PALLASO KUENDELEA NA SHOWS ZAKE LICHA YA KUUMIA GOTI

PALLASO KUENDELEA NA SHOWS ZAKE LICHA YA KUUMIA GOTI

Staa wa muziki kutoka nchini Uganda Pallaso ametusanua kuwa ataendelea na shows zake kama ilivyoratibiwa baada ya kupata jeraha la goti kwenye moja ya perfomance yake katika hoteli ya La Grande viungani mwa jiji la Kampala. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” ametumia mitandao yake ya kijamii kuwafahamisha mashabiki wake na wale waliokuwa wamempa shows hapo awali kwamba atumbuiza akiwa ameketi jukwaani hadi pale atakapopata nafuu licha ya kuumia goti. “Niliumia goti kwenye jukwaa lililolegea katika Hoteli ya La Grande wakati nikitumbuiza jana usiku. Ilinibidi nifanye maonyesho yangu yote nikiwa nimekaa kwenye kiti, maumivu hayavumiliki lakini nitakuwa sawa. Nikiendelea kutafuta matibabu zaidi, nataka nifawahamishe kuwa shoo zote nilizopaswa kutumbuiza hazitaahirishwa. Lakini itabidi umnisamehe kwa kutumbuiza kwenye kiti hadi nitakapopata nafuu,” aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii. Ikumbukwe kwamba siku chache zilizopita, wadau pamoja na mashabiki wa muziki wake walimuashia moto kwa kususia baadhi ya shows zake licha ya mapromota kumlipa pesa zake zote.

Read More
 PALLASO AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUSUSIA ONESHO LAKE HUKO KYOTERA, UGANDA

PALLASO AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUSUSIA ONESHO LAKE HUKO KYOTERA, UGANDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Pallaso ameingia tena kwenye headlines mara baada ya kususia moja ya onesho lake huko Kyotera, masaka wikiendi hii iliyopita. Duru za kuaminika znasema mashabiki walimsubiri pallaso kwa takriban masaa matatu lakini msanii huyo hakutokea kwenye performance yake, jambo lilowafanya mashabiki kuzua vurugu na kuaharibu kila kitu kwenye ukumbi wa burudani na kuacha mapromota wakikadiria hasara ya mamilioni ya pesa. Juhudi za msanii Sheebah Karungi kuwatuliza mashabiki ziliambulia patupu kwani walionekana wenye hasira zaidi wakiwataka waliondaa onesho hilo kuwaregeshea pesa zao kwa kushindwa kutimiza ahadi ya kumleta pallaso jukwaani awape burudani. Hii ni mara ya pili kwa pallaso kususia show, kwani mapema mwezi huu alijipata pabaya tena baada ya kushindwa kutokea kwenye moja ya show yake huko masaka, kitendo kilichowakera mapromota na mashabiki, na kama njia ya kuwaomba mashabiki zake msamaha alihamua kufagia mji wa masaka. Utakumbuka Pallaso amekuwa akiendeleza ziara yake iitwayo Golden tour kwa kipindi cha mwezi mmoja ambapo amezunguka kwenye miji zaidi ya 25 nchini uganda kuw

Read More
 PALLASO AWACHANA MAPROMOTA WANAOMLAMU ANATOZA PESA NYINGI KWA SHOWS ZA NDANI

PALLASO AWACHANA MAPROMOTA WANAOMLAMU ANATOZA PESA NYINGI KWA SHOWS ZA NDANI

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Pallaso amewachana mapromota wanaotilia shaka kiasi cha pesa anacholipisha kwa shows za ndani ya nchini. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Pallaso amewataka mapromota ambao wanasema hastahili kulipwa shillingi laki 2 za Kenya kwa show moja kutompa michongo ya shows zao kwani hana muda wa kuwashawishi kutokana ukubwa wa brand yake ya muziki. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” amejinasibu kwa kusema kwamba hakuna show hata moja ambayo imefanya vibaya tangu mapromota waanze kumpa shows huku akisisitiza kuwa anastahili kulipwa shillingi laki 2 kwa show moja kwani amewekeza pesa nyingi kujenga chapa yake kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda.

Read More
 PALLASO ADOKEZA MPANGO WA KUZINDUA KAMPUNI ITAKAYOSHUGHULIKA NA MATAMASHA YA MUZIKI

PALLASO ADOKEZA MPANGO WA KUZINDUA KAMPUNI ITAKAYOSHUGHULIKA NA MATAMASHA YA MUZIKI

Staa wa muziki nchini Uganda Pallaso amedokeza mpango wa kuja na kampuni itakayoshughulika na matamasha ya muziki. Katika mahojiano yake hivi karibuni Pallaso amesema amechukua hatua hiyo kama njia ya kuwaondoa madalali na mapromota ambao wamekuwa wakipora pesa nyingi kupitia kazi za muziki huku wakimlipa malipo duni. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” amesema kampuni hiyo pia itamsaidia kutanua wigo wa muziki wake uweze kuwafikia watu wengi duniani. Pallaso ni moja kati wasanii ghali na waliopata shows nyingi nchini Uganda ambapo inadaiwa anatoza kati ya shillingi laki 3  na 6 za Kenya kwa shows za ndani ya nchi. Utakumbuka Pallaso anajianda kuanza ziara yake ya kimuziki iitwayo Golden tour Machi 6 mwaka huu tour ambayo itazunguka zaidi ya miji 25 nchini kwa kipindi cha mwezi mmoja

Read More
 PROMOTA ABTEX ATISHIA KUMALIZA CAREER YA PALLASO BAADA YA MSANII HUYO KUSUSIA PERFORMANCE YAKE

PROMOTA ABTEX ATISHIA KUMALIZA CAREER YA PALLASO BAADA YA MSANII HUYO KUSUSIA PERFORMANCE YAKE

Promota wa muziki nchini Uganda Abtex amesikitishwa na kitendo cha mwanamuziki Pallaso kutofika kwa wakati kwenye moja ya show aliyopewa nafasi kuperform huko Masaka. Kwenye mkao na wanahabari Abtex amesema kitendo hicho sio cha kingwana na inaonesha ni jinsi gani pallaso hawashimu mashabiki zake ikizingatiwa kuwa walikuwa tayari wameshalipa pesa zao kwa ajili ya kumuona hitmaker huyo wa  ngoma ya “Malamu” akifanya performance yake. Hata hivyo Abtex ametishia kuwashawishi mapromota wenzake nchini Uganda kususia kumpa pallaso shows kwenye matamasha yao ya muziki kwani msanii huyo anakwenda kinyume na mikataba yao maelewano. Utakumbuka juzi kati pallaso alishinda kufika kwa wakati kwenye moja ya show huko masaka nchini uganda jambo ambalo lililazimu msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii kuomba radhi kwa hatua yake hiyo baada ya mashabiki kuzua vurugu alipofika stejini kama amechelewa.

Read More
 PALLASO: HUU NI MWAKA WANGU WA KUVUNA NILICHOKIPANDA KUPITIA MUZIKI WANGU

PALLASO: HUU NI MWAKA WANGU WA KUVUNA NILICHOKIPANDA KUPITIA MUZIKI WANGU

Nyota wa muziki nchini Uganda Pallaso ameibuka na kujigamba kuwa mwaka huu anaenda kuvuna pesa nyingi kupitia muziki ambao kwa mujibu wake ameufanyia uwekezaji mkubwa. Akizungumza baada ya kutumbuiza kwenye private party moja viungani mwa jijini la Kampala Bosi huyo wa lebo ya Team Good music amesema kuwa huu ni mwaka wake  kuanza kuingiza kipato kupitia bidii yake kwenye kazi zake za muziki. Hitmaker huyo wa “Nalonda Nemala” anasubiri kwa hamu kuanza kuingiza pesa atakapoanza kutumbuiza kwenye matamasha ya muziki pindi tu uchumi wa nchi ya Uganda itakapofunguliwa Januari 24 mwaka huu wa 2022 baada ya kufungwa kwa takriban miaka miwili kutokana na msala wa Korona. Utakumbuka mwaka wa 2019 nyota ya pallaso ilianza kungaa kwenye muziki lakini kutokana na janga la korona hakuweza kuingiza pesa nyingi kupitia muziki wake baada ya matamasha kufungwa kama njia ya kuzuia msambao wa virusi vya corona.

Read More