NOTI FLOW AFUNGUKA SABABU ZA KUACHANA NA KING ALAMI

NOTI FLOW AFUNGUKA SABABU ZA KUACHANA NA KING ALAMI

Rapper wa kike kutoka Kenya Noti flow amefunguka sababu za kuachana na mpenzi wake King alami ikiwa ni wiki kadhaa zimepita tangu amzawadi na gari mpya. Kupitia kikao cha maswali na majibu pamoja na mashabiki zake Noti Flow amesema alimvumania King Alami mchana kweupe na mwanaume mzee eneo la runda wakipigana mabusu makali kitu ambacho kilimkasirisha ns kuchukua maamuzi magumu ya kuvunja uhusiano wao. Wawili hao ambao wanashiriki mapenzi ya jinsia moja wamekuwa wakichumbiana tangu mwaka wa 2021 ambapo walienda mbali zaidi na kuchora tattoo za majina yao kwenye miili yao.

Read More
 ERIC OMONDI AMVUA NGUO NOTI FLOW KWA KUMVUNJIA HESHIMA

ERIC OMONDI AMVUA NGUO NOTI FLOW KWA KUMVUNJIA HESHIMA

Mchekeshaji maarufu nchini Eric Omondi ameingia kwenye headlines mara baada ya kutupia maneno makali mtandaoni na rapa Noti Flow kuhusu magari waliyowanunulia wapenzi wao hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Omondi amemtaka Noti Flow kutofuatilia maisha yake ya ndani huku akitishia kumfundisha adabu pamoja na mpenzi wake King Alami. “Ambie huyu CHOKORA Asiwahi Ita jina yangu tena!!!!  Ama nitamshika na huyu demu wake NIWAKULE mpaka wakue straight. IDIOT!!!!” Ameandika Omondi. Post hiyo haikupokelewa vyema na Noti Flow ambaye alishuka kwenye uwanja wa comment ya post hiyo na kumchana tena Eric Omondi akisema mchekeshaji huyo amemkasirikia kwa sababu gari lake ni la kukodisha. “He’s mad cz it’s car hire post logbook bruh. Chokora ni wewe na car hire zako. Clout chaser.” Ameandika Noti Flow. Ikumbukwe purukushani kati ya Eric Omondi na Noti Flow ilianza mara baada ya mrembo huyo kumtaka Omondi aoneshe stakabadhi za gari aliyomnunulia mpenzi wake juzi kati ambapo alienda mbali na kujigamba kuwa tangu amnunulie gari mpenzi wake king alami mastaa wengi kutoka kenya wameanza kumuiga kwa kukodisha magari wakati hana lolote katika maisha.

Read More
 NOTI FLOW AFUNGUKA JUU YA UTATA UNAOZINGIRA WIMBO WAKE WA “FOTO MOTO”

NOTI FLOW AFUNGUKA JUU YA UTATA UNAOZINGIRA WIMBO WAKE WA “FOTO MOTO”

Rapper wa Kike kutoka nchini Kenya Noti Flow amefunguka na kudai kwamba hajawahi faidi na mirabaha ya wimbo wake uitwao Foto Moto ambao alimshirikisha Benzema. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Noti Flow amesema licha ya kuwekeza pesa nyingi kuandaa wimbo wa Foto Moto na hata kuchezwa kwenye vituo vya redio na runinga nchini hajawahi lipwa hata senti moja kutoka kwenye wimbo huo ambao ulipata umaarufu mkubwa nchini mwaka wa 2020. Mrembo huyo ameilaumu kampuni ya ngoma iliyokuwa ikisimamia kazi zake kwenye mtandao wa youtube kwa kitendo cha kusalia kimya kuhusu hakimiliki ya wimbo wa Foto Moto baada ya mtumiaji mmoja wa youtube kujitokeza na kudai kuwa noti flow na benzema walimuibia mdundo wake na kisha wakaitumia kwenye wimbo wa Foto Moto. Utakumbuka wimbo wa Foto Moto wake Noti Flow akiwa amemshirikisha Benzema ilitoka mwaka wa 2020 na video yake kwenye mtandao wa youtube ina zaidi ya views millioni 4.5.

Read More
 NOTI FLOW AMPA SOMO MWANAUME ALIYEMUOMBA PENZI KWA SHILLINGI LAKI 2 ZA KENYA

NOTI FLOW AMPA SOMO MWANAUME ALIYEMUOMBA PENZI KWA SHILLINGI LAKI 2 ZA KENYA

Female rapper kutoka Kenya Noti Flow ameonekana kutopendezwa na kitendo cha mwanaume mmoja aliyezama kwenye dm yake na kumuomba penzi kwa Shillingi laki mbili za Kenya. Kupitia instagram page yake Noti Flow ameshare screen short ya ujumbe aliyotumiwa na mwanaume huyo huku akimpa somo kuwa hana shida ya pesa ikizingatiwa kuwa huwa anatumia kati ya shilling laki 5 hadi million moja kwa wiki. Hitmaker huyo wa “Foto Moto” ameenda mbali zaidi na kusema kwamba hatokubali kununuliwa kwa shilling laki 2 huku akiwaonya wanaume wanaomzimia kimapenzi kukoma kumtumia jumbe za mapenzi kwenye mitandao yake ya kijamii kwani ana furaha kwenye mahusiano yake na mrembo King Alami. Utakumbuka Noti Flow ni moja kati ya wasanii wenye utata nchini kutokana na maamuzi yake ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja na mrembo mwenzake King Alami.

Read More
 NOTI FLOW AMTOLEA UVIVU MUSTAFA

NOTI FLOW AMTOLEA UVIVU MUSTAFA

Siku chache baada ya staa wa muziki nchini Colonel Mustafa kudai kwamba alivunja uhusiano wake wa na Noti Flow mara baada ya mrembo huyo kumuibia akaunti yake ya instagram, sasa Noti Flow amejitokeza na kukanusha madai hayo. Akiwa kwenye moja ya interview Noti Flow amesema madai hayo haya msingi wowote kwani ni yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumuacha Mustafa baada ya msanii huyo kumvunjia heshima kwa kumsaliti. Hitmaker huyo wa Foto Moto ameenda mbali zaidi na kumtolea uvivu mustafa kwa kusema kwamba msanii huyo hajui kuandika kiingereza kwa ufasaha na hata wafuasi ambao aliwapata instagram ni kwa sababu ya juhudi zake. Hata hivyo amesema kama kweli Colonel Mustafa anahisi ana ushawishi mkubwa nchini afungue akaunti nyingine ya mtandao wa instagram aone kama atapata wafuasi wengi. Ikumbukwe kipindi cha nyuma Noti  Flow alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa Colonel Mustafa lakini mahusiano yao yalikuja yakavunjika kwa kile kilichodaiwa kuwa mrembo huyo alikuwa msumbufu.

Read More