Kimeumana! Diss Track Yawafanya Marapa Octopizzo na Kayvo Washikane Mashati

Kimeumana! Diss Track Yawafanya Marapa Octopizzo na Kayvo Washikane Mashati

Rap ya Kenya imewaka moto tena baada ya marapa Octopizzo na Kayvo KForce kujipata wakirushiana maneno makali kiasi cha karibu kuzichapa kwa makonde. Chanzo cha mvutano huu kilikuwa diss track ya Kayvo, iliyolenga moja kwa moja kuhoji uhalali wa Octopizzo katika kiwanda cha hip hop. Baada ya Diss hiyo, wawili hao walikutana uso kwa uso, hali ikawa tete. Octopizzo alionekana kumwonya Kayvo akome, akimtaka aache kuingilia maisha yake ya muziki kwa kuachia “diss tracks za kijinga” na badala yake ajikite kuboresha sanaa yake. Kayvo hakusita kujibu, akimtuhumu Octopizzo kwa kudhoofisha jina lake. Alidai kuwa kauli za rapa huyo kwenye Iko Nini Podcast, kwamba hatoki Kibera, zilimchafua hadharani. Octopizzo naye hakusalia kimya; alirudisha moto kwa kudai Kayvo amekuwa akijipendekeza kama mwana wa Kibera ilhali hajakulia wala kuishi humo. Kayvo alipuuza hoja hizo akisisitiza kwamba hazina mashiko. Kauli hizo zilimkera zaidi Octopizzo, ambaye alimtaka Kayvo aonyeshe makazi yake Kibera kama anadai ni mwenyeji. Aidha, alimshutumu kwa kutumia jina la Kibera kwa manufaa binafsi. Mzozo huo uliwafikisha pabaya kiasi cha kushikana mashati na kuanza kurushiana makonde, lakini hali hiyo ilidhibitiwa na watu wa karibu waliowaingilia kati. Kwa kumbukumbu, wawili hao waliwahi kuwa marafiki na hata kuachia wimbo wa pamoja uitwao “Voice of Kibera” mwaka 2011, kabla ya nyota ya Octopizzo kung’aa na kupelekea tofauti za kimawazo na kimaisha.

Read More
 Octopizzo Awataka Wakenya Wapunguze Hasira kwa George Ruto

Octopizzo Awataka Wakenya Wapunguze Hasira kwa George Ruto

Msanii maarufu wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Octopizzo, amewataka Wakenya wapunguze hasira zao dhidi ya George Ruto, mwanawe Rais William Ruto, kufuatia uzinduzi wa matatu maarufu inayofahamika kama Nganya mwishoni mwa wiki hii. Kupitia mitandao ya kijamii, Octopizzo amewakosoa Wakenya wanaomshambulia George kutokana na hali ya kiuchumi inayokumba taifa, akisisitiza kuwa “dhambi za mzee si za mtoi.” akimaanisha kuwa makosa au historia ya mzazi haifai kuhamishiwa kwa watoto wao. “Dhambi za mzee si za mtoi,” aliandika msanii huyo, akisisitiza kuwa George ana haki ya kuishi maisha anayopenda bila kulaumiwa kwa sababu ya hadhi ya baba yake Octopizzo pia ameelezea kuwa ni jambo la kawaida kwa mtoto wa bilionea kuishi maisha ya kifahari, akionekana kushangazwa na jinsi baadhi ya Wakenya wanavyomshinikiza George kutafuta kazi ilhali baba yake ana uwezo mkubwa wa kifedha.  “Babake ni billionaire alafu mnataka George afanye kazi gani? Aanze kuuza mandazi?” aliandika kwa kejeli, akilenga kuonyesha kuwa ni kawaida kwa watoto wa viongozi matajiri kuwa na maisha ya kifahari. Uzinduzi wa Nganya ya George Ruto ulifanyika kwa mbwembwe kubwa jijini Nairobi, huku baadhi ya Wakenya wakilalamikia matumizi ya kifahari wakati taifa linapitia changamoto za kiuchumi.

Read More
 Siasa si Majina, ni Maendeleo – Ujumbe wa Octopizzo kwa Wakenya

Siasa si Majina, ni Maendeleo – Ujumbe wa Octopizzo kwa Wakenya

Msanii maarufu wa muziki wa hip hop nchini Kenya, Octopizzo, ameibua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii baada ya kuchapisha ujumbe mzito katika mtandao wa X (zamani Twitter), akiwataka Wakenya wawe makini na hali ya kisiasa nchini. Kupitia ujumbe huo, Octopizzo amewataka raia kukataa kile alichokiita usahaulifu wa kisiasa, akieleza kuwa upinzani unaojitokeza hivi sasa si mpya kwa kweli, bali unaundwa na viongozi waliowahi kushika nyadhifa serikalini kwa muda mrefu bila kuleta maendeleo ya maana kwa taifa. “Wakenya hawapaswi kusahau historia ya kisiasa. Huu unaoitwa upinzani mpya ni mkusanyiko wa viongozi waliokataliwa, au waliodumu serikalini kwa zaidi ya miaka ishirini bila kuwa na mafanikio yoyote ya kushikika. Wanaonekana kutamani madaraka, si mageuzi ya kweli,” ameandika msanii huyo. Octopizzo ameendelea kwa kutoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu na kutanguliza maendeleo ya taifa badala ya kushabikia watu binafsi au vyama. “Tuwe waangalifu na tujitolee kwa maendeleo, si kwa kushabikia watu au majina. Kama taifa, tunastahili uongozi unaowajali wananchi si wakati wa uchaguzi pekee, bali kila siku.” Ameongeza kwa msisitizo. Ujumbe huu umepokelewa kwa hisia tofauti mitandaoni, baadhi ya wananchi wakimsifu kwa kutoa kauli yenye busara na ujasiri,huku wengine wakitumia fursa hiyo kujiuliza maswali kuhusu mwelekeo wa kisiasa nchini. Hii si mara ya kwanza kwa Octopizzo kutoa maoni kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa, kwani amekuwa akitumia majukwaa yake ya mitandao ya kijamii kuhamasisha umma kuhusu haki, uwajibikaji, na maendeleo ya vijana nchini.

Read More
 Octopizzo awaasa wasanii wakubwa Afrika Mashariki kuwasaidia watu wenye uhitaji kwenye jamii

Octopizzo awaasa wasanii wakubwa Afrika Mashariki kuwasaidia watu wenye uhitaji kwenye jamii

Rapa Octopizzo amewahimiza wasanii wakubwa Afrika Mashariki kuhakikisha wanaisaidia jamii kwa kuwawezesha watu wenye uhitaji. Akizungumza katika mahojiano na Wasafi, Octo ameeleza kuwa hapendi kila kitu kuhusu msanii Diamond ila anafarajika na namna ambavyo ametengeneza fursa za ajira kwa vijana. Octopizzo pia amewatolea uvivu wasanii ambao hutumia kiki kutangaza muziki wao kwa kusema kwamba wana njaa ya maskini. Rapa huyo amewataka wasanii nchini Kenya kuzingatia suala la kutayarisha muziki mzuri badala ya kiki ambazo hazina msingi wowote. Hata hivyo amesema kwamba haihitaji kuimba Kiingereza ili utoboe kimataifa, kwani kuna ngoma nyingi sana zimekuwa kubwa dunia nzima na hazijaimbwa kwa Kiingereza.

Read More
 Rapa kutoka Kenya Octopizzo aachia rasmi album yake mpya

Rapa kutoka Kenya Octopizzo aachia rasmi album yake mpya

Rapa kutoka nchini Kenya Octopizzo ameachia rasmi album yake mpya inayokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. Album hiyo inayokwenda kwa jina la Lamu Nights  ina jumla ya ngoma 10 za moto ambazo amewashirikisha wakali kama Wendy Kay, Jivu, Tito Wagithomo, Coaster Ojwang, Okella Max na Burklyn Boyz. Album hiyo ina nyimbo kama No Signal, Bad Vibes, Want It, Vacation, Moaning, Achupa na na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa Youtube. Lamu Nights ni Album ya saba kwa mtu mzima Octipozzo, baada ya Fuego iliyotoka mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 12 ya moto.

Read More
 OCTOPIZZO AMTAKA RUTO AHALALISHE BANGI

OCTOPIZZO AMTAKA RUTO AHALALISHE BANGI

Msanii wa Hip Hop nchini Kenya, Octopizzo amemtaka Rais mteule William Ruto kuihalalisha bangi pindi tu atakapokula kiapo cha kuingia ofisini kama Rais wa tano wa Kenya. Katika video ambayo imesambazwa mitandaoni, Octopizzo anamuelezea Ruto kwamba hata kama ataona kuhalalisha bangi ni jambo gumu basi aifanye isiwe kama ni hatia kwa mtu anayepatikana naye bali liwe tu ni jambo la kawaida. “Najua wewe ni mkristo na kwa hiyo hili gumzo huenda litakuwa gumu kidogo kwako lakini unajua bangi ni moja ya dawa ambazo ni takatifu zaidi duniani. Na amabcho nakuomba hata si kuhalalisha matumizi yake bali ni kuiweka bangi isiwe kama hatia kwa mtu anayepatikana nayo,” alisema Octopizzo. “Juzi nilikuona ulikutana na seneta wa Delaware, huko mtu anaruhusiwa kutembea na bangi gramu 3 kwa kujivinjari tu ilmradi mtu ako na miaka 21. Hii ni biashara ya mabilioni na tunajua kuna watu serikalini wenye wanafanya biashara hiyo,” Staa huyo alisema.

Read More
 OCTOPIZZO AWEKA WAZI VIGEZO VYA KUFANYA NAYE KOLABO

OCTOPIZZO AWEKA WAZI VIGEZO VYA KUFANYA NAYE KOLABO

Rapa Octopizzo  amefunguka kuhusiana na swala la yeye kutofanya kolabo na wasanii wenzake hususani wa nje. Kupitia Mambo Mseto ya Radio Citizen Octopizzo amesema hatokuja kufanya kolabo na mtu ambaye ana faida kwake kwa kuwa anafanya muziki kama biashara. Haikushia hapo ameenda mbali zaidi na kusema kwamba ikitokea amefanya kolabo na msanii yeyote ni lazima awe na Master Recording za muziki wake kwani hapendi suala la kufaidisha lebo za muziki. Mbali na hayo ameonyosha maelezo kuhusu kufanya wimbo wa pamoja na Khaligraph Jones kwa kusema watafanya kazi na rapa huyo muda sahihi ukifika kwa kuwa hawana ugomvi kama walimwengu wanavyodai mtandaoni.

Read More
 OCTOPIZZO AKIRI KUCHOSHWA NA WANAOMKOSOA MTANDAONI

OCTOPIZZO AKIRI KUCHOSHWA NA WANAOMKOSOA MTANDAONI

Rapa Octopizzo amefunguka sababu za kutowajibu wanaomkosoa kwenye mitandao ya kijamii tofauti na ilivyokuwa awali. Akipiga stori na presenter Ali Octopizzo amesema aliamua kuweka kando kila kitu kwa ajili ya afya yake ya akili lakini pia kujihusisha na mambo ambayo yataamuingizia hela kwani alikuja kugundua kuwa alikuwa anapoteza muda wake mwingi kupishana na watu wasiokuwa na malengo maishani. Octopizzo ambaye anafanya vizuri na ngoma mpya “Tom Mboya” amesema kwamba anapenda sana watu wanapomkosoa mtandaoni kwa kuwa inampa changamoto ya kurekebisha baadhi ya vitu ambavyo haviendi sawa kwenye muziki wake. Utakumbuka Octopizzo amekuwa kwenye tour yake tangu mwezi Machi Mwaka huu ambapo amekuwa akihubiri amani na kuwahamasisha vijana wajitokeze kwa wingi kuwachagua viongozi watakaowafaa kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Read More
 TECNO YAMTAMBULISHA OCTOPIZZO KAMA BALOZI WA SIMU ZAO ZA SPARK 9 SERIES

TECNO YAMTAMBULISHA OCTOPIZZO KAMA BALOZI WA SIMU ZAO ZA SPARK 9 SERIES

Rapa Octopizzo ametangazwa kuwa balozi wa simu mpya ya Mkononi kutoka kampuni ya Tecno Kenya inayokwenda  kwa jina la Tecno Spark 9 Series itakayouzwa katika maduka yote ya simu nchini. Akizungumza na waandishi habari leo jijini Nairobi, Mkurugenzi wa Techno, Peter Shi amesema kuwa wanatarajia  jamii itafaidika kwa kupata elimu kuhusu bidhaa za kampuni hiyo kupitia kwa balozi Octopizzo kwani wameamua kuileta simu ya Techno Spark 9 series  ili waweze kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kumiliki simu janja . Kwa upande wake Rapa Octopizzo ameishukuru kampuni Techno kwa kumwamini na kutambua kuwa ana vigezo stahili kuwa balozi wao na kuahidi kuwa hatowaangusha katika kuitangaza kampuni hiyo sambamba na bidhaa zake zinazozalishwa na kampuni hiyo ambayo utengeneza simu, Kompyuta na vifaa vingine vya teknolojia Octopizzo sasa atatakiwa kutangaza bidhaa za Techno Spark 9 Series kwa mashabiki zake kupitia mitandao yake ya kijamii kwa lengo la kuiongezea kampuni hiyo mauzo.

Read More
 OCTOPIZZO ADOKEZO UJIO WA KOLABO NA NYASHINSKI, ZIARA YAKE YA KIMUZI PAMOJA NA ALBUM MPYA

OCTOPIZZO ADOKEZO UJIO WA KOLABO NA NYASHINSKI, ZIARA YAKE YA KIMUZI PAMOJA NA ALBUM MPYA

Mkali wa muziki wa Hiphop nchini Octopizzo ametangaza ujio wa wimbo wake mpya aliyomshirikisha na lejendari wa muziki Nyashinski Octopizzo amethibitisha taarifa hiyo njema kwa mashabiki zake Kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kushare picha akiwa na  Nyashinski  ambapo  amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea collabo yao ambayo kwa mujibu wake itakuwa moto wa kuotea mbali. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Motivation” hajeweka wazi ni lini hasa ngoma hiyo itaingia sokoni ila itakuwa wimbo wake wa kwanza kufanya na  Nyashinski tangu aanze safari yake ya muziki. Mbali na hayo, Octopizzo ametangaza kuja na ziara ya kimuziki iitwayo live music tour samba na kuachia album mpya ambayo hajataja Siku Rasmi ya kuachia Album hiyo lakini ameweka baadhi ya picha zikimuonesha akiwa kwenye maandalizi ya Album yake Mpya. Hii  inaenda kuwa Album ya 7 kwa mtu mzima Octopizzo, baada ya  Fuego”  iliyotoka mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 12 ya moto.

Read More