Msanii wa kike nchini Uganda Pia Ponds amekanusha tuhuma zilizoibuliwa na promota kuwa alidinda kutumbuiza kwenye onyesho la mkesha wa mwaka mpya lilofanyika jiji London Uingereza licha ya kulipwa pesa zote.
Kupitia mitandao yake kijamii Pia Ponds amesema mapromota onesho hilo hawakumlipa pesa zake zote lakni pia walikwenda kinyume na maktaba walioweka kabla ya shoo.
Hitmaker huyo “Tuupate” amehapa kumshtaki promota wa onesho hilo kwa kumharibia jina na tuhuma za uongo.
Kauli ya Pia Ponds imekuja mara baada ya promota wa onesho hilo Richmond Promotions kudai kuwa mrembo huyo alisusia kutumbuiza kwenye onesho lao licha ya kulipwa pesa zake zote na hata kupewa kila kitu alichokuwa anahitaji.
Richmond Promotions alienda mbali zaidi na kusema yupo mbioni kumfungulia mashtaka Pia Ponds kwa madai ya kutoheshimu mkataba wao wa makubaliano kabla ya onesho kuanza.