Msanii Mr Seed Awataka Mabloga Wazingatie Muziki Badala ya Skendo
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mr Seed, amewaonya mabloga na vyombo vya habari vya burudani kuzingatia kazi za wasanii badala ya kueneza skendo zisizo na tija. Kupitia Instastory yake, Seed amesema kuwa mara nyingi wanamuziki nchini hukosa kupata nafasi ya kupigiwa debe kutokana na kuelezewa zaidi kupitia skendo, hali inayodidimiza ubunifu na maendeleo ya muziki. Mr Seed ameongeza kuwa wasanii wanahitaji uungwaji mkono kwa kazi zao ili kukuza tasnia ya muziki wa Kenya kimataifa, na akasisitiza kuwa muziki ndio kiini cha utambulisho wao, si skendo binafsi. Hata hivyo, amesema amesikitishwa kuona juhudi zake hazipewi kipaumbele kwenye mitandao ya habari za burudani, huku skendo ndizo zikipewa uzito. Kauli yake inakuja muda mfupi baada ya kuachia kibao kipya kinachoitwa Baby, ambacho ameshirikiana na kundi la Ethic Entertainment.
Read More