Mercy Kyallo Akanusha Kuwatapeli Wateja Kupitia Yallo Leather

Mercy Kyallo Akanusha Kuwatapeli Wateja Kupitia Yallo Leather

Mjasiriamali na mdogo wake mtangazaji maarufu Betty Kyallo, Mercy Kyallo, ameweka wazi kilichosababisha sintofahamu kuhusu ucheleweshaji wa oda za bidhaa zake maarufu za ngozi chini ya brand yake ya Yallo Leather. Kupitia Instagram, Mercy ameeleza kuwa changamoto hiyo imetokana na wazalishaji wawili wakuu wa malighafi kufunga biashara, jambo lililosababisha upungufu wa vifaa muhimu na hivyo kusababisha mkwamo wa uzalishaji. Mrembo huyo amehakikishia wateja wake kuwa hakuna oda itakayopotea na kwamba kila mteja atapokea bidhaa yake. Lakini pia amekanusha madai ya kutapeli, akibainisha kuwa biashara yake imesimama kwa misingi ya uaminifu na uwazi. Kwa mujibu wa mjasiriamali huyo, Yallo Leather bado ipo imara na changamoto zinazoshuhudiwa kwa sasa ni za muda tu. Ameomba wateja wake waendelee kuwa na subira wakati oda zilizokwama zikikamilishwa. Yallo Leather imekuwa ikivutia wapenzi wa mitindo kwa ubunifu na ubora wa bidhaa zake, na licha ya changamoto hizo za muda mfupi, mashabiki wengi wameendelea kumpa moyo Mercy huku wakisubiri bidhaa zao kwa hamu.

Read More
 Mercy Kyallo Adaiwa Kuwalaghai Wateja Kupitia Kampuni ya Yallo Leather

Mercy Kyallo Adaiwa Kuwalaghai Wateja Kupitia Kampuni ya Yallo Leather

Mfanyabiashara na dada yake aliyekuwa mtangazaji maarufu Betty Kyallo, Mercy Kyallo, ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kufichuliwa kwa madai ya kuwalaghai wateja wake kupitia kampuni yake ya bidhaa za ngozi, Yallo Leather. Kwa mujibu wa malalamiko yaliyosambaa mitandaoni, wateja kadhaa wamedai kuwa walinunua mikoba kutoka kwa Yallo Leather kwa kulipia mapema, lakini baada ya hapo walipoteza mawasiliano na kampuni hiyo. Wengine wamesema walipewa visingizio visivyoisha kwa miezi mingi kabla ya kupata majibu yoyote ya maana. “Tulilipa, tukasubiri kwa wiki na miezi, lakini Mercy na timu yake walitoweka kimya. Tulilazimika kuhusisha polisi ndipo tukarudishiwa pesa zetu,” alisema mmoja wa wateja kupitia mtandao wa X (zamani Twitter). Wengi wameeleza kuwa walituma malalamiko kupitia nambari za huduma kwa wateja za kampuni hiyo bila mafanikio, na walihisi kana kwamba walikuwa wameachwa gizani baada ya kulipa pesa zao. Baadhi yao walidai kurudishiwa hela zao tu baada ya kupeleka suala hilo kwa mamlaka za usalama. Kampuni ya Yallo Leather, ambayo hapo awali ilisifiwa kwa bidhaa zake za kipekee zinazotengenezwa kwa ngozi halisi, sasa inakabiliwa na changamoto kubwa ya kuaminika. Hadi sasa, Mercy Kyallo hajatoa tamko rasmi kuhusu madai hayo, jambo ambalo linaendelea kuongeza wasiwasi miongoni mwa wateja wake na umma kwa ujumla. Wananchi na wateja waliolalamika sasa wanaitaka kampuni hiyo kutoa maelezo ya kina na kuhakikisha haki inatendeka kwa wale waliolaghaiwa. Wengine pia wametaka mashirika ya kibiashara na walinda haki za walaji kufuatilia suala hili kwa karibu ili kulinda wateja wengine wasipitie hali kama hiyo.

Read More