Pia Ponds akiri kutumia pesa zote za akiba kwenye surgery ya jino

Pia Ponds akiri kutumia pesa zote za akiba kwenye surgery ya jino

Msaniii wa kike kutoka nchini Uganda Pia Ponds amekiri kutumia pesa zake za akiba kwenye shughuli ya kupata jino jipya baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani. Kwenye mahojiano yake hivi karibu Mrembo huyo amesema mchakato wa upasuaji wa kupata jino jipya nchini Kenya ulimgharimu pesa nyingi kiasi cha kutumia mirahaba ya wimbo wake Tupaate kufanikisha matibabu yake. Hitmaker huyo “sSlay Farmers” ambaye amekuwa akificha sana kwa umma amewataka mashabiki kukaa mkao wa kupokea ujio wake mpya ambao utakuwa wakitofauti kama alivyozoeleka kwenye muziki wake. Pia Ponds sio msanii wa kwanza kuweka maneno ya bandia nchini Uganda, kipindi cha nyuma tuliona msanii wa Swangz Avenue Azawi akifanya hivyo alipopata umaarufu kupitia wimbo wake wa “Quinamino”

Read More
 PIA PONDS AWAACHA MASHABIKI NJIA PANDA KUHUSU MWAANDISHI WA HITSONG YAKE “TUPAATE”

PIA PONDS AWAACHA MASHABIKI NJIA PANDA KUHUSU MWAANDISHI WA HITSONG YAKE “TUPAATE”

Female singer kutoka nchini Uganda Pia Ponds amewaacha mashabiki na maswali mengi kuhusu ni nani hasa alimuandikia wimbo wake wa “Tupaate”. Hii ni baada ya mrembo huyo kuibuka na kujinasibu kuwa yeye ndiye mwaandishi halisi wa wimbo huo kauli ambayo inakinzana na aliyoitoa mwaka wa 2021 aliposema kuwa msanii mwenzake Azawi ndiye alihusika kwenye uandishi wa ngoma hiyo ambayo inapatikana kwenye EP yake mwaka wa 2020 “Tupaate”. Mrembo huyo alienda mbali zaidi na kujinasibu kuwa yeye ni moja kati ya waandishi wazuri wa nyimbo wenye vipaji nchini Uganda. Utakumbuka wimbo wa “Tupaate” kutoka kwa Pia Ponds uliachia katikati mwaka mwa 2020 lakini ilikuja ikapata umaarufu Afrika Mashariki wakati video ya Mc Africa akiwa anavibe na wimbo huo iliposambaa kwenye mitandao ya kijamii. Ilikuwa ni mshangao kwa Pia Ponds kupata hitsong kwenye safari yake muziki ikizingatiwa kuwa wakosoaji wa muziki wake wamekuwa wakidai kuwa hana kabisa cha kuimba.

Read More
 PIA PONDS KUFUNGULIA MASHTAKA PROMOTA KWA KUMSUSHIA TAARIFA UONGO

PIA PONDS KUFUNGULIA MASHTAKA PROMOTA KWA KUMSUSHIA TAARIFA UONGO

Msanii wa kike nchini Uganda Pia Ponds amekanusha tuhuma zilizoibuliwa na promota kuwa alidinda kutumbuiza kwenye onyesho la mkesha wa mwaka mpya  lilofanyika jiji London Uingereza licha ya kulipwa pesa zote. Kupitia mitandao yake kijamii Pia Ponds amesema mapromota onesho hilo hawakumlipa pesa zake zote lakni pia walikwenda kinyume na maktaba walioweka kabla ya shoo. Hitmaker huyo “Tuupate” amehapa kumshtaki promota wa onesho hilo kwa kumharibia jina na tuhuma za uongo. Kauli ya Pia Ponds imekuja mara baada ya promota wa onesho hilo Richmond Promotions kudai kuwa mrembo huyo alisusia kutumbuiza kwenye onesho lao licha ya kulipwa pesa zake zote na hata kupewa kila kitu alichokuwa anahitaji. Richmond Promotions  alienda mbali zaidi na kusema yupo mbioni kumfungulia mashtaka Pia Ponds kwa madai ya kutoheshimu mkataba wao wa makubaliano kabla ya onesho kuanza.

Read More