Peter Miracle Baby Afunguka kwa Uchungu Jinsi KRG The Don Alivyomdhalilisha Mtandaoni

Peter Miracle Baby Afunguka kwa Uchungu Jinsi KRG The Don Alivyomdhalilisha Mtandaoni

Msanii aliyegeukia muziki wa mugithi, Peter Miracle Baby, amefunguka kwa uchungu namna msanii KRG The Don alivyodhalilisha mtandaoni kwa maneno makali kipindi ambacho afya yake ilikuwa imedhoofika. Akizungumza kuhusu tukio hilo, Peter amesema kuwa alikuwa mlegevu na amelala kitandani hospitalini wakati KRG alipotumia maneno yaliyomuumiza kihisia na kumuathiri kisaikolojia. Amedai kuwa kipindi hicho alikuwa hana nguvu za kujibu wala kujitetea, jambo lililomfanya kuyaona maneno hayo kuwa ya kikatili na yasiyo na huruma. Hata hivyo, licha ya kukerwa na tukio hilo, msanii huyo amesema tayari amemsamehe KRG, akiwataka mashabiki waache kuendeleza uhasama au malumbano. Amefafanua kuwa hataki kubeba chuki kwa sasa kwani anataka kuzingatia afya na maendeleo ya maisha yake binafsi. Peter Miracle Baby ametoa kauli hiyo baada ya wafuasi wake kupuuzilia mbali azma ya KRG The Don ya kuwania kiti cha Useneta kaunti ya Nairobi kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2027 nchini Kenya. Wengi walidai kuwa msanii huyo hana sifa ya kuwa kiongozi kwa kutokana na mienendo yake ambayo wametaja kuwa ya kijeuri.

Read More
 Peter Miracle Baby Afichua Ukweli Kuhusu Mtoto wa Shalkido

Peter Miracle Baby Afichua Ukweli Kuhusu Mtoto wa Shalkido

Mwanamuziki Peter Miracle Baby, memba wa kundi la Sailors, amepuuzilia mbali madai kuwa marehemu Shalkido aliacha mtoto, akisisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli. Akizungumza kwenye mitandao ya kijamii, Miracle Baby ameonekana kukerwa na kitendo cha mwanamke mmoja kujitokeza mtandaoni na kudai alizaa mtoto na Shalkido, akisema madai ya mwanamke huyo hayana msingi wowote kwani anatumia jina la marehemu kutafuta kiki wakati familia bado ipo kwenye majonzi. Miracle Baby amesema kuwa kama kweli Shalkido angepata mtoto, basi bibi yao (Grandmother) angekuwa anafahamu hilo kwa sababu marehemu alikuwa karibu sana na familia yake. Pia amekiri kuwa Shalkido alikuwa na mpenzi enzi za uhai wake lakini walitengana muda mrefu kabla ya kifo chake, na hawakuwahi kupata mtoto kutokana na hali ngumu ya maisha waliyokuwa nayo wakati huo. Katika hatua nyingine amenyosha maelezo kuhusu picha inayoenea mtandao ikimuonyesha Shalkido akiwa na mtoto mchanga, akisema mtoto huyo si wake, bali ni wa dada yake ambaye alilelewa na bibi yao (Grandmother). Hata hivyo, amewataka walimwengu kuacha kueneza uvumi usio na msingi na kumruhusu Shalkido kupumzika kwa amani, akisisitiza kuwa kutumia jina la marehemu kwa kiki ni kukosa heshima kwa familia na marafiki waliobaki. Ibada ya wafu ya kumuaga msanii Shalkidoh inatarajiwa kufanyika leo katika kanisa la All Saints Cathedral, Nairobi, kuanzia saa 11:30 asubuhi. Ibada hiyo inatarajiwa kuwaleta pamoja wasanii, wadau wa muziki, na mashabiki wengi watakaoungana kumuaga Shalkido kwa heshima na upendo kabla ya mazishi yake Alhamisi Oktoba 16.

Read More
 CAROL KATRUE AMKIA KIFUA MIRACLE BABY KWA KUKIMBIA UJA UZITO

CAROL KATRUE AMKIA KIFUA MIRACLE BABY KWA KUKIMBIA UJA UZITO

Msanii wa Mugithi Carol Katrue amemkingia kifua mume wake Peter Miracle Baby kwenye sakata la kumpa uja uzito mrembo aitwaye Tash Baby. Kwenye mahojiano na Mungai Eve Katrue amekataa ombi la Tash Baby kutaka mume wake kufanya vipimo vya DNA kuthibitisha kama alizaa nae mtoto kwa kusema kuwa uja uzito wa mrembo huyo sio wa Miracle Baby bali ni wa jamaa aitwaye Lorenzo. Katika hatua nyingine amekanusha tuhuma za Peter Miracle Baby kumtelekeza baba yake mzazi kwa kusema kuwa wazazi wa mume wake huyo wanaisha maisha mazuri, hivyo stori za mwanaume aliyejitokeza juzi kati mtandaoni na kudai ni baba mzazi wa Peter Miracle Baby hazina ukweli wowote. Carol Katrue amesema stori za Baba Mzazi wa msanii huyo kuishi maisha ya taabu zilitungwa na ukurasa mmoja wa udaku kwenye mtandao wa Facebook kwa lengo la kujitafutia umaarufu.

Read More
 BABA MZAZI WA PETER MIRACLE BABY ALIA KUPITIA MAISHA MAGUMU, AOMBA MSAADA WA KIFEDHA

BABA MZAZI WA PETER MIRACLE BABY ALIA KUPITIA MAISHA MAGUMU, AOMBA MSAADA WA KIFEDHA

Wakati msanii Peter Miracle Baby anaendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa Mugithi, kumbe Baba yake mzazi hana makazi na anapitia maisha magumu sana mtaani. Kupitia video ambayo inasambaa mtandaoni Mzee David Ndolo maarufu Notorious, ameonekana mtaani akiomba msaada kwa kijana wake huyo ambaye hawana mahusiano mazuri. Mzee huyo amesema kuwa hafurahishwi kabisa na maisha anayoishi mtaani ambapo amemtaka Miracle Baby kuingilia kati na kumtoa kwenye maisha ya uchochole. “Niaje wathii, mi ndio baba Miracle Baby, anaitangwa Willy Mpole, nimemzalia hapa Mlango Mkubwa…Anaitangwa Miracle Baby Wilson … Mimi naitangwa David Ndolo … Mi ndio baba yake nimemzaa … siezi kubali hiyo maisha ju ni ya shida nay a kuteseka na kusononeka Zaidi,” alisema. Miracle Baby hata hivyo amejibu tuhuma hizo kwa kejeli kwa kuandika “Niseme Nini mimi willy mpole na msee mwingine asiniulize kuhusu babangu tena kwani coz sikujizaa mm na amjuae baba ya mtoto ni mama so io swali si yangu kujibu “

Read More
 PETER MIRACLE BABY AKANUSHA MADAI YA KUWA NA WANAWAKE WENGI

PETER MIRACLE BABY AKANUSHA MADAI YA KUWA NA WANAWAKE WENGI

Msanii wa Sailors Gang Peter Miracle Baby kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu tuhuma zilizokuwa zikimuanda za kuwatelekeza wanawake aliozaa nao. Katika mahojiano na Mungai Eve, Miracle Baby amekanusha madai ya kuwa na wanawake wengi kwa kusema kwamba wanawake wote waliokuwa wanadai amepata nao watoto kwenye mitandao ya kijamii walikuwa wanatumia jina lake kujitafutia umaarufu mtandaoni. Katika hatua nyingine amewajibu walimwengu waliokuwa wanadai kuwa amekaliwa sana na mke wake Carol Katrue kwa kusema kwamba madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa ni mapenzi ya dhati aliyonayo kwa mke wake ndio yamewafanya watu kuanza kumzungumzia vibaya. Utakumbuka kipindi cha nyuma wanawake mbali mbali  walijitokeza mtandaoni wakidai kwamba wana ujazito wa Peter Miracle Baby jambo ambalo lilipelekea mke wake Carol Katrue kurushiana maneno makali na baadhi ya wanawake hao kama njia ya kumkingia kifua mume wake.

Read More