Magix Enga Atambulisha Mpenzi Mpya Baada ya Kuachana na Baby Mama Wake
Prodyuza na msanii wa muziki nchini Kenya, Magix Enga, amezua gumzo mitandaoni baada ya kutambulisha mpenzi wake mpya wiki chache tu tangu atangaze kuachana na mama wa mtoto wake. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Magix ameshare picha akiwa pamoja na mchumba wake na kueleza kuwa ameingia rasmi kwenye ndoa. Haikuishia hapo, alienda mbali zaidi na kumtaja mwanamke huyo kuwa malkia wake wa moyo na chanzo cha furaha kubwa katika maisha yake. Hatua hiyo imewaacha mashabiki wengi wakiwa na maswali iwapo msanii huyo tayari amefunga ndoa au ni namna ya kuonesha hadharani ukubwa wa penzi lake kwa mwanamke huyo. Tukio hilo linajiri wiki chache baada ya Magix kuthibitisha kuachana na baby mama wake, ambapo alisema uamuzi huo ulifikiwa kwa makubaliano ya pande zote bila migogoro. Msanii huyo alibainisha kuwa licha ya kusitisha uhusiano wao wa kimapenzi, ataendelea kushirikiana kwa karibu na mama huyo katika malezi ya mtoto wao, akisisitiza kuwa ustawi wa mtoto unabaki kuwa kipaumbele chake kikuu.
Read More