NANDY NA BILLNASS WAPATA MTOTO

NANDY NA BILLNASS WAPATA MTOTO

Msanii wa Bongofleva, Nandy na mume wake, Billnass wamejaliwa kupata mtoto wao wa kwanza. Akithibitisha taarifa hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Dr Cheni ambaye alikuwa MC wa harusi yao, amewapongeza wawili hao na kuwatakia afya njema pamoja na mtoto wao. “Wow Congratulations Mr and Mrs Billnass na Nandy kwa kupata mtoto Mungu awakizie awalindie kitoto Chenu. Mbarikiwe sanaa” ameandika Dr Cheni. Utakumbuka hivi karibuni Nandy alitangaza kusimamisha tamasha lake, Nandy Festival baada ya kupita kwenye mikoa miwili kati ya mitano nchini Tanzania iliyokuwepo kwenye ratiba yake

Read More
 NANDY AFUNGUKA KUJISIKIA VIBAYA RAYVANNY KUTOZWA FAINI YA SHILLINGI MILLIONI 2

NANDY AFUNGUKA KUJISIKIA VIBAYA RAYVANNY KUTOZWA FAINI YA SHILLINGI MILLIONI 2

Staa wa muziki kutoka Tanzania Nandy kwa mara ya kwanza amefunguka jinsi alivyojiskia baada ya kusikia msanii Rayvanny anatakiwa alipe kiasi cha pesa cha shilingi milioni 2 kama faini ya kutokufuata mikataba na lebo yake ya WCB. Kupitia mahojiano yake na Clouds Media Nandy amedai kuwa alifanya mawasiliano na msanii moja kwa moja na sio record label ya WCB baada ya taarifa za mwanamuziki huyo kujiengua kwenye record label hiyo, na alijiskia vibaya baada ya kusikia stori hizo japo kuwa hana uhakika nazo maana zimezuka tu mitandaoni. “Nimeziona hizo taarifa na nimejisikia vibaya maana nimeona kama mimi ndio niliosababisha hivyo lakini niliona katika instastory yake kuwa ameandika yeye ni msanii huru hivyo sikuamini kama kalipishwa maana si unajua tena stori za mitandaoni” Alisema Nandy. Utakumbuka baada ya Rayvanny kutokea kama surprise kwenye tamasha la Nandy Festival 2022 huko Songea nchini Tanzania na kuzuka stori mitandaoni kuwa lebo yake ya zamani ya WCB imemuhitaji kulipa kiasi cha pesa cha milioni 2kwa kosa la kukiuka mikataba walioingia kwa kwenda kutumbuiza katika tamasha hilo. Mbali na hayo amesema kwa sasa miongoni mwa vitu ambavyo havipendi ni pamoja na marafiki wa mume wake Billnass “Sipendi marafiki wa mume wangu na wanalijua hilo wananiambiaga mimba hiyo inakusumbua kuna muda napokea simu zake nawaambia muacheni analea mimba”

Read More
 NANDY AFUNGUKA JUU YA UJAZITO WAKE

NANDY AFUNGUKA JUU YA UJAZITO WAKE

Mwanamuziki wa Bongofleva Nandy  kwa mara ya kwanza ameweza kufunguka machache kuhusiana na ujauzito wake. Akizungumza kwenye sherehe ya ‘kitchen party’ yake wikiendi hii iliyopita Nandy amesema, mumewe mtarajiwa (Billnass) ndio wa kwanza kugundua kuwa  ana ujauzito mara baada ya kuona mabadiliko mbalimbali kama ya kitabia. Lakini pia amebainisha kitu alichokuwa akikitamani ni kupata mtoto akiwa tayari yupo ndani ya ndoa, hivyo kwa namna ilivyotokea amesema ni baraka pia. “Nilikuwa natamani kupata mtoto nikiwa tayari nipo ndani ya ndoa. Nimejaliwa nikiwa bado sijaingia kwenye ndoa lakini huyu mtoto ntaingia nae kwenye harusi na kwenye ndoa hivyo sio kitu kibaya ni baraka na wazazi wote wameridhia” – ameeleza Nandy. Ikumbukwe, Nandy na Billnass ambao kwa sasa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza hivi karibuni, wana mpango kufungua ndoa mwezi huu wa Julai.

Read More
 NANDY NA BILLNASS MBIONI KUPATA MTOTO WAO WA KWANZA.

NANDY NA BILLNASS MBIONI KUPATA MTOTO WAO WA KWANZA.

Mastaa wawili wa muziki kutoka nchini Tanzania Bill Nass na Nandy ambao wamekuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi tangu mwaka 2016 wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza pamoja. Nandy kupitia ukurasa wake wa Instagram amethibitisha hilo kwa kupost picha ya ujauzito wake na kusindikiza na caption inayosomeka “Asante Mungu kwa zawadi hii” Taarifa za Nandy kuwa na ujauzito zilikuwa za muda mrefu lakini bado hazikudhibitishwa na yeye mwenyewe tofauti na ilivyokuwa inadaiwa. Wawili hao wanatarajia kufunga ndoa mwezi huu wa saba baada ya Billnass kumvisha pete ya Uchumba Nandy siku ya Februari 20 mwaka huu

Read More
 NANDY ATOA POLE KWA MASHABIKI WALIOTAPELIWA KWA JINA LAKE

NANDY ATOA POLE KWA MASHABIKI WALIOTAPELIWA KWA JINA LAKE

Msanii wa muziki wa bongofleva Nandy ametoa pole kwa watu wote waliotapeliwa kwa jina lake kwenye mitandao ya kijamii. Nandy ametoa pole hiyo katika taarifa yake ya wazi kuwa ahusiki na wanaotangaza kuwa ana SuperMarket inayoendesha utaratibu wa kutoa ajira kwa watu wakitumia kivuli cha jina lake. Nandy ameeleza hilo kupitia Insta Story kwenye mtandao wa instagram akiongeza kuwa mbali na kuwa anaelewa changamoto ya ajira nchini tanzania lakini watu wawe makini wasitapeliwe na kwa upande wake hana mpango wa kufungua biashara ya namna hiyo.

Read More
 NANDY APOKEZWA TUZO YA GOLD PLAQUE NA MTANDAO WA YOUTUBE

NANDY APOKEZWA TUZO YA GOLD PLAQUE NA MTANDAO WA YOUTUBE

Mwanamuziki nyota wa muziki wa bongofleva , Nandy  amepewa tuzo ya Gold Plaque)na mtandao wa Youtube kwa kufikisha subscribers Milioni 1 kwenye channel yake. Tuzo hiyo imekuwa ikitolewa kwa watoa maudhui kwenye mtandao wa Youtube ambao channel zao zinafikisha wafuatiliaji (subscribers) kuanzia 100,000 na kuendelea. Nandy ambaye mwezi ujao anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake rappa Billnass, alijiunga na mtandao wa youtube Julai 5 mwaka 2016, anakuwa msanii wa pili wa kike nchini tanzania kufikisha Idadi hiyo kubwa ya wafuatiliaji kwenye mtandao huo. Anayeongoza kuwa na (subscribers) wengi kwa wasanii wakike nchini tanzania ni Zuchu ambaye anawafuatiliaji (1.97M), watatu ni Rose Muhando ( na subscribers elfu 577), wanne ni Christina Shusho na (subscribers elfu 475), na watano ni Vanessa Mdee na  (subscribers elfu 303).

Read More
 NANDY AFANIKIWA KUREJESHA INSTAGRAM YAKE BAADA YA KUDUKULIWA

NANDY AFANIKIWA KUREJESHA INSTAGRAM YAKE BAADA YA KUDUKULIWA

Akaunti ya Instagram ya mwanamuziki wa Bongofleva Nandy imerudi baada ya wadukuzi kuimiliki kwa siku kadhaa. Nandy alitangaza kupotea kwa akaunti yake ya Instagram kupitia mtandao wa kijamii wa Snapchat baada ya mashabiki kushindwa kuipata akaunti hiyo yenye zaidi ya wafuasi 6.3M. Kwa sasa akaunti hiyo imerudi hewani kama ilivyokuwa hapo awali. Ikumbukwe akaunti ya Instagram ni msaada mkubwa kwa wasanii katika kutangaza na kazi zao mbalimbali pamoja na kuwa karibu na mashabiki wao.

Read More
 NANDY ATHIBITISHA KUFUNGWA KWA AKAUNTI YAKE YA INSTAGRAM

NANDY ATHIBITISHA KUFUNGWA KWA AKAUNTI YAKE YA INSTAGRAM

Staa wa muziki wa Bongofleva Nandy amethibitisha rasmi kuwepo na shida kwenye akaunti yake rasmi ya mtandao wa Instagram ambayo ina followers milioni 6.3 Kwa mujibu wa nyanzo vya habari za burudani kutoka nchini Tanzania, akaunti ya msanii huyo imekuwa disabled (imefungwa) na Instagram wenyewe baada ya jaribio la kudukuliwa na mtu ambaye bado hajafahamika. Hata hivyo duru za kuaminika zinasema uongozi wake upo kwenye hatua za kuirejesha akaunti hiyo. Utakumbuka kando na kujitangaza, miaka ya hivi karibuni akaunti za mastaa wa muziki zimekuwa moja ya vyanzo vyao muhimu vya kipato na wale wenye followers wengi wamekuwa wakipata deals zenye hela nyingi.

Read More
 NANDY AANIKA ORODHA YA WASANII ALIOFANYA NAO COLLABO 2022

NANDY AANIKA ORODHA YA WASANII ALIOFANYA NAO COLLABO 2022

Staa wa muziki wa bongofleva Nandy ameanika mkeka wake kwa mwaka 2022 upande wa Kolabo na wasanii wa ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Kupitia ukurasa wake wa instagram hitmaker huyo wa “Yuda” ametangaza Kolabo yake na Davido pamoja na Patoranking wa Nigeria. Mbali na hao, ametangaza pia kuwa na ngoma nyingine na Sauti Sol baada ya “Kiza Kinene” iliyotoka miaka miwili iliyopita. Kolabo nyingine aliyotupasha Nandy ni ile alitusanua mwaka jana aliyosema atafanya na msanii wa singeli nchini tanzania Dulla Makabila. Hata hivyo ameachia mashabiki zake swali, aanze na collabo kati ya hizi ambazo ameziweka wazi huku pia Akisema kuwa mikakati ya kuja na tamasha lake la nandy festival 2022, hivyo Mashakibi wakae mkao wa kula mambo mazuri yanakuja kutoka kwake.

Read More