Nandy na Billnass Wavishana Pete Tena Baada ya Kwanza Kupotea

Nandy na Billnass Wavishana Pete Tena Baada ya Kwanza Kupotea

Wasanii wa Bongo Fleva, Nandy na Billnass,wamevalishana pete kwa mara nyingine tena baada ya pete yao ya kwanza kuripotiwa kupotea. Nandy amethibitishwa tukio hilo kupitia Instastory yake, ambapo ameshiriki video ikionyesha wakitoka kanisani ambako walienda mahsusi kwa ajili ya kufanyiwa ibada maalum na kupata baraka kutoka kwa mchungaji Katika video hiyo, wanandoa hao wanaonekana wakiwa na furaha huku mashabiki wengi wakisifu uamuzi wao na kuona kama ishara ya uthabiti wa uhusiano wao. Kupotea kwa pete ya awali kulikuwa kumeibua maswali miongoni mwa mashabiki, lakini hatua yao ya kuvalishana pete upya imeweka wazi kwamba wanadumisha safari yao ya kimapenzi kwa msimamo na upendo.

Read More
 Nandy Afunguka Sababu za Kutumia AI Kwenye Video ya Sweety

Nandy Afunguka Sababu za Kutumia AI Kwenye Video ya Sweety

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Nandy, amefunguka sababu kuu ya kutumia teknolojia ya Artificial Intelligence (AI) katika utayarishaji wa video ya wimbo wake uitwao Sweety aliomshirikisha Jux, akisema hatua hiyo ilikuwa ya kulinda ndoa na heshima za kifamilia. Kwenye mahojiano hivi karibuni, Nandy amesema wazo la kutumia AI lilitokana na tahadhari baada ya kutambua kuwa baadhi ya mashabiki wanaweza kutafsiri vibaya maudhui ya video hiyo endapo wangeonekana pamoja katika baadhi ya sehemu zenye hisia za kimahaba. Amesema kama msanii aliyeolewa, anapaswa kuwa makini na aina ya kazi anazofanya ili kuepuka kuzua tafsiri zisizofaa kwa mume wake na mashabiki wake. Aidha, Nandy ameeleza kuwa teknolojia ya AI imesaidia kufanikisha video yenye ubora wa kimataifa bila wao kuhitaji kuigiza kwa pamoja. Hatua hiyo pia imeonyesha namna muziki wa Afrika Mashariki unavyoweza kutumia ubunifu wa kisasa kutatua changamoto za kijamii bila kuathiri ubora wa kazi za sanaa.

Read More
 Nandy Asema Ana Nyota ya Ajabu Kwenye Muziki wa Bongofleva

Nandy Asema Ana Nyota ya Ajabu Kwenye Muziki wa Bongofleva

Mwanamuziki kutoka Tanzania, Nandy, amejivunia safari yake ya takribani miaka 10 katika tasnia ya muziki wa Bongofleva, akisema kuwa kila wimbo anaouachia unakuwa hit na kupokelewa kwa kishindo na mashabiki. Kupitia Instastory, Hit maker huyo wa “Sweety” amewashukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono tangu alipoanza rasmi safari yake ya muziki, akisisitiza kuwa bila wao asingefika alipo leo. Nandy amesema kuwa anahisi ana nyota ya ajabu kwenye muziki, kwani kila mara anapotoa kazi mpya haipiti muda mrefu kabla haijatawala chati na kufurahiwa na mashabiki ndani na nje ya Tanzania. Ameongeza kuwa safari yake haijakuwa rahisi, lakini kujituma, nidhamu na baraka za Mungu zimemsaidia kudumu kwa muda mrefu huku akiendelea kushikilia nafasi yake kama mmoja wa wasanii wakike wenye ushawishi mkubwa kwenye Bongo Fleva.

Read More
 Sakata la Hakimiliki Lavuruga Kazi Mpya ya Nandy na Jux

Sakata la Hakimiliki Lavuruga Kazi Mpya ya Nandy na Jux

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy, ameonyesha kuchukizwa na hatua ya msanii chipukizi anayefahamika kama Bride Vuitton, ambaye amewasilisha maombi YouTube kutaka wimbo wake mpya “Sweety” aliomshirikisha Jux kushushwa kwa madai ya hakimiliki {copyright} Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy ameeleza kuwa kufika hatua aliyo nayo sasa kumemgharimu jitihada na uwekezaji mkubwa, jambo ambalo anaona halithaminiwi na kitendo cha Bride Vuitton. Amesema kuwa msanii huyo mchanga ameona sakata hilo kama fursa ya kujitengenezea umaarufu, lakini hajafikiria hasara kubwa ambayo hatua hiyo inaweza kusababisha kwa kazi yake mpya. Nandy ameongeza kuwa Bride Vuitton angetafuta njia nyingine za kujiweka kwenye tasnia bila kuhusisha kazi ya wasanii wenzake. Kwa mujibu wake, kitendo cha kutaka kushusha video ya “Sweety” siyo tu kumrudisha nyuma bali pia kinahatarisha ndoto na uwekezaji wake mzima. Hata hivyo, licha ya kukasirishwa na kitendo hicho, Nandy amewataka mashabiki wake pia kumpa sapoti Bride Vuitton kwa kusikiliza wimbo wake “Joro”, akisisitiza kuwa njia bora ya kupata nafasi katika muziki ni kupitia jitihada na uvumilivu, si kwa kuua ndoto za wengine.

Read More
 Nandy Afunguka Sababu za Kukosekana kwa Video ya “Tonge Nyama”

Nandy Afunguka Sababu za Kukosekana kwa Video ya “Tonge Nyama”

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Nandy, ametangaza rasmi kuwa hakutakuwa na video ya wimbo wake mpya alioufanya kwa ushirikiano na msanii Marioo, unaoitwa “Tonge Nyama.” Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nandy amefafanua kwamba mashabiki wengi wamekuwa wakimuuliza kuhusu video ya wimbo huo na nafasi ya Marioo katika promosheni yake. Amebainisha kuwa wimbo huo kwa sasa unakabiliwa na hitilafu za kisheria, jambo lililosababisha uamuzi wa kutokutengeneza video. Nandy pia ametoa shukrani kwa mashabiki waliouunga mkono wimbo huo kupitia changamoto mitandaoni, wanablogu, vyombo vya habari na vilabu vya usiku. Hitmaker huyo wa Sugar, amesisitiza kuwa licha ya changamoto hizo, mashabiki wanaweza kuendelea kufurahia “Tonge Nyama” kupitia majukwaa mengine ya kidijitali na kwenye vilabu. Msanii huyo amehitimisha waraka wake kwa kuwaahidi mashabiki wake miradi mipya, ikiwemo albamu mpya ambayo amesema ipo mbioni kuzinduliwa. Nandy, amejikuta kwenye mgogoro na kijana anayejiita Mr Tonge Nyama, ambaye amedai kuwa jina lake limetumika na Nandy bila ridhaa yake katika wimbo mpya wa msanii huyo. Mr Tonge Nyama anataka alipwe fidia ya Shilingi Milioni 200 za Kitanzania, akisema jina hilo limetumiwa kwa manufaa ya kibiashara.

Read More
 Nay wa Mitego, Billnass na Nandy Wazozana Hadharani

Nay wa Mitego, Billnass na Nandy Wazozana Hadharani

Mzozo mkali wa maneno umeibuka tena kwenye mitandao ya kijamii kati ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego, Billnass na mkewe Nandy, ukihusisha tuhuma za fitna, chuki na wivu wa maendeleo. Chanzo cha mvutano huo ni kauli ya Billnass aliyodai kuwa alipitia fitna za kutaka kufungwa kwa kesi ya wizi ambayo Nay wa Mitego alihusishwa nayo kwa kauli zisizo rasmi. Billnass, kupitia mahojiano yake na East Africa Radio, alionesha wazi kutoridhishwa na kile alichokiita hila zilizopangwa dhidi yake na watu aliowahi kuwachukulia marafiki. Baada ya maneno hayo, Nay wa Mitego hakusita kujibu kupitia sehemu ya maoni kwenye posti hiyo. Nay alimtaja Billnass kuwa ni msanii mjinga anayependa kiki bila mipaka na kumuita mwizi ambaye alistahili hata kifungo kwa tabia zake. “Acha nikupe unachotaka, wewe ni mwizi, ungeenda jela kwa tabia yako ya wizi. Nina kazi nyingi za kufanya, siwezi kushughulika na kukukandamiza wewe. Mgande Nandy ivyo ivyo ili usije ukaendelea na udokozi,” aliandika Nay wa Mitego. Kauli hiyo iliwasha moto zaidi pale mke wa Billnass, msanii Nandy, alipoamua kumjibu Nay moja kwa moja kwa hasira kali. Kupitia sehemu ya maoni, Nandy alimshutumu Nay kwa wivu na kumuita mvuta bangi, huku akidai kuwa ana chuki kutokana na kushindwa kimaisha. “Nay wa Mitego wewe cho…k…o, jina langu limeingiaje hapo? Mvuta bangi wewe! Una wivu wa maendeleo. Umejaribu kupambana umeshindwa, umebaki kuwa shabiki. Wa kuibiwa muibiwe nyie, na mnacho cha kuibiwa kwanza? Endelea na chaka zako ujikomboe, maisha upande huu mzito boob utasanda! Kithetheeee wewe, fyuu,” aliandika Nandy kwa hasira. Mashabiki kwenye mitandao wamegawanyika, baadhi wakimtetea Nay kwa kusema anasema ukweli bila uoga, huku wengine wakimtaka apunguze maneno ya matusi na wivu. Wengine wamewaomba wasanii hao warekebishe tofauti zao kwa hekima na busara badala ya kurushiana maneno hadharani. Kwa sasa, hakuna dalili za pande hizi kupoa, na mashabiki wanaendelea kufuatilia kwa karibu kuona ni nani atarushia dongo linalofuata.

Read More
 Nandy Athibitisha Albamu Mpya Kutoka Mwezi Novemba

Nandy Athibitisha Albamu Mpya Kutoka Mwezi Novemba

Malkia wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy,amefunguka kwa mashabiki wake kuhusu kusubiriwa kwa albamu yake mpya, akieleza kuwa itaachiwa rasmi mwezi Novemba mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mkali huyo wa ngoma ya “Sugar” aliwatuliza mashabiki waliokuwa wakihoji ni lini albamu hiyo itatoka, huku akifafanua kuwa kuchelewa huko kumesababishwa na sababu za msingi, ikiwa ni pamoja na kukamilisha kolabo zilizobaki na maandalizi ya mwisho ya albamu yenyewe. “Mashabiki zangu, comments zenu naziona kuhusu album. Niwaambie tu, album itatoka mwezi 11 kwa sababu za kimsingi kabisa. Tumalizie some colabo na maandalizi ya album yenyewe. Tungependa kutoa burudani kipindi tulivu na rahisi kwetu. Thank you, tuendelee ku-enjoy muziki mzuri,” aliandika Nandy. Ujumbe huo umeibua hisia mseto kutoka kwa mashabiki, baadhi wakionyesha hamu yao ya kusikia kazi mpya kutoka kwa msanii huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa mstari wa mbele katika kukuza muziki wa Tanzania kimataifa. Hadi sasa, Nandy hajataja jina rasmi la albamu hiyo, lakini vyanzo vya karibu vinaeleza kuwa itakuwa miongoni mwa kazi zake kubwa zaidi, ikiwahusisha wasanii wa ndani na wa kimataifa.

Read More
 Nandy Asikitishwa na Taarifa za Yammi, Aomba Faragha na Heshima

Nandy Asikitishwa na Taarifa za Yammi, Aomba Faragha na Heshima

Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy, amepatwa na kigugumizi kuzungumzia taarifa zilizogonga vichwa vya habari kwamba msanii wake wa zamani Yammi alifikiria kujiua kutokana na msongo wa mawazo. Katika mahojiano maalum na waandishi wa habari, Nandy amesema kuwa taarifa hizo zilimshtua na kumgusa sana, na kwamba anatamani kukutana na Yammi uso kwa uso ili wazungumze kwa kina, badala ya kuwasiliana kwa njia ya simu pekee. Hata hivyo, Nandy ametumia fursa hiyo kuwaomba waandishi wa habari kuacha kumuliza maswali kuhusu Yammi kila mara anapofanya mahojiano. Amesema hatua hiyo imekuwa ikimletea usumbufu wa kihisia na kuonekana kama chanzo cha matatizo ya hitmaker huyo wa ngoma ya “Raha”. Tamko hilo la Nandy limekuja wakati mashabiki wengi wakiendelea kutoa maoni tofauti kuhusu uhusiano wa wawili hao, huku baadhi wakihusisha tofauti zao na suala la Yammi kuwa msanii aliyekuwa chini ya lebo ya The African Princess inayomilikiwa na Nandy kabla ya kuondoka kimyakimya

Read More
 “Bora Nife Nikapumzike…” – Yamii Aandika Ujumbe wa Kushtua Instagram

“Bora Nife Nikapumzike…” – Yamii Aandika Ujumbe wa Kushtua Instagram

Msanii chipukizi wa muziki wa Bongo, Yamii, ameibua hofu mitandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kusikitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram akieleza hali ya kukata tamaa na msongo wa mawazo, kabla ya kuufuta muda mfupi baadaye. Katika ujumbe huo, Yamii alielezea hali ya kuchoka kimaisha na kusema kuwa haoni tena sababu ya kuendelea kuishi, akionesha kuwa amefikia kikomo cha uvumilivu wake. Aliomba msamaha kwa wazazi wake, ndugu na mashabiki, akionekana kubeba huzuni kubwa moyoni. Aliitaja pia msanii mwenzake Nandy, akimwomba radhi iwapo aliwahi kumkosea. “Mashabiki zangu naombeni mniombee. Msamaha kwa mama angu na baba angu na baba yangu. Mimi ndio tegemeo lakini naona siwezi kuishi tena. Nimechoka, bora nife nikapumzike. Naombeni msamaha kwa wote wote niliowahi kuwakosea. Mimi basi tena nimefika mwisho, siwezi tena, bora nikapumzike. Siwezi tena siwezi tena walahi siwezi… @officialnandy pia dada angu naomba nisamehe popote niliwahi kukukosea,” Aliandika kwa hisia kali Ujumbe huo ulisambaa kwa kasi mitandaoni, huku mashabiki na watu maarufu wakieleza kusikitishwa na hali hiyo. Wengi walihoji hali ya afya ya kiakili ya msanii huyo na kutoa wito kwa watu wa karibu naye kumsaidia haraka. Baada ya ujumbe huo kufutwa, mjadala uliendelea kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya mashabiki wakianza kampeni ya kumwombea na kumtia moyo kwa hashtag kama #PrayForYamii na #MentalHealthMatters. Wengine walitoa wito kwa wasanii wenzake, familia na mashabiki kuwa karibu naye ili kumsaidia kupitia kipindi hiki kigumu. Hadi kufikia sasa, Yamii hajatoa kauli yoyote rasmi kuhusu ujumbe huo, na haijafahamika hali yake ya sasa. Mashabiki na wadau wa burudani wanaendelea kufuatilia kwa makini

Read More
 Upendo wa Nandy kwa Billnass Wagusa Mioyo ya Mashabiki Mitandaoni

Upendo wa Nandy kwa Billnass Wagusa Mioyo ya Mashabiki Mitandaoni

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Nandy, ameonesha kwa mara nyingine ukubwa wa mapenzi yake kwa mume wake ambaye pia ni rapa, Billnass, kwa kauli ya kugusa hisia iliyoacha wengi wakitafakari juu ya upendo wa dhati. Kupitia mahojiano ya hivi karibuni, Nandy alieleza kuwa mapenzi yake kwa Billnass ni ya kipekee kiasi kwamba hawezi hata kufikiria kuendelea kuishi endapo angebaki peke yake. “Nampenda sana Billnass. Ikiwa kuna siku kifo kitatutenganisha, basi ni heri iwe mimi nitaondoka kwanza. Siwezi kuimagine maisha yangu bila yeye,” alisema kwa hisia. Kauli hiyo imezua hisia mseto mtandaoni, wengi wakiguswa na upendo wao wa dhati, huku wengine wakisifia jinsi wawili hao wanavyoendeleza ndoa yao kwa upendo na heshima, licha ya changamoto za maisha ya mastaa. Nandy na Billnass, ambao walifunga ndoa yao rasmi mwaka 2022, wamekuwa mfano wa kuigwa katika jamii, wakionesha mshikamano si tu kwenye maisha ya ndoa bali pia katika kazi zao za muziki. Mara kwa mara wamekuwa wakishirikiana kwenye miradi ya pamoja na kuonesha hadharani mapenzi yao, hali ambayo imewavutia na kuwapa matumaini mashabiki wao. Wakati ambapo ndoa nyingi za mastaa hukumbwa na drama na migogoro, wawili hawa wameendelea kuwa mfano wa kuigwa, huku wakitoa msukumo kwa wengine kuamini katika mapenzi ya kweli.

Read More
 Yammi Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuondoka The African Princess

Yammi Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Kuondoka The African Princess

Msanii wa muziki wa Bongo, Yammi, ameandika ujumbe mzito wa kihisia katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo, ikiwa ni mara ya kwanza kujitokeza hadharani tangu kuachana na lebo ya The African Princess inayoongozwa na Nandy. Kupitia mtandao wake wa Instagram, Yammi amechapisha ujumbe wa kwanza rasmi tangu aachane na lebo hiyo, akieleza hisia zake za ndani kuhusu safari yake ya muziki, changamoto alizokutana nazo, na matumaini ya mustakabali mpya. “Leo ni wakati muhimu sana kwangu, safari yangu haijawahi kuwa rahisi. Mipaka yangu imejaribiwa kwa njia ambazo sikuweza hata kufikiria… Kuna muda nilitaka kukata tamaa, lakini kupitia yote nimegundua kuwa lazima nibaki imara na kuendelea kufuata ndoto zangu.” Aliandika Katika ujumbe huo uliogusa hisia za mashabiki wengi, Yammi alieleza kuwa kila changamoto aliyopitia imemfunza kitu na kumjenga kuwa msanii mwenye maono mapya na nguvu zaidi. “Kila sehemu na kila jambo limenifundisha vitu. Alhamdulillah… here I come more stronger and determined than ever!” Alimalizia kwa hisia kali. Mashabiki wake wamemiminika kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii wakimpongeza kwa ujasiri na kumtakia mafanikio mema katika hatua yake mpya ya maisha ya muziki. Wengi wamesisitiza kuwa wanamsubiri kwa hamu na shauku kubwa, wakiamini kuwa Yammi bado ana mengi ya kuonyesha duniani. Yammi, ambaye alifahamika kupitia vibao kama “Namchukia” na “Tunayoyaweza”, alikuwa mmoja wa wasanii waliokuwa wakikuzwa chini ya lebo ya The African Princess, inayomilikiwa na Nandy. Tangu kuingia kwake kwenye tasnia ya muziki, ameonyesha uwezo mkubwa wa sauti, hisia, na utunzi wa hali ya juu. Uamuzi wake wa kuachana na lebo hiyo bado haujaelezwa kwa kina, lakini ujumbe wake wa kihisia unaashiria mwanzo mpya na ari ya kuendelea kupambana ili kufanikisha malengo yake ya kisanii.

Read More
 Nandy amtambulisha msanii mpya ndani ya lebo yake

Nandy amtambulisha msanii mpya ndani ya lebo yake

Msanii wa Bongofleva Nandy amemtambulisha msanii mpya na wa kwanza ndani ya lebo yake ya “The African Princess”, anaitwa Yammi Nandy ambaye ndiye mkurugenzi wa “The African Princess Label”, amemtaja msanii wake mpya Yammi kuwa ni binti mdogo mwenye ndoto ya kuwa msanii mkubwa na mafanikio. Aidha,Yammi amewashukuru Watanzania kwa mapokezi yao katika safari yake ya muziki ambayo ameianza rasmi Januari 19, mwaka 2023. “Asanteni sana kwa watu wote mlionipokea vizuri. Kiukweli nina mengi ya kuwashukuru ila niseme tu Nawapenda Sana  #ThreeHearts #ItsYammi”, Yammitz ametumia ukurasa wake wa Instagram kushukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata. Yammi tayari ameachia EP yake mpya iitwayo Three hearts yenye nyimbo 3 ambazo ni Namchukia, Tunapendezana na Hanipendi. Inapatikana kupitia mitandao ya kupakua na kusikiliza muziki duniani.

Read More