NYOTA NDOGO AMSHAMBULIA MWANABLOGU ALIYEMZUSHIA TAARIFA ZA UONGO

NYOTA NDOGO AMSHAMBULIA MWANABLOGU ALIYEMZUSHIA TAARIFA ZA UONGO

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Nyota Ndogo amechukizwa na kitendo cha mwanablogu mmoja  kuchapisha taarifa za uongo dhidi yake. Mwanablogu huyo alichapisha taarifa akisema kwamba Nyota Ndogo  alidai kwenye moja ya interview kuwa asipoimba jina lake litazidi kuzungumziwa nchini ikizangatiwa kuwa ni msanii mkongwe ambaye ameacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini. Sasa kupitia instagram page yake Nyota Ndogo ameibuka na kukanusha madai yaliyoibuliwa na blogger huyo kwa kusema kwamba hajawahi jigamba kuwa yeye ni bora kuliko msanii yeyote kwani hapendi kabisa kujisifu kwenye maisha yake. Hitmaker huyo wa “Watu na Viatu” amesema kama watu wamechoshwa na muziki wake wa sasa ni afadhali waanze kusapoti biashara yake ya vyakula ya Nyota Ndogo jikoni ambayo makao yake yapo mjini voi, kaunti ya Taita Taveta.

Read More
 NYOTA NDOGO AELEZA ANAVYOITWA SURA MBAYA NA WANAUME MITANDAONI

NYOTA NDOGO AELEZA ANAVYOITWA SURA MBAYA NA WANAUME MITANDAONI

Msanii mkongwe kwenye muziki  nchini Nyota Ndogo, amefunguka namna ambavyo amekua akishambuliwa kwa maneno ya kejeli mtandaoni na baadhi ya wanaume kwa kumuita sura mbaya. Nyota Ndogo kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka namna amekuwa akipokea kejeli haswa kutoka kwa wanaume, baada ya kufikisha umri wa miaka 40 mwaka huu. “Sasa kuitwa mazee na sura Mbaya nishazoea munaweza mukatafuta maneno makali mengine yakuniita na wengi wao uwa wanaume mybe I look much better at 40 kushinda your galfriend mwenye ako 25.hatukatai uzee uzee ni sunna ni hatizeeki kizembe hatujitupi wall yangu ikikusinya ni block” amesema Nyota Ndogo. Hata hivyo Hitmaker huyo wa “Watu na Viatu” amesema kwamba amezoea kuitwa sura mbaya na hivyo wanaomshambulia wanapaswa kutafuta maneno mengine ya kumuita huku akieleza kwamba yeye ni mrembo kuliko wapenzi wao wa miaka 25.

Read More
 NYOTA NDOGO AINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA JOY MILLERS LIMITED.

NYOTA NDOGO AINGIA UBIA WA KUFANYA KAZI NA KAMPUNI YA JOY MILLERS LIMITED.

Staa wa muziki nchini Nyota Ndogo amelamba dili nono la kuwa balozi wa unga wa ugali wa Raha Premium. Nyota Ndogo ametengaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram huku akieleza kuwa ana furaha kujiunga na familia ya Raha Premium. Lakini pia ameishikuru uongozi wa kampuni ya Joy Miller Limited kwa kutambua nguvu yake na kuhamua kumpatia dili hilo ambalo litamjengea heshima. Nyota Ndogo sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Raha Premium kwa mashabiki zake kupitia mitandao ya kijamii kwa lengo la kuongeza mauzo ya unga hiyo ya ugali. Hitmaker huyo wa “Watu na Viatu” anajunga na msanii Bahati pamoja mke wake Diana Marua ambao pia waliingia ubia wa kufanya kazi na kampuni ya Joy millers limited mwezi Agosti mwaka huu. Ikumbukwe nyota ndogo ni mmoja kati ya wasaani ambao wamewekeza kwenye biashara kuuza vyakula na amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kutangaza mgahawa wake ambao ameupa jina la  Nyota Ndogo jikoni.

Read More