Rayvanny akiri kukua kisanaa tangu aondoke WCB

Rayvanny akiri kukua kisanaa tangu aondoke WCB

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Rayvanny amesema tangu aondoke kwenye Label ya WCB amejihisi kukua Kimuziki na kwa sasa anawaza mambo makubwa zaidi. Akizungumza na mtandao wa Habari Leo, amesema changamoto anazokutana nazo pamoja na ushindani uliopo kwenye game ya bongo fleva, vimemkomaza zaidi. “Ukweli sijutii maamuzi yangu, zaidi napambana ili niweze kuwa mkubwa zaidi, sababu huku kila kitu wakuulizwa ni Mimi na sababu ndio Boss mkubwa ninayehusika na mambo yote ikiwemo kulipa wasanii na mengineyo.” amesema Rayvanny. Aidha amesema kwa jinsi anavyofanya vizuri katika game hiyo, anaamini mpaka kufikia mwaka ujao atakuwa miongoni mwa wasanii wakubwa nchini na wenye wafuasi wengi kuliko ilivyo hivi sasa.

Read More
 MBOSSO AFUNGUKA KUFANYA KAZI NA RAYVANNY

MBOSSO AFUNGUKA KUFANYA KAZI NA RAYVANNY

Hitmaker wa “Moyo”, Msanii Mbosso amefunguka uhusiano wake na Bosi wa Next Level Music Rayvanny. Katika mahojiano yake hivi karibuni Mbosso amesema licha ya Rayvanny kuondoka kwenye lebo ya WCB bado wana uwezo wa kufanya kazi pamoja kwani wao ni marafiki wakubwa. “Ni mwanangu, kwa hiyo inapokuja kazi ambayo natakiwa nifanye na Rayvanny lazima tufanye ni rafiki yangu, nakutana naye, anakuja ofisini tunapiga stori, yaani hakuna noma,” amesema Mbosso. Julai mwaka huu Rayvanny alijiondoa rasmi kwenye lebo ya WCB aliyoitumikia kwa miaka saba na kuelekeza nguvu zake katika lebo yake, Next Level Music ambayo inamsimamia msanii Mac Voice. Utakumbuka chini ya WCB Mbosso alimshirikisha Rayvanny katika wimbo wake uitwao Pakua kutoka kwenye albamu yake, Definition of Love huku Rayvanny akimshirikisha Mbosso kwenye ngoma yake, Zuena inayopatika kwenye albamu, Sound From Africa.

Read More
 RAYVANNY ATAJWA NA JARIDA MAARUFU LA FORBES

RAYVANNY ATAJWA NA JARIDA MAARUFU LA FORBES

Mwanamuziki na C.E.O wa record label ya Next Level Music Rayvanny ametajwa na mtandao maarufu wa Forbes Africa katika orodha ya wanamuziki 20 kutoka barani Africa wanaotabiriwa kufanya vizuri katika muziki wa Afrika (future of the african music). Rayvanny ametajwa kwenye orodha hiyo sambamba na wasanii wengine wakubwa afrika kama Diamond Platnumz Burnaboy, Davido, Wizkid, Angelina Kidjo, Black Cofee, Tiwa Savage na wengine. Orodha hii ya Forbes imetaja kuzingatia uwakilishi na uhusika wa wasanii husika katika matamasha na tuzo kubwa za muziki kama Grammy.

Read More
 NANDY AFUNGUKA KUJISIKIA VIBAYA RAYVANNY KUTOZWA FAINI YA SHILLINGI MILLIONI 2

NANDY AFUNGUKA KUJISIKIA VIBAYA RAYVANNY KUTOZWA FAINI YA SHILLINGI MILLIONI 2

Staa wa muziki kutoka Tanzania Nandy kwa mara ya kwanza amefunguka jinsi alivyojiskia baada ya kusikia msanii Rayvanny anatakiwa alipe kiasi cha pesa cha shilingi milioni 2 kama faini ya kutokufuata mikataba na lebo yake ya WCB. Kupitia mahojiano yake na Clouds Media Nandy amedai kuwa alifanya mawasiliano na msanii moja kwa moja na sio record label ya WCB baada ya taarifa za mwanamuziki huyo kujiengua kwenye record label hiyo, na alijiskia vibaya baada ya kusikia stori hizo japo kuwa hana uhakika nazo maana zimezuka tu mitandaoni. “Nimeziona hizo taarifa na nimejisikia vibaya maana nimeona kama mimi ndio niliosababisha hivyo lakini niliona katika instastory yake kuwa ameandika yeye ni msanii huru hivyo sikuamini kama kalipishwa maana si unajua tena stori za mitandaoni” Alisema Nandy. Utakumbuka baada ya Rayvanny kutokea kama surprise kwenye tamasha la Nandy Festival 2022 huko Songea nchini Tanzania na kuzuka stori mitandaoni kuwa lebo yake ya zamani ya WCB imemuhitaji kulipa kiasi cha pesa cha milioni 2kwa kosa la kukiuka mikataba walioingia kwa kwenda kutumbuiza katika tamasha hilo. Mbali na hayo amesema kwa sasa miongoni mwa vitu ambavyo havipendi ni pamoja na marafiki wa mume wake Billnass “Sipendi marafiki wa mume wangu na wanalijua hilo wananiambiaga mimba hiyo inakusumbua kuna muda napokea simu zake nawaambia muacheni analea mimba”

Read More
 RAYVANNY AJIBU KISOMI MADAI YA KUPIGWA FAINI NA WCB

RAYVANNY AJIBU KISOMI MADAI YA KUPIGWA FAINI NA WCB

Mwanamuziki wa Bongofleva Rayvanny ni kama amejibu yanaendelea mitandaoni kuhusu kupigwa faini ya shilling million 2 za Kenya na lebo yake ya zamani WCB. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Rayvanny amechapisha ujumbe unao wajulisha watu wake kuwa yeye ni msanii anayejitegemea na yupo katika management nyingine kama alivyo weka utambulisho wake katika mtandao wa instagram. “Hellow my people RAYVANNY ni independent artist ,chek my new management for all bookings details on my bio” ameandika Rayvanny Kwa mujibu wa taarifa zinazoendelea kushika kasi kwa sasa mtandaoni zinaeleza kuwa mwanamuziki ambaye anatajwa kutoka kwenye record label ya WcB Wasafi Rayvanny amekumbana na faini ya shilling million 2 kutoka WCB kwa kukiuka sheria na kanuni za mkataba. Taarifa zinadai kuwa sababu kubwa ni kitendo cha mwanamuziki huyo kuhudhuria tamasha la mwanamuziki mwenzake Nandy “Nandy Festival” mapema mwezi uliopita mkoani Ruvuma nchini Tanzania, kabla ya kukamilisha masharti yote ya kujitoa katika record label hiyo ya WcB Wasafi ikiwemo kulipa kiasi cha zaidi ya Million 40 za Kenya.

Read More
 RAYVANNY AONDOKA LEBO WCB INAYOMILIKIWA NA DIAMOND PLATINUMZ

RAYVANNY AONDOKA LEBO WCB INAYOMILIKIWA NA DIAMOND PLATINUMZ

Hatimaye msanii wa Bongofleva, Rayvanny ameiaga rasmi lebo ya WCB Wasafi ambayo alikuwa akifanya nayo kazi zake za kimuziki Kupitia ukurasa wake wa Instagram amemshukuru boss wa lebo hiyo msanii Diamond Platnumz kwa nafasi aliyompa. “Thank You wcb_wasafi ” – Ameandika Rayvanny ambaye hupenda kujiita Chui. Ikumbukwe, Rayvanny alisainiwa na WCB mwaka 2016, na tangu awe chini ya lebo hiyo ameachia ngoma nyingi, ikiwemo album moja pia ameacha alama ya mafanikio makubwa kama kushinda tuzo ya BET mwaka 2017, kutumbuiza kwenye tuzo za MTV EMA

Read More
 RAYVANNY AKIRI KUUMIZWA NA KITENDO VITU KUCHOMWA KWENYE VIDEO ZA NYIMBO ZAKE

RAYVANNY AKIRI KUUMIZWA NA KITENDO VITU KUCHOMWA KWENYE VIDEO ZA NYIMBO ZAKE

Nyota wa muziki nchini Tanzania, msanii Rayvanny amefunguka namna anavyoumizwa na kuchomwa kwa vitu kwenye video zake, na sasa ametoa agizo kwa director wake Eris Mzava kutoweka scene za namna hiyo kwenye video za nyimbo zake. Rayvanny amebainisha hilo kupitia insta story yake ambapo ameteketeza kwa moto gari aina ya Alteza kwenye video yake mpya ya wimbo wa ” Te Quiero” aliyomshirikisha Marioo. “Najua kweli ni uhalisia lakini hakuna scene imeniumiza moyo kama scene ya kuchoma gari. Director Mzava naomba tuishie hapa kuchoma choma vitu” ameandika Rayvanny Instagram. Ikumbukwe, hii inakuwa mara ya pili kwa boss huyo wa Next Level Music kuteketeza vitu kwa moto kupitia video zake huku akitumia gharama kubwa katika uandaaji.

Read More
 DIRECTOR JOOWZEY AKOSOA VIDEO YA I MISS YOU YA RAYVANNY

DIRECTOR JOOWZEY AKOSOA VIDEO YA I MISS YOU YA RAYVANNY

Moja kati ya waongozaji maarufu wa video za muziki nchini Tanzania Director Joowzey, ametoa maoni yake kuhusu video mpya ya “I Miss You” ya mwanamuziki Rayvanny. Joowzey ambaye ameongoza video za wanamuziki mbalimbali kama Whozu, Aslay ,na Mabantu, amedai kuwa kwa asilimia kubwa script na stori kuhusu video ni nzuri na vimefanyika kwa usahihi lakini upande wa rangi iliyotumika katika video hiyo haikua sahihi, hii ni kutokana na director Ivan aliyeongoza video hiyo kumtegemea mtu mwingine katika upande wa rangi. Kauli yake imekuja mara baada ya Rayvanny kujinadia kuwa video ya wimbo wake wa “I Miss You” aliyomshirikisha Zuchu ndio video ghali zaidi kuwahi kutayarisha nchini Tanzania ikizingatiwa kuwa ilimgharimu kiasi cha shillingi millioni 80 za Tanzania.

Read More
 RAYVANNY AKIRI VIDEO YA WIMBO WA I MISS YOU NDIO GHALI ZAIDI TANZANIA

RAYVANNY AKIRI VIDEO YA WIMBO WA I MISS YOU NDIO GHALI ZAIDI TANZANIA

Nyota wa muziki wa Bongofleva, Rayvanny amedai kuwa video ya wimbo wake, “I Miss You” ambayo ndio video yenye gharama kubwa zaidi miongoni mwa zile ambazo zimetengenezwa nchini Tanzania. Boss huyo wa Next Level Music (NLM) amesema hayo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram ambapo ameeleza, ametumia kipindi cha miezi mitatu hadi video ya wimbo huo aliyomshirikisha Zuchu kukamilika. Akifafanua zaidi kuhusu scene 3 za nguvu za video hiyo, Rayvanny amesema scene ya helikopta iliwatesa sana kwani kila ilipokuwa ikiruka iliwabidi kulipia kwani imeshutiwa vipande zaidi ya kimoja. Scene ya nyumba amesema ilibidi watengeneze nyumba na baada ya shughuli kuisha wakaichoma moto na Scene ya Train ameitaja kuwa pesa imetumika sana

Read More
 RAYVANNY AFIKISHA STREAMS MILIONI 100 BOOMPLAY

RAYVANNY AFIKISHA STREAMS MILIONI 100 BOOMPLAY

Nyota wa muziki wa Bongofleva Rayvanny anaendelea kugonga vichwa vya habari kuhusiana na STREAMS za kazi zake mtandaoni. Good news ni kwamba Rayvanny amefanikiwa kufikisha jumla ya STREAMS Milioni 100 kwenye App namba moja ya kusikiliza na kupakua muziki mtandaoni ya Boomplay Music. Bosi huyo wa lebo ya Next level Music anakuwa msanii wa kwanza Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kufikia idadi hiyo kubwa ya streams. Aidha, kwa Tanzania anayemkaribia Rayvanny kuwa na idadi kubwa ya streams ni Diamond Platnumz ambaye hadi sasa ana zaidi ya streams Milioni 90.3.

Read More
 RAYVANNY AWABARIKI MASHABIKI NA FLOWERS II EP

RAYVANNY AWABARIKI MASHABIKI NA FLOWERS II EP

Mshindi pekee wa tuzo ya BET Tanzania na Mkurugenzi wa lebo ya Next Level Music Rayvanny ameachia EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Flowers 2. Rayvanny ameamua kuwa surprise mashabiki zake kwa kuachia EP hiyo mpya yenye nyimbo tisa huku akiwa amewashirikisha wasanii mbalimbali kama marioo, nadia mukami, zuchu, ray c, guchi na Roki. EP hiyo ni muendelezo wa EP yake ya kwanza ya Flowers iliyotoka mwanzoni mwa mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya nyimbo 8. Lakini pia ni EP ya tatu kwa mtu mzima Rayvanny baada ya new chui ep aliyotoka,mwaka wa jana ikiwa na jumla mikwaju sita ya moto. Mpaka sasa Rayvanny ana jumla ya EP tatu na Album moja ambayo ni Sound from Africa iliyotoka mwaka huu 2021

Read More
 RAYVANNY ATANGAZA TAREHE RASMI YA KUACHIA FLOWERS II EP

RAYVANNY ATANGAZA TAREHE RASMI YA KUACHIA FLOWERS II EP

CEO wa Next Level Music na Member wa WcB msanii Rayvanny ameachia Track list ya , EP  yake iitwayo Flowers II’. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rayvanny ameshare artwork ya EP hiyo yenye Jumla ya Nyimbo 9 za moto ambapo amesema itaingia rasmi Sokoni Februari 10, mwaka wa 2022. Kwenye Followers II EP Rayvanny amewashirikisha wasanii kama Zuchu, Roki, Nadia Mukami, Marioo, na Ray C huku akisema kuwa EP hiyo ni zawadi maalum kwa ajili ya siku ya wapenda nao, Valentine’s day. EP hiyo itakuwa kama muendelezo wa EP yake ya kwanza ya Flowers iliyotoka mwanzoni mwa mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya nyimbo 8 ikiwemo HitSong yake ya “Teamo”

Read More