Pastor Kanyari Amtaka Tash Kuheshimu Matakwa ya Mama Betty Bayo katika Mgogoro wa Mali

Pastor Kanyari Amtaka Tash Kuheshimu Matakwa ya Mama Betty Bayo katika Mgogoro wa Mali

Mvutano kuhusu mali ya marehemu Betty Bayo umechukua mkondo mpya baada ya mchungaji Victor Kanyari kutoa wito kwa aliyekuwa mume wa msanii huyo, Tash, kusikiliza na kuheshimu matakwa ya mama mzazi wa Betty katika suala hilo nyeti. Kanyari amesema kuwa mama huyo bado ana machungu makubwa ya kumpoteza mwanawe, na kwamba kupuuza hisia zake kunaweza kumletea Tash madhara ya kiroho, akisisitiza kuwa laana inaweza kumpata asipoheshimu mzazi aliye katika majonzi. Mvutano huo uliibuka baada ya mama mzazi wa Betty kudai kuwa mali ya marehemu iliandikishwa kwa jina lake, na kwamba Tash asijaribu kuingia kwenye mchakato wa kudai haki au kusimamia urithi bila ridhaa yake. Mama huyo pia ameonekana kuwa thabiti kwenye msimamo wake, akieleza kuwa yuko tayari kufungua shauri rasmi endapo kutakuwa na upinzani wowote. Hadi sasa, pande zote hazijatoa tamko la pamoja, huku hali ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki na familia kufahamu mwelekeo wa mgogoro huu unaohusisha mali, ustawi wa watoto, na hisia nzito za kuondokewa na mpendwa.

Read More
 Prophet Kanyari Aomba Msamaha kwa Marehemu Betty Bayo Katika Ibada ya Mazishi

Prophet Kanyari Aomba Msamaha kwa Marehemu Betty Bayo Katika Ibada ya Mazishi

Mhubiri Victor Kanyari ameibua hisia nzito leo wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Betty Bayo, akitoa hotuba ya kuonyesha masikitiko yake pamoja na kumwomba msamaha kwa yaliyowahi kutokea kati yao wakati wa uhai wake. Kanyari ametumia muda huo muhimu kueleza kuwa drama na changamoto zilizozikumba maisha yao ya awali zilimfanya Betty kupitia wakati mgumu, jambo ambalo leo analiona kama doa ambalo halikupaswa kumwangukia. Amemtaja marehemu Betty kama mwanamke mchapakazi, mwenye moyo wa kusamehe, mama mwenye upendo na rafiki wa kweli ambaye aliwahi kuwa sehemu muhimu ya maisha yake. Katika hotuba yake, amesisitiza kwamba licha ya changamoto walizowahi kushuhudia kwa pamoja, Betty alibaki kuwa mtu wa amani, hekima na aliyejitolea kuwalea watoto na kuendeleza huduma yake ya muziki wa injili bila kuyumbishwa. Mazishi ya marehemu Betty Bayo yalifanyika leo katika eneo la Mugumo Estate, Kaunti ya Kiambu, ambako familia na marafiki wa karibu walimpumzisha kwenye nyumba yake ya milele baada ya kutoa heshima zao za mwisho.

Read More
 Pastor Kanyari Akana Kufahamishwa Kuhusu Ugonjwa wa Betty Bayo

Pastor Kanyari Akana Kufahamishwa Kuhusu Ugonjwa wa Betty Bayo

Mchungaji Victor Kanyari amekanusha madai kwamba aliwahi kufahamishwa kuhusu ugonjwa wa mkewe wa zamani, marehemu Betty Bayo, kabla ya kifo chake. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, amesema taarifa za kifo cha Betty zilimuumiza sana, akieleza kuwa kama angeambiwa mapema kuhusu hali yake, angejitahidi kumsaidia kadri ya uwezo wake. Kanyari amepuzilia mbali madai kwamba hakumpenda Betty, akisisitiza kuwa alimpenda kwa dhati hata baada ya wao kuachana. Amesema licha ya tofauti zao za kifamilia, alikuwa akimheshimu na kumtambua kama mama wa watoto wake. Mchungaji huyo amewataka watu kuacha kueneza maneno na mijadala kuhusu marehemu, akisema familia inapaswa kupewa faragha na muda wa kuomboleza kwa utulivu. Marehemu Betty Bayo alifariki dunia mnamo Novemba 10 katika Hospitali ya Kenyatta, ambako alikuwa akipokea matibabu baada ya kugunduliwa na ugonjwa wa damu aina ya acute myeloid leukaemia, wiki moja tu kabla ya kifo chake.

Read More
 Kanyari Akosolewa kwa Kutumia Kifo cha Aliyekuwa Mke Wake Kutafuta Kiki

Kanyari Akosolewa kwa Kutumia Kifo cha Aliyekuwa Mke Wake Kutafuta Kiki

Mjadala mkali umeibuka mtandaoni baada ya mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii kumshutumu Mchungaji Victor Kanyari kwa kutumia kifo cha aliyekuwa mke wake, mwimbaji wa nyimbo za injili Betty Bayo, kama njia ya kutafuta kiki. Taarifa hiyo imevutia hisia kali kutoka kwa Wakenya, wengi wakionesha kutoridhishwa na namna Kanyari ameonekana kujitokeza hadharani akionekana kulia na kushiriki kwa ukaribu katika maandalizi ya mazishi ya marehemu. Mtandaoni, watumiaji wengi wameeleza kuwa kitendo hicho hakifai kwani Kanyari na Betty walishatalikiana miaka kadhaa iliyopita, na marehemu alikuwa ameolewa tena na mwanaume mwingine. Wengi wamesema kuwa hatua ya Kanyari kuonekana kana kwamba anaongoza kamati ya mazishi inamvunjia heshima mume wa sasa wa marehemu. Mjadala huu umeendelea kuchukua nafasi kubwa kwenye mitandao, huku baadhi wakimtetea Kanyari wakisema ana haki ya kuomboleza kwa sababu walishiriki maisha na watoto pamoja, huku wengine wakisisitiza umuhimu wa kumpa familia nafasi ya kupanga mazishi kwa utulivu na heshima.

Read More
 Pastor Kanyari Angua Kilio Akiomboleza Kifo cha Betty Bayo

Pastor Kanyari Angua Kilio Akiomboleza Kifo cha Betty Bayo

Mchungaji maarufu wa Jijini Nairobi, Victor Kanyari, amezidi kugubikwa na majonzi kufuatia kifo cha aliyekuwa mke wake na mwanamuziki wa injili, Betty Bayo. Katika video zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii, Kanyari ameonekana akishindwa kujizuia kutokana na huzuni kubwa iliyompata baada ya kusikia taarifa za msiba huo huku wasanii na marafiki wa marehemu wakijumuika naye kumpa faraja.. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kanyari ameeleza maumivu yake kwa maneno yaliyojaa huzuni, akisema kwamba kifo cha Betty kimemuacha na pengo kubwa lisilozibika. Amesema msanii huyo ambaye ni mama ya watoto wake atabaki daima kuwa sehemu ya familia yake licha ya changamoto walizowahi kupitia pamoja kipindi cha ndoa yao. Mchungaji huyo mwenye utata, ameongeza kuwa ataendelea kubeba kumbukumbu, upendo na roho ya marehemu moyoni mwake, akimtakia pumziko la amani. Kanyari na Betty Bayo walikuwa wametengana miaka michache iliyopita kutokana na tofauti za kifamilia, lakini waliendelea kuwa marafiki na wazazi wenza waliokuwa na ushirikiano mzuri katika malezi ya watoto wao. Licha ya Bayo kuolewa tena, wawili hao waliendelea kushirikiana kwa amani katika kuwalea watoto wao, akiwemo binti yao Sky, ambaye Kanyari alimrejelea katika ujumbe wake wa rambirambi.

Read More
 Pastor Kanyari Aibua Mjadala kwa Kutoza Waumini Ada ya KSh300 ya Uanachama

Pastor Kanyari Aibua Mjadala kwa Kutoza Waumini Ada ya KSh300 ya Uanachama

Mchungaji mwenye utata Victor Kanyari amezua gumzo mtandaoni baada ya kutangaza kuwa waumini wa kanisa lake watalazimika kujisajili rasmi kwa ada ya KSh 300, ambayo italipwa kila mwezi ili kudumisha uanachama wao. Kulingana na tangazo hilo, waumini ambao hawatalipa ada hiyo hawatahesabiwa kama wanachama kamili wa kanisa, hali ambayo imezua hisia mseto kutoka kwa umma na wadau wa dini. Wapo wanaoona kuwa hatua hiyo ni aina ya biashara ya kiroho, huku wengine wakihalalisha kwa kusema ni njia ya kusaidia kugharamia huduma za kanisa. Hii si mara ya kwanza Kanyari kuzua utata. Mchungaji huyo amekuwa akihusishwa mara kwa mara na mbinu tata za uongozi wa kidini, ikiwemo madai ya kutumia miujiza bandia katika ibada zake za awali.

Read More