Drake amchana Kanye West na Megan Thee Stallion kupitia wimbo wa Circo Loco

Drake amchana Kanye West na Megan Thee Stallion kupitia wimbo wa Circo Loco

Rapa kutoka Marekani Drake ameamua kutapika nyongo kwenye “Circo Loco” ngoma ambayo inapatikana kwenye Album ya pamoja na 21 Savage, Her Loss. Drizzy amefunguka ya moyoni kwamba aliamua kupatana na Kanye West na kufanya onesho la pamoja (Free Larry Hoover Concert) Disemba 10, mwaka 2021 kwa sababu ya heshima tu ya godfather wake, J. Prince. “Linking with the opps, b*tch, I did that shit for J Prince. B*tch, I did it for the mob ties” – amechana Drizzy. Utakumbuka Drake pia kupitia hii single amemchana Megan Thee Stallion kufuatia madai yake ya kupigwa risasi na Tory Lanez kwa kusema kuwa alidanganya juu ya tukio hilo. “This b**ch lied about getting shot but she still a stallion. She don’t even get the joke but she still smiling.” amechana Drake.

Read More
 Megan Thee Stallion avamiwa, wezi waondoka na mali ya mamilioni

Megan Thee Stallion avamiwa, wezi waondoka na mali ya mamilioni

Nyumba ya Rapa Megan Thee Stallion ya mjini Los Angeles, nchini Marekani imevamiwa na majambazi ambao walifanikiwa kuiba vitu vyenye thamani ya takribani shillingi millioni 36 za Kenya. Tovuti ya TMZ imeripoti kwamba watu wawili walionekana wakivunja milango na kuingia kwenye nyumba hiyo hadi chumbani ambapo waliiba vito vyake vya thamani na pesa taslimu. Wakati tukio hilo linatokea, Megan Thee Stallion hakuwepo ndani, alikuwa mjini New York ambapo baada ya kupata taarifa hizo aliingia Twitter na kuelezea hisia zake lakini pia kutangaza kuchukua mapumziko kwenye muziki baada ya onesho lake kwenye kipindi cha Saturday Night Live (SNL) wikendi hii.

Read More
 MEGAN THEE STALLION AJIBU TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DABABY

MEGAN THEE STALLION AJIBU TUHUMA ZA KUTOKA KIMAPENZI NA DABABY

Rapa kutoka Marekani Megan Thee Stallion ni kama amemjibu DaBaby baada ya kufunguka kwenye ngoma yake mpya kwamba alifanya mapenzi na Megan siku moja kabla ya tukio ambalo anadai kupigwa risasi mguuni na Tory Lanez. DaBaby alifunguka hayo kupitia ngoma yake mpya “BOOGYMAN” na kusema amekuwa akitoka na Megan mara kibao tu. Sasa ni kama Thee Stallion ameamua kumjibu DaBaby ambapo akiwa Jukwaani kwenye Tamasha la iHeartRadio, alisikika akisema “Sifahamu kuhusu ninyi, lakini Mimi binafsi naupenda sana mwili wangu.” ishara ya kukanusha yote yaliyoimbwa na DaBaby.

Read More
 DAKTARI KWENYE KESI YA TORY LANEZ ATHIBITISHA MEGAN THEE STALLION KUKATWAA NA VIOO

DAKTARI KWENYE KESI YA TORY LANEZ ATHIBITISHA MEGAN THEE STALLION KUKATWAA NA VIOO

Daktari amethibitisha kwamba Megan Thee Stallion hakupigwa risasi mguuni kama anavyodai bali alikatwa na vioo kwenye tukio ambalo linamtaja Tory Lanez kumpiga risasi. Uchunguzi umebainisha kwamba baada ya kutokea vurugu baina ya washkaji ambao walikuwa pamoja nao kwenye gari, zilipigwa risasi kadhaa ambazo zilivunja vioo vya gari na wakati Megan Thee Stallion akijitahidi kutoka nje ya gari, alivikanyaga na kumuumiza. Aprili 6 mwaka huu Tory Lanez aliachiwa kwa dhamana ya shilling milllioni 40 za Kenya baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka amri ya mahakama iliyotolewa kumkinga Megan Thee stallion kwenye shtaka lao linaloendelea. Ikumbukwe Tory Lanez anakabiliwa na Mashtaka mawili ambayo ni kumshambulia rapa Megan thee Stallion mwaka 2020 na pia kubeba silaha yenye risasi kinyume na sheria.

Read More