Megan Thee Stallion Afunguliwa Kesi Mpya Mahakamani
Jaji katika Mahakama Kuu ya Los Angeles ameamuru kuwa rapa maarufu Megan Thee Stallion na kampuni yake ya usimamizi Roc Nation wakabiliane na kesi ya madai yaliyowasilishwa na mpiga picha wake wa zamani, Emilio Garcia. Mwezi Aprili 2024, Emilio Garcia alifungua kesi akidai kuwa alilazimika kushuhudia tendo la ngono lililotokea wakati Megan alikuwa kwenye ziara yake ya muziki (Tour). Aidha, Emilio anadai pia kutolipwa malipo yake kwa kazi za muda wa ziada alizofanya akiwa mpiga picha binafsi wa rapa huyo, ambapo alihudumu kati ya mwaka 2018 hadi Juni 2023. Kesi hiyo bado inaendelea mahakamani, huku mawakili wa Megan Thee Stallion na Roc Nation wakipinga vikali madai hayo. Wakili wa upande wa Megan amesisitiza kuwa madai ya Emilio Garcia ni ya uongo na yanatumiwa kama mbinu ya kumchafua jina la mteja wao. Hata hivyo, mahakama imeamua kuwa madai hayo ya Emilio yatalazimika kushughulikiwa kisheria huku pande zote zikitoa hoja zao mbele ya jaji. Kesi hii imevutia umakini mkubwa kutoka kwa vyombo vya habari na mashabiki wa rapa huyo, huku wengi wakisubiri kuona hatma ya kesi hii ambayo inaweza kuwa na athari kwa hadhi ya Megan Thee Stallion na kampuni yake.
Read More