CAROL SONNIE AMJIBU KIMAFUMBO BABY DADDY WAKE MULAMWAH

CAROL SONNIE AMJIBU KIMAFUMBO BABY DADDY WAKE MULAMWAH

Baby Mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carrol Sonnie amefunguka kwa mara ya kwanza siku chache baada ya Mulamwah kuibua kashfa nzito dhidi yake. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram ameandika ujumbe wa mafumbo ambao umetafsiriwa Β na walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuwa inamlenga moja kwa moja mpenzi wake wa zamani mulamwah. “Wakati maisha inakupa sababu mia moja ya kuangua kilio na kuhuzunika, una jukumu la kuonesha maisha sababu millioni moja ya kutabasamu na kushukuru. Baki na nguvu,” Ameandika Caroll Sonnie kupitia Instastory yake. Utakumbuka juzi kati Mulamwah aliibuka kupitia mitandao yake ya kijamii na kufunguka mengi kuhusu maisha yake ya ndani kwa kusema kwamba alivunja mahusiano yake na Carol Sonnie baada ya mrembo huyo kumsaliti kimapenzi kwa kutoka na mwanaume mwingine. Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kumkana mtoto aliyezaa na Carol Sonnie kwa kusema kuwa sio wake kwa kusema mtoto huyo sio wake.

Read More
 MULAMWAH AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI LEBO YAKE YA MUZIKI

MULAMWAH AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI LEBO YAKE YA MUZIKI

Mchekeshaji maarufu nchini Kendrick Mulamwah amemtambulisha rasmo msanii wake mpya kwenye lebo yake ya muziki ya Mulamwah Entertainment. Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchekeshaji huyo amesema msanii wake anaitwa Ruth K ambapo amemshukuru kwa kuonyesha uvumilivu na bidii kabla ya lebo yake hajachukua hatua ya kusimamia shughuli zake za muziki. Mbali na hayo Mulamwah amekanusha kuwa kwenye mahusiano na mrembo kama inavyodhaniwa mtandaoni kwa kusema kwamba watu walitafsiri vibaya ukaribu wao huku akikiri kuwa kwa sasa hana mpenzi kwani ameelekeza nguvu zake kwenye suala la kufanyia kazi shughuli zake. Hata hivyo amesema wimbo mpya wa msanii wake Ruth K akiwa ameshirikisha val wambo kwa jina la Serereka utatoka rasmi siku ya Ijumaa Aprili mosi mwaka huu Ruth anakuwa msanii wa pili kusaini na lebo ya muziki ya mulamwah Entertainment baada ya Val Wambo aliyetambulishwa chini ya lebo hiyo mwishoni mwa mwaka wa 2021.

Read More
 MCHEKESHAJI KENDRICK MULAMWAH AGEUKIA MUZIKI WA HIPHOP

MCHEKESHAJI KENDRICK MULAMWAH AGEUKIA MUZIKI WA HIPHOP

Mchekeshaji maarufu nchini Kendrick Mulamwah ameamua kugeukia muziki wa Hiphop ikiwa ni katika kutimiza ndoto zake za kuwa rapa. Mulamwah ambaye ametamba kwenye fani ya ucheshi kwa miaka mingi ameachia rasmi wimbo wake wa kwanza wenye mahadhi ya HipHop ambao kaupa jina la “The Recoil Freestyle”. Kuptia ngoma hiyo ambayo ni disstrack, mchekeshaji huyo amesikika akiwachana watu wote ambao wamekuwa wakimubeza kupitia kazi zake za ucheshi mara baada ya kuachana na Baby Mama wake Carol ‘Sonnie’ Muthoni. Hata hivyo ngoma hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kumkatisha tamaa asigeukia muziki kwani hana kipaji cha kurap huku wengine wakimpongeza kwa hatua ya kuonesha upande wake mwingine kando na ucheshi. Mulamwah anajiunga kwenye orodha ya mastaa kama Prof. Harmo, na Flaqo ambao hapo awali walitambulika kama wasanii wa ucheshi na baadae wakageukia kufanya muziki.

Read More
 BABY MAMA WA MULAMWAH CAROL SONNIE AWACHARUKIA WANAOMPONDA MTANDAONI

BABY MAMA WA MULAMWAH CAROL SONNIE AWACHARUKIA WANAOMPONDA MTANDAONI

Baby mama wa mchekeshaji Mulamwah, Carol Sonnie amesikitisha na namna baadhi ya watu ambao wameanza kufanya mzaha na ishu ya kuachana na mchekeshaji huyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Carol Sonnie ameandika waraka mrefu akiwataka wanaotumia picha yake wakidai kwamba wanachumbia kushusha picha hizo ujumbe ambao umetafsiriwa unamlenga mchekeshaji Propesa ambaye juzi kati alipost picha ya mrembo huyo akidaiwa kuwa ni wapenzi. Mrembo huyo ambaye ni mtoto wa mmoja amesema kitendo hicho sio cha kingwana ikizingatiwa kuwa inamharibia sifa mbele ya umma pamoja na mtoto wake. Hata hivyo amewatolea uvivu wale ambao wanashinikiza afanye vipimo vya DNA kubaina kama kweli mtoto wake huyo ni wa Mulamwah kwa kusema kwamba jambo hilo ni lake na Baby Daddy wake huku akisisitiza kuwa kuachana kwao haihusiani na mtoto wao. Ikumbukwe Mulamwah ambaye ni baba ya mtoto mmoja kwa sasa na baby mama wake Carol Sonnie waliweka wazi uhusiano wao mwaka wa 2017.

Read More