Marioo aachia rasmi Tracklist ya Album yake mpya

Marioo aachia rasmi Tracklist ya Album yake mpya

Mkali wa Bongo Fleva Marioo ameachia Tracklist ya Album yake mpya The Kid You Know ambayo itatoka rasmi Disemba 9 mwaka huu. Album hiyo ya kwanza kwa Marioo, ina jumla ya mikwaju 17 huku ndani akiwashirikisha wakali kama Ali Kiba, Harmonize, Rayvanny, Jux, Ladipoe na wengine wengi. Ikumbukwe, hii inakuwa ni album ya kwanza kwa Marioo  katika safari yake ya muziki.

Read More
 Marioo kuachia historia fupi ya maisha yake kabla ya kutoa Album yake mpya mwezi Desemba 2022

Marioo kuachia historia fupi ya maisha yake kabla ya kutoa Album yake mpya mwezi Desemba 2022

Baada ya kuachia cover ya album yake mpya iitwayo “The Kid You Know” anayotarajia kuitoa Desemba 9, 2022, mwimbaji wa Bongofleva Marioo ametangaza kuwa ataachia historia fupi ya maisha yake kabla ya ujio wa album yake mpya. Marioo ameeleza hilo kupitia insta story yake. Pia amebainisha kwa sasa unaweza ukai Pre-Order “The Kid You Know” kupitia Africori. Album hiyo ya Marioo itakuwa na jumla ya nyimbo 18, huku nyimbo 3 toka kwenye album hiyo tayari zimeshatoka ambazo ni “Mi Amor”, “Naogopa” pamoja na “Dear EX”, nyimbo 15 zilizobaki zote ni mpya.

Read More
 Marioo atamba na album yake mpya, Asema ni moto wa kuotea mbali.

Marioo atamba na album yake mpya, Asema ni moto wa kuotea mbali.

Staa wa muziki wa Bongofleva, Marioo ni kama tayari ameikamilisha Album yake mpya ambayo huenda ikaingia sokoni hivi karibuni. Kupitia insta story kwenye mtandao wa Instagram Mkali huyo wa ngoma ya Dear Ex amesema ngoma zilizopo kwenye album yake hiyo ni za moto lakini pia kuna nyimbo ambazo zimebaki na anashindwa aziweke wapi. “Yaani kwenye albamu mangoma yamejaa halafu yote moto, halafu bado nipo na mawe mengine, hata sijui nayafanyia nini na bado nipo na mood ya kurekodi” amesema Marioo. Kwenye andiko lake hilo ameishia kwa kusema anafikiria kuwabariki mashabiki zake na zawadi ambayo walimwengu wametafsiri huenda msanii huyo ana mpango wa kuachia EP kabla ya Album. Utakumbuka juzi kati Marioo alitudokezea kuwa ngoma zake kama Mi Amor, Naogopa na Dear EX zitakuwepo kwenye albamu yake mpya.

Read More
 MAPANCH NA MARIOO WATUPIANA LAWAMA KUHUSU WIMBO WA “MY LOVE”

MAPANCH NA MARIOO WATUPIANA LAWAMA KUHUSU WIMBO WA “MY LOVE”

Agosti 10, msanii wa Bongfleva Mapanch aliachia video ya ngoma yake My Love aliyomshirikisha Marioo. Hata hivyo takriban siku nne baadaye, video hiyo iliondolewa youtube. Mapanch anadai aliyeiondoa ni Marioo ambaye alituma malalamiko ya hakimiliki. Msanii huyo amesema amechukizwa na kitendo hicho kwa kueleza kuwa Marioo ni mnafiki na mbaya zaidi ni yeye ndiye aliyetaka kuwepo kwenye wimbo huo. Hata hivyo Marioo amezungumza kwanini hakutaka video ya My Love aliyoshirikishwa na mapanch itoke. Marioo amesema ngoma hiyo ilikaa sana ndani licha ya kuwahimiza mara kadhaa wawaiache kuitoa kwa sababu muziki wake unabadilika kadri siku zinavyokwenda.

Read More
 MARIOO AFIKISHA VIEWS MILLIONI 100 YOUTUE

MARIOO AFIKISHA VIEWS MILLIONI 100 YOUTUE

Kuizuia nyota ya Marioo ni sawa na kuziba mwanga kwa kiganja cha mkono. Nyota huyo  kutoka Tanzania anaendelea kugonga vichwa vya habari na mara hii ni kuhusiana na idadi ya views youtube. Good news kwa mashabiki wa mkali huyo ni kwamba amefikisha watu Milioni 100 waliotazama kazi zake mbalimbali katika channel yake ya mtandao wa Youtube. Marioo alijiunga na mtandao huo Januari 4, mwaka wa 2018 na amepata watazamaji wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo. Baadhi ya matukio anayoyaweka katika mtandao huo ni video, shoo anazozifanya na utayarishaji wa video za nyimbo zake. Kutokana na idadi hiyo ya watazamaji, marioo amewaacha mbali baadhi ya wasanii wa Afrika wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki.

Read More
 MARIOO AWAPA SOMO WASANII CHIPUKIZI

MARIOO AWAPA SOMO WASANII CHIPUKIZI

Staa wa Muziki wa Bongofleva Marioo ambaye kwa sasa anafanya poa na singo yake “Mi Amor” ameamua kutoa somo kwa wasanii chipukizi. Kupitia Instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Marioo amewaambia wasanii hao kuwa wanapohitaji kutoa wimbo wahakikishe wimbo husika unakuwa mkali kuliko nyimbo zilizopo masikioni mwa watu. Mbali na hayo, ameendelea kutusanua kuhusu ujio wa album yake mpya kwa kusema kwamba album yake itaitwa “The Boy You Know” na itaingia sokoni kabla ya mwaka huu haujakamilika. Utakumbuka usiku wa kuamkia Aprili 3 kwenye hafla ya ugawaji wa tuzo za Tanzania Music Awards Marioo alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kiume wa Bongofleva na Wimbo Bora wa Bongo Fleva wa Mwaka kupitia ngoma yake ya “Beer Tamu”

Read More
 WIMBO WA MARIOO “MI AMOR” WAFIKISHA STREAMS MILIONI 10 BOOMPLAY

WIMBO WA MARIOO “MI AMOR” WAFIKISHA STREAMS MILIONI 10 BOOMPLAY

Disemba 24 mwaka wa 2021 Staa wa muziki wa Bongofleva Marioo alitubariki na singo inayokwenda kwa jina la “Mi Amor” akiwa amemshirikisha msanii wa kike nchini Jovial. Habari njema kwa mashabiki wa Marioo ni kwamba Wimbo huo umefanikiwa kufikisha jumla ya streams millioni 10 kwenye mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa Boomplay. Sanjari na hilo wimbo wa “Mi Amor” pia unazidi kufanya vizuri kwenye mtandao wa youtube kwani mpaka sasa video yake imeweza kutazamwa zaida ya mara millioni 3.3 tangu ipakiwe kwenye mtandao huo Februari 25, 2022. “Mi Amor” unakuwa wimbo wa kwanza kutoka kwa Marioo kuwa na idadi hiyo kubwa ya STREAMS, ikizipita nyimbo kama “For You” wenye streams Milioni 4.9 ulitoka mwaka jana, “Beer Tamu” wenye streams Milioni 3.8 na watatu katika top 3 ya kazi za Marioo ilizofikisha streams zaidi ya Milioni ni “Mama Amina” wenyewe una streams Milioni 1.6

Read More
 NIKKI MBISHI:  MARIOO ALISTAHILI KUPEWA MIRABAHA NA COSOTA KUTOKA KAZI ZAKE KUPIGWA SANA KWENYE MEDIA

NIKKI MBISHI: MARIOO ALISTAHILI KUPEWA MIRABAHA NA COSOTA KUTOKA KAZI ZAKE KUPIGWA SANA KWENYE MEDIA

Rapa kutoka nchini Tanzania Nikki Mbishi amesema Marioo kupitia wimbo wake “BIA TAMU” alistahili kuwa namba moja kwenye orodha ya wasanii ambao wamepata gawio la mirabaha kutoka Chama cha Hatimiliki Tanzania – COSOTA. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Nikki mbishi amesema wimbo wa Bia Tamu umepigwa kuliko wimbo wowote nchini Tanzania katika kipindi cha miezi 7 iliyopita. “Yaani mtu unakuja na hoja jenzi ambayo pengine ingewapa hamasa Con Boi na Rapcha watu wanahisi umewalinganisha. Jamaa wapo kama COSOTA wakiulizwa vigezo vya kutoa mirabaha, hata mjinga anajua MARIOO alistahili kuwa namba moja BIA TAMU imepigwa kulizo nyimbo zote kwa 7 months ago.” alichomekea Nikki Mbishi wakati akichangia hoja kwenye tweet ya Wakazi iliyoibua mjadala mzito Twitter, tangu juzi. Kwa mujibu wa COSOTA,  Ali Kiba ndiye aliongoza kwa wasanii wa bongo fleva waliopata pesa nyingi za Mirabaha ambapo alipata kiasi cha shilling 3 za Kenya huku Marioo akikosekana hata kwenye TOP 20 ya orodha hiyo.

Read More
 FOBY AUPONDA UWEZO WA MARIOO KWENYE MUZIKI WA BONGOFLEVA

FOBY AUPONDA UWEZO WA MARIOO KWENYE MUZIKI WA BONGOFLEVA

Msanii wa Bongofleva Foby amefunguka kuwa mkali wa ngoma ya “Beer tamu” Marioo hawezi kuvikwa taji la Ufalme wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania. Kupitia mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, mwanamuziki huyo amedai kwamba Marioo hawezi kuwa mfalme wa muziki wa Bongofleva ikiwa anaimba muziki wa Amapiano, kwani mfalme anatakiwa kukuza na kufanya mziki wao wa nyumbani na sio kuiga muziki kutoka mataifa mengine. HitMaker wa ngoma ya “Ode” amechukizwa na kitendo cha rapa Damian Sol kumkana hadharani kwamba hamfahamu kwa kusema kuwa rapa huyo amewavunjia heshima vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikipiga nyimbo zake ikizingatiwa kuwa wamekutana mara nyingi kwenye matamasha mbali mbali ya muziki. Ikumbukwe Foby kwa sasa anafanya vizuri kwenye Digital Platforms mbali mbali na EP yake iitwayo ME, MYSELF & 1 ambayo aliiachia rasmi mwishoni mwa mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 5 ya moto.

Read More
 BAHATI ATUHUMIWA KUIBA IDEA YA WIMBO WA JE UNANIFIKIRIA KUTOKA KWA MARIOO

BAHATI ATUHUMIWA KUIBA IDEA YA WIMBO WA JE UNANIFIKIRIA KUTOKA KWA MARIOO

Mkali wa muziki nchini Bahati ameingia tena katika mijadala kwenye mitandao nchini  baada ya kudaiwa kuiba  idea ya wimbo wa  ‘For You’ wa msanii  wa Bongofleva Marioo Kulingana na ripoti inayosambaa mitandaoni, inadaiwa Bahati ametumia mdundo na ubunifu wa video wa wimbo huo kwenye wimbo wake mpya wa”Je unanifikiria”, hivyo kuibua maswali mengi miongoni mwa wadau wa muziki nchini ambao walienda mbali zaidi na kuhoji kuwa msanii huyo amekosa ubunifu kwenye muziki wake. Hata hivyo Bahati hajetoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo yaliyoibuliwa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Read More
 MARIOO MBIONI KUJA NA “I’AM MARIOO TOUR”

MARIOO MBIONI KUJA NA “I’AM MARIOO TOUR”

Hitmaker wa Beer Tamu, Marioo ametangaza ujio wa tour yake nchini Tanzania aliyoipa jina la “I’am Marioo tour.” Marioo ameweka wazi ujio wa tour yake hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwaachia mashabiki swali kupendekeza ni mkoa gani nchini Tanzania ambao asiache kukanyaga kwenye tour yake hiyo. Pamoja na kuweka wazi ujio wa tour yake hiyo marioo hajagusia endapo kuna wasanii wengine ambao anatarajia kushirikiana nao kwenye tour hiyo au atakuwa mwenyewe tu. Kauli ya marioo inakuja siku chache baada ya kuwatolea uvivu wasanii wa bongo fleva kwa kuwaita wanafiki pale linapokuja suala la kupeana michongo ya kufanikiwa kwenye muziki

Read More