MR SEED AMZAWADI MAMA YAKE MZAZI KIPANDE CHA ARDHI

MR SEED AMZAWADI MAMA YAKE MZAZI KIPANDE CHA ARDHI

Msanii nyota nchini Mr. Seed anazidi kujipakulia baraka ya wazazi wake mara baada ya kumzawadi mama yake mzazi kipande cha ardhi ambacho ana mpango wa kumjengea mjengo wa kifahari. Kupitia video aliyoiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram Bosi huyo wa lebo ya muziki ya Starborn Empire ametusanua kuwa shamba hilo aliyomnunulia mama yake lipo eneo la Matuu, Kaunti ya Machakos. Hakuishia hapo ameenda mbali zaidi na kutoa ushuhuda wa ndani ya maisha yake kwa kusema kwamba kuna kipindi familia yake ilipitia maisha magumu kiasi cha kukosa chakula kila siku. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ndoa” amewahimiza vijana na mastaa wenzake kukumbuka  wazazi wao wanapofanikiwa kimaisha kwa kuwanunulia vitu vya thamani kwani bila wao wasingeweza kufanikisha baadhi ya malengo yao. Utakumbuka mwaka wa 2018 Mr. Seed alimzawadi mama yake mzazi gari mpya aina Toyota Audi kwa kuwa mama bora kwake lakini pia mwaka wa 2021 aliingia kwenye headlines nchini alipomnunulia mke wake Nimo gari mpya aina ya Mazda Demio kwa kusimama nae kipindi ambacho alikuwa amefulia kiuchumi.

Read More
 MR. SEED AMVUA NGUO RINGTONE, AMSHAURI AFUNGE NDOA KWANI UMRI UNAMPA KISOGO

MR. SEED AMVUA NGUO RINGTONE, AMSHAURI AFUNGE NDOA KWANI UMRI UNAMPA KISOGO

Nyota wa muziki nchini Mr. Seed ameibuka na kumtaka staa wa muziki wa nyimbo za injili Ringtone kuoa. Msanii huyo amedai kwamba Ringtone ameshakuwa mtu Mzima, hivyo anaamini kuwa akioa itamletea heshima sana katika jamii. Akiwa kwenye moja ya interview Mr. Seed amesema majukumu ya ndoa pekee ndiyo yatamnyamazisha Ringtone ambaye katika siku za hivi karibu amekuwa gumzo mitandaoni kutokana na sarakasi zake. Hitmaker huyo wa “Dawa ya Baridi” amesema amechoshwa na mienendo ya Ringtone kuingilia ndoa za wasanii wenzake kila mara ikizingatiwa kuwa yeye binafsi ameshindwa kumpata mwanamke wa ndoto yake. Hata hivyo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba ringtone ni msherati namba moja ambaye amejificha kwenye muziki wa injili kwani amekuwa na mazoea ya kuzama kwenye  DM za warembo wa  Instagram akiomba penzi. Kauli ya mr seed imekuja mara baada ya ringtone kuonekana kumshambulia kila mara kwenye interviews mbali mbali kufuatia hatua yake ya kuanza kuimba nyimbo za mapenzi tofauti na muziki wa injili ambao ulimtambulisha kwenye kiwanda cha muziki nchini

Read More
 “BLACK CHILD ALBUM” YA MR. SEED YAFIKISHA STREAMS 500,000 BOOMPLAY

“BLACK CHILD ALBUM” YA MR. SEED YAFIKISHA STREAMS 500,000 BOOMPLAY

Nyota wa muziki nchini Mr. Seed anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Albamu yake “Black Child” ambayo tayari ina takriban wiki tatu tangu itoke rasmi.   Album ya “Black Child” ambayo ndio albamu ya kwanza ya  Mr. Seed tangu aanze muziki imefanikiwa kufikisha  zaidi ya Streams laki tano kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay.   Ikumbukwe album ya Black Child kutoka kwa mtu mzima iliachiwa rasmi Septemba 13 mwaka huu wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 10 ya moto huku  ikiwa na kolabo 9 pekee.    

Read More