Mungu. Kwa ujumla, ratiba ngumu za kikazi za wawili hao ndizo zilizokatiza honeymoon yao, lakini wameonyesha dhamira ya kuendelea na maisha ya kifamilia kwa matumaini na baraka za Mungu.

Read More
 Wasanii wa injili Uganda waeleza kwanini tamasha la Levixone halikuvutia umati mkubwa

Wasanii wa injili Uganda waeleza kwanini tamasha la Levixone halikuvutia umati mkubwa

Wanamuziki wa Injili kutoka nchini Uganda wamefunguka Kwanini Tamasha la msanii mwenzao Levixone halikupata mapokezi mazuri huko Kololo Airstrip wikiendi iliyopita. Kulingana na Justine Nabbosa, waimbaji wa nyimbo za injili hawapati upendo wa kutosha na uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya waumini wa kikristo. “Matamasha yetu hayavutii umati mkubwa  kwa sababu Wakristo hawatusaidii. Siku zote wanatuona tukitumbuiza kanisani bure, jambo ambalo linawazuia kuja kwenye matamasha yetu,” anasema Justine Nabbosa. Msanii wa Injili Betty Namaganda anasema, “Wakristo wanafikiri tunapaswa kubaki kanisani tukiimba bure lakini sisi pia tunahitaji pesa za kujikimu kimaisha. Napenda kuvishukuru vyombo vya habari vya kidunia kwa kutusaidia kutangaza show zetu”. Utakumbuka mwaka 2018, Levixone aliweka rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa nyimbo za injili kuuza tiketi zote (sold out) za show yake  aliyoiita “Turn The Reply”  katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval huko nchini Uganda kabla ya kuhamia Kololo Airstrip.

Read More
 SAKATA LA NDOA YA MSANII LEVIXONE NA DESIRE LUZINDA LACHUKUA SURA MPYA

SAKATA LA NDOA YA MSANII LEVIXONE NA DESIRE LUZINDA LACHUKUA SURA MPYA

Msanii aliyegeuki muziki wa Injili nchini Uganda Desire Luzinda inadaiwa kuwa hajafunga ndoa na mwimbaji mwenzake Levixone kwa nia njema kwani anamtumia kwa ajili ya kupata msaada wa kifedha kutoka kwa wafadhili. Chanzo cha karibu na mrembo huyo kinasema kipindi Desire anaanzisha wakfu wake Desire Luzinda Foundation alijaribu kuomba msaada kwa kanisa ambalo anashiriki nchini Marekani lakini alikataliwa kwa sababu hakuwa ameolewa. Uongozi wa kanisa hilo ulimshauri kuingia kwenye ndoa kwanza kama mkristo kamali ili aweze kupewa msaada wa kufadhili wakfu wake. Sasa rafiki yake wa zamani mwimbaji Levixone ndiye alikuwa kimbilio kwake na inatajwa hiyo ndio sababu ya mrembo huyo kuficha mahusiano yake ya kimapenzi. Hata hivyo wawili hao hawajatoa tamko lolote dhidi ya tuhuma hizo ila ni jambo la kusubiriwa. Utakumbuka video ya Levixone akiwa anatambulishwa kwa wazazi wa Desire Luzinda ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kitendo ambacho kiliwaacha walimwengu na maswali  juu ya wawili hao kuhalalisha mahusiano yao. Hii ilikuja mara baada ya uvumi wa wawili hao kutoka kimapenzi kuzungumziwa sana mtandaoni kwa kipindi cha miezi miwili.

Read More