Mbosso Adai Nusra Atoe Uhai Akiwafurahisha Mashabiki Simba SC

Mbosso Adai Nusra Atoe Uhai Akiwafurahisha Mashabiki Simba SC

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Mbosso, amefunguka kuhusu namna alivyoweka nguvu kubwa kuhakikisha onyesho lake kwenye Simba Day linakuwa la kipekee, akieleza kuwa nusra ajitoe uhai wake ili kuwafurahisha mashabiki wa Simba Sports Club. Kupitia Instagram, Mbosso amesema alijiandaa kwa moyo wake wote na kuweka nguvu, muda na rasilimali nyingi kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Amebainisha kuwa mapenzi yake kwa Simba SC na mashabiki wake ndiyo yaliyomsukuma kufanya maandalizi ya hali ya juu, akisisitiza kuwa alijitolea zaidi ya kawaida ili burudani iwe ya kukumbukwa. Licha ya mafanikio makubwa ya perfomance yake, msanii huyo pia amewaomba mashabiki na viongozi wa Simba SC msamaha endapo kulikuwa na mapungufu yoyote katika utendaji wake wa Kazi, akisema yeye ni mwanadamu na hawezi kufanya kila kitu kwa ukamilifu. Simba Day hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kuzindua msimu mpya wa klabu hiyo yenye mashabiki wengi, na mwaka huu Mbosso alipewa nafasi ya kuwa headliner, nafasi ambayo amesema itaendelea kubaki kuwa kumbukumbu muhimu katika maisha yake ya muziki.

Read More
 Mbosso Ajeruhiwa Akiwa Location ya Video Shoot

Mbosso Ajeruhiwa Akiwa Location ya Video Shoot

Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Mbwana Yusuf Kilungi maarufu Mbosso, ameripotiwa kupata jeraha kwenye mguu wake wa kulia wakati wa shughuli za utayarishaji wa kazi yake mpya ya muziki. Tukio hilo lilitokea akiwa location akirekodi video, ambapo inadaiwa alidondoka ghafla baharini katika harakati za kuhakikisha mashabiki wake wanapata burudani ya kiwango cha juu. Ingawa haijafahamika ukubwa wa jeraha hilo, watu wa karibu na msanii huyo wamesema kuwa hali yake si ya kutia wasiwasi na anaendelea kupata matibabu. Mashabiki wake wameonyesha wasiwasi kupitia mitandao ya kijamii, huku wengi wakimtumia jumbe za kumtakia afueni ya haraka. Mbosso, anayejulikana kwa sauti yake ya kipekee na vibao kama Hodari na Fall, amekuwa akijiandaa na miradi mipya ya muziki, na tukio hili limekuja wakati mashabiki wakingoja kwa hamu kazi yake mpya.

Read More
 Mbosso Apata Views Nyingi Kenya Kuliko Tanzania Kwenye YouTube

Mbosso Apata Views Nyingi Kenya Kuliko Tanzania Kwenye YouTube

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva, Mbosso, ameibua mjadala baada ya takwimu kuonyesha kuwa muziki wake unasikilizwa zaidi nchini Kenya kuliko nyumbani kwao Tanzania. Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za YouTube, nyimbo za Mbosso zimeangaliwa zaidi ya mara milioni 102 kutoka Kenya, ikilinganishwa na mara milioni 47 kutoka Tanzania. Hii inamaanisha kwamba takribani asilimia 68.5 ya watazamaji wake kutoka Kenya na Tanzania wanatoka Kenya pekee. Ufanisi huu unaonyesha namna Mbosso alivyojijengea mashabiki wakubwa nchini Kenya, huku muziki wake ukiendelea kushika nafasi kwenye redio, majukwaa ya kidijitali na mitoko ya burudani. Wachambuzi wa muziki wanasema hali hii inathibitisha nguvu ya soko la Kenya kwa wasanii wa Afrika Mashariki, na kwa Mbosso, inaweza kufungua milango ya ushirikiano zaidi na wasanii wa Kenya pamoja na kuongeza idadi ya shoo katika nchi hiyo.

Read More
 Marioo Adai Hajawahi Kuandikiwa Wimbo, Mashabiki Wahoji Bifu na Mbosso

Marioo Adai Hajawahi Kuandikiwa Wimbo, Mashabiki Wahoji Bifu na Mbosso

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Marioo, amefunguka kuhusu safari yake ya muziki, akisema licha ya mafanikio makubwa aliyopata hajawahi kubebwa na lebo kubwa wala kuandikiwa wimbo na mtu yeyote. Kupitia Instastory, msanii huyo amesema kuwa yeye ndiye msanii pekee mwenye hits “back to back”, akiongeza kuwa tayari ameshinda mara kadhaa tuzo za Msanii Bora wa Mwaka (Bongo Fleva), jambo linaloashiria ukubwa wa mchango wake katika tasnia. Marioo, ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake “Dunia”, pia amewajibu mashabiki waliokuwa wakimtaka kutoa, “Global Song”, akiahidi kwamba wimbo huo utapatikana kwenye Deluxe Version ya albamu yake “The God Son”, iliyotoka rasmi mwezi Novemba 2024. Kauli hiyo ya Marioo imepokewa kwa mitazamo tofauti, huku baadhi ya mashabiki wakidai huenda ujumbe huo umemlenga aliyekuwa staa wa WCB, Mbosso, ambaye juzi kati Diamond Platnumz alidai kwamba ndiye aliyeandika wimbo wake maarufu “Pawa.” Hali hiyo imezidisha minong’ono ya uwepo wa bifu la chini kwa chini kati ya Marioo na Mbosso, hasa ikizingatiwa kuwa wote wanahesabika kati ya waimbaji wenye mashabiki wengi na nyimbo zinazotamba kwa sasa.

Read More
 Mbosso Ajibu Madai ya Diamond Platnumz Kuhusu Deni na Uandishi wa Nyimbo

Mbosso Ajibu Madai ya Diamond Platnumz Kuhusu Deni na Uandishi wa Nyimbo

Mzozo kati ya Diamond Platnumz na msanii wake wa zamani Mbosso umeendelea kuchukua sura mpya baada ya wawili hao kufichua mambo ya ndani ya Label ya WCB Wasafi. Baada ya Diamond kudai kuwa ameandika nyimbo nyingi za Mbosso na kumkopesha zaidi ya shilingi milioni 323 ambazo hakulipwa, Mbosso naye amejibu kwa kueleza kuwa yeye pia amekuwa akishiriki kuandika nyimbo za Diamond, ingawa hataki kuzitaja. Amesema tangu enzi zake akiwa Yamoto Band, Diamond alikuwa akimuita nyumbani kwake au studio kushiriki katika kazi hizo. Kupitia Instastories, Mbosso amekanusha madai kwamba anamwonea wivu Diamond, akibainisha kuwa kuna watu wa kati wanaojaribu kuwapandikizia uhasama. Amesema wazi kuwa huenda Diamond alikuwa na jambo moyoni kwa muda mrefu na sasa ameona wakati umefika wa kulitoa hadharani. Hata hivyo, licha ya mkanganyiko huo, Mbosso amesema ataendelea kumheshimu Diamond kwa mchango wake mkubwa katika maisha yake ya muziki. Kwa upande wake, Diamond amesisitiza kuwa Mbosso aliachwa na deni kubwa alipoondoka WCB, lakini aliamua kumsamehe bila malipo yoyote. Aidha, Diamond amedai kuwa wakati Rayvanny anaondoka WCB, Mbosso alimshawishi asifanye kazi naye, akimpinga kushirikiana naye kwenye nyimbo. Hata hivyo, Diamond amesema alikataa kuingiwa na chuki, akisisitiza kuwa kuondoka kwa msanii kwenye Label hakupaswi kuwa chanzo cha ugomvi.

Read More
 Mbosso Amtaka Diamond Kuvunja Ukimya Kuhusu Kauli za Baba Levo

Mbosso Amtaka Diamond Kuvunja Ukimya Kuhusu Kauli za Baba Levo

Mwanamuziki Mbosso ameibuka na kuweka wazi msimamo wake kufuatia mvutano unaoendelea mitandaoni kati yake, Diamond Platnumz, na Baba Levo, kuhusu tuhuma za kushirikiana kumchafua kwa jina au kazi zake. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Mbosso amesema kwa uwazi kuwa hana ukaribu wowote na Baba Levo, na hivyo hawezi kushirikiana naye kwa jambo lolote, tofauti na madai yanayoenezwa. Amefafanua kuwa yeye si mtu wa migogoro, na kwamba anamuheshimu Diamond kama kiongozi na kama msanii mkubwa aliyechangia ukuaji wa muziki wake. Hata hivyo, Mbosso amesisitiza kuwa ni wajibu wa Diamond kuzungumza hadharani kumkemea Baba Levo, kwani ukimya wake unaweza kutafsiriwa kama kukubaliana au kuunga mkono vitendo vya matusi na kejeli vinavyotolewa hadharani na Baba Levo. Kauli ya Mbosso imekuja muda mfupi baada ya Baba Levo kumuomba msamaha na Diamond Platinumz akidai kuwa hana ajenda yoyote na Mbosso ya kumchafulia brand yake. “Mzee Lukuga, sina Agenda yoyote na Mbosso na wala siwezi kupanga njama yoyote na Mbosso, nisamehe mzee wangu” Aliandika Instagram. Ikumbukwe jana kulizuka sintofahamu kati ya Mbosso na Baba Levo baada ya Baba Levo kudai kuwa ngoma ya Pawa imetungwa na Diamond Platnumz, ambapo Mbosso alikasirika na kudai huenda WCB inamfanyia figisu wakati aliondoka salama na anaheshimu sana mchango wao kwenye muziki na mara zote amekuwa akiwashukuru.

Read More
 Mbosso Aachia EP Mpya Room Number 3

Mbosso Aachia EP Mpya Room Number 3

Staa wa Bongo Fleva Mbosso ameanza ukurasa mpya katika muziki wake kwa kuachia EP yake ya tatu iitwayo Room Number 3, miezi michache baada ya kuondoka kwenye lebo ya WCB Wasafi. EP hiyo, ambayo ina nyimbo 7 bila collabo yoyote, tayari imechukua nafasi ya kwanza kwenye majukwaa makubwa ya muziki kama Apple Music na Spotify, hatua inayothibitisha kuwa Mbosso bado ni nguvu kubwa kwenye tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki. Nyimbo zilizopo kwenye EP hiyo ni: Pawa, Nusu Saa, Tena, Merijaah, Siko Single, Aviola, na Asumani. Maudhui ya EP yanahusu mapenzi, maisha na hisia za kina, yakionyesha ubunifu wa Mbosso akiwa msanii huru. Kwa mashabiki wa muziki wa Kiswahili, Room Number 3 ni ishara ya mwanzo mpya kwa Mbosso, na sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya kidijitali.

Read More
 Mbosso anyosha maelezo kuhusu kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Mbosso anyosha maelezo kuhusu kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Msanii wa Bongo Fleva, Mbosso amefunguka kuhusu tatizo la ugonjwa wa moyo ambalo limemwandama tangu akiwa mtoto. Akizungumza katika mahojiano maalum Mbosso ambaye ni msanii wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) amesema kwamba ugonjwa huo unasababishwa na mafuta kuwa mengi kwenye mishipa ya damu ya kwenda kwenye moyo. Dalili alilozitaja za ugonjwa huo ni pamoja na maumivu upande wa kushoto wa kifua, viungo kupoteza hisia na kwake anatetemeka vidole. Hata hivyo Mbosso amesema tangu atambue kuwa ana ugonjwa huo wa moyo amekuwa akimtembelea daktari wake mara kwa mara na kuyafuata maagizo yake katika juhudi za kutaka kupo.

Read More
 Mbosso afunguka sababu za kusitisha tour yake nchini Marekani

Mbosso afunguka sababu za kusitisha tour yake nchini Marekani

Nyota wa muziki wa Bongofleva, Mbosso ambaye kwa sasa anafanya vizuri na EP yake mpya, amesitisha ziara (tour) yake ya muziki nchini Marekani hadi tarehe mpya zitakapotangazwa tena. Marekani ambayo ilitarajiwa kuanza Novemba 25 mpaka Desemba 16, 2022. Kupitia instastory ya Mbosso metoa sababu za Kusitisha Ziara yake ya kwa kusema kuwa Daktari amemtaka kutokusafiri au kukaa kwenye Ndege kwa zaidi ya Masaa nane. Mbali na hayo Mbosso ameahidi kuwa Tour hiyo itaendelea pindi atakapo pata ruhusa kutoka kwaa Daktari.. Itakumbukwa, ziara (tour) hiyo ya Mbosso ilitakiwa kuanza rasmi mwezi huu, tarehe 25 na kumalizika Desemba 16.

Read More
 Wimbo mpya wa Mbosso “Yataniua” wafutwa youtube kwa madai ya hakimiliki

Wimbo mpya wa Mbosso “Yataniua” wafutwa youtube kwa madai ya hakimiliki

Siku moja baada ya msanii kutoka lebo ya WCB, Mbosso kuzindua EP yake aliyoipa jina la KHAN katika ufukwe wa Bahari Beach jijini Dar es Salaam, moja kati ya nyimbo sita zilizomo kwenye EP hiyo imeondolewa Youtube. Ngoma iliyoondolewa, inaitwa Yataniua ambayo Mbosso ameimba na bosi wake, Diamond Platnumz na hivyo kufanya ngoma zilizosalia YOUTUBE kuwa tano, Asalaam, Wayo, Shetani, Pole na Huyu Hapa. Tangu kuzinduliwa kwa EP hiyo, kuliibuka mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, Diamond akituhumiwa kuigilizia nyimbo mbili kwenye kipande alichoimba katika wimbo huo. Kipande cha kwanza anachodaiwa kukopi ni kutoka kwa msanii Asake wa Nigeria katika Wimbo wake wa Peace Be Unto You ambapo alichokibadilisha Diamond ni maneno tu lakini staili ya uimbaji inafanana kwa kila kitu na kipande hicho cha Asake. Kipande cha pili ambacho Diamond anadaiwa kukopi, ni kutoka kwenye ngoma ya Adiwele kutoka kwa msanii wa Afrika Kusini, Young Stunna akiwa amewashirikisha Kabza De Small na DJ Maphorisa. Bado haijafahamika ni nini sababu kubwa ya kuondolewa kwa ngoma hiyo ingawa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba huenda wenye nyimbo zao wameuripoti wimbo huo kwa kukiuka sheria za hati miliki. Licha ya kuondolewa Youtube, bado wimbo huo unaendelea kupatikana kwenye platforms nyingine kama Audiomack na Spotify.

Read More
 Mbosso atangaza ujio wa ziara yake ya muziki nchini Marekani

Mbosso atangaza ujio wa ziara yake ya muziki nchini Marekani

Mwimbaji nyota kutoka lebo ya WCB, Mbosso ametangaza rasmi ujio wa ziara yake kimuziki ya kimatifa ya Marekani. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema ziara hiyo itaanza rasmi tarehe 25, mwezi Novemba hadi 16, mwezi Desemba. “King Khan Live in USA: Nov 25th – Dec 16th.”, Amaandika Mbosso. Mbosso ambaye ana zaidi ya streams Milioni 100 katika mtandao wa Boomplay, kwenye mahojiano yake na Dizzim Online mwishoni mwa wikiendi hii iliyoputa, aliweka wazi Oktoba 21, anaachia EP yake mpya ambayo ameitaja kuwa ndio project yake atakayoifungia mwaka.

Read More
 MBOSSO AFUNGUKA KUFANYA KAZI NA RAYVANNY

MBOSSO AFUNGUKA KUFANYA KAZI NA RAYVANNY

Hitmaker wa “Moyo”, Msanii Mbosso amefunguka uhusiano wake na Bosi wa Next Level Music Rayvanny. Katika mahojiano yake hivi karibuni Mbosso amesema licha ya Rayvanny kuondoka kwenye lebo ya WCB bado wana uwezo wa kufanya kazi pamoja kwani wao ni marafiki wakubwa. “Ni mwanangu, kwa hiyo inapokuja kazi ambayo natakiwa nifanye na Rayvanny lazima tufanye ni rafiki yangu, nakutana naye, anakuja ofisini tunapiga stori, yaani hakuna noma,” amesema Mbosso. Julai mwaka huu Rayvanny alijiondoa rasmi kwenye lebo ya WCB aliyoitumikia kwa miaka saba na kuelekeza nguvu zake katika lebo yake, Next Level Music ambayo inamsimamia msanii Mac Voice. Utakumbuka chini ya WCB Mbosso alimshirikisha Rayvanny katika wimbo wake uitwao Pakua kutoka kwenye albamu yake, Definition of Love huku Rayvanny akimshirikisha Mbosso kwenye ngoma yake, Zuena inayopatika kwenye albamu, Sound From Africa.

Read More